Kutapika Damu kwa Mtoto wa umri wa Miaka miwili tatizo nini?

Mtali

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
3,420
2,460
Ndugu wanajamii humu ni wiki moja imepita nimeshuhudia mtoto akitapika damu kwa wingi hadi niliogopa kwani sija wahi kuona tatizo kama hilo. Hivi tatizo hili linatokana na nini? Na matibabu yake ni yapi? Na matibabu yanapatikana wapi ndugu zanguni? Nahitaji msaada wenu kujua hili na kulishughulikia.
 
Wahi haraka hospitali. Kuna wakati mtoto anatokwa na damu puani ila anameza damu (usingizini) alafu akiamka anatapika damu. Ila anaweza kua na shida nyingine kubwa zaidi... pole sana.
 
Yani mkuu wiki moja imepita mtoto unatapika damu bado unaulizia matibabu yanapatikana wapi?

Hujui hospitali nini?

Please mpeleke hospitali mtoto na siku nyingine sio kutapika damu tu bali hata kuharisha damu ni lazima umpeleke mtoto hospitali haraka sana.

Tunaitaji kuelimishwa sana mambo ya afya, hii noma.

Kila la kheri, Mungu amsaidie mtoto apone.
 
Nashukuru kwa ushauri wenu nilifanikiwa kumtibu kwa wakati husika....... Hii thread nili ileta baada ya kutoka hospitali.... Nashukuru Mungu ali mnusuru katika hali hii..... Godbless U all.....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom