Kutangaza kuwa Serikali ya CCM sasa inatoa fedha kwa wamachinga ni Ushindi mkubwa kwao na kwa 'WASHIKADAU' wengine

Shoctopus

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
3,434
1,985
Asalam-aleikhum Wana-JF

Kwanza nawapongeza Rais SSH na viongozi wa Serikali ya CCM, hasa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala ambaye ameonyesha ujasiri mkubwa na mfano mzuri katika kutekeleza uamuzi wa Rais SSH wenye lengo la kubadili mfumo wa biashara ya umachinga kimazingira.

Tukumbuke kwamba hayati JPM aliwatambua wamachinga na kuwapa vitambulisho rasmi kabla ya Uchaguzi MKUU wa 2020, na kwa makosa makubwa, kuwapa ruksa ya kufanya biashara popote nchi nzima.

Kitendo hicho kiliwajengea wamachinga nguvu kubwa dhidi ya viongozi wa Serikali kuanzia serikali za mitaa hadi juu, pamoja na polisi katika kusimamia sheria za mipangomiji na usafi wa mazingira.

Na matokeo yake sote tunayaona; kwamba hadi leo wamachinga wenyewe na 'Uongozi wa Wamachinga' kwa pamoja wamekuwa moto wa kuotea mbali! Kwa maneno mengine hii ni "political pressure group" iliyopata mafanikio makubwa katika mazingira magumu kwa vikundi vingine rasmi vya kisiasa, kutokana na mbinu zinazotumiwa na CCM kuwaweka nje ya mfumo wa utawala.

Kwa vile "Serikali ya CCM" mbele ya wamachinga 'imesalim amri' na imetangaza kwamba sasa inatoa fedha kwa wamachinga; ni Ushindi mkubwa sana kwa kundi hilo la wananchi kisiasa!

Lakini pia ni ushindi kwamba na Fedha yao 20,000/- ya vitambulisho vya ujasiriamali imezaa' matunda makubwa sana na matamu sana! Kwasababu Serikali imewasikiliza na inaenda kuwasikiliza zaidi.

Kwahiyo kuanzia sasa tunaweza kusema wamachinga ni KADA isiyo rasmi ya CCM na tutegemee mambo kadhaa kutokea:

* Watamdai Rais awape viti maalum bungeni,

* Wanafungua ukurasa mpya wa muundo wa BUNGE kikatiba kama ifuatavyo:

1. Bunge la JMT kuwa "Bunge la Washikadau", badala ya bunge la majimbo ya uchaguzi kupitia vyama vya siasa.

2. Kwakuwa CCM imewasukuma nje ya mfumo wadau wa kisiasa kupitia vyama rasmi vya siasa; utegemee idadi ya "Washikadau" wengine wenye nguvu pia nje ya vyama rasmi vya siasa, kujitokeza kutokana na makundi yaliyopo ya wadau tarajiwa.

Kwamfano bodaboda, madereva, makondakta, wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimbaji wadogo wadogo nk.! Nyuma ya makundi hayo wapo NGO's, CBO's, wafanyakazi, waumini wa dini, walemavu, waganga wa kienyeji nk. ambao baadhi hawana platforms za uhakika kisiasa.

Swali fikirishi la kujiuliza ni kwamba kutokana na uzoefu tuliouona kwenye zoezi la wamachinga, wachimbaji wadogo wadogo, wakulima na wafugaji, kwa jinsi CCM inavyotaka kuwatumia kisiasa inabidi tujiulize:

Huko tuendako kati ya "CCM na serikali" na hawa (pressure groups) machinga na wadau wengine tarajiwa kama hao hapo juu; ni upande upi hasa utakuwa au wenye nguvu halisi sasa na mbele ya safari?

CCM katika kutafuta uhalali wa kisiasa baada ya kuharibu mfumo wa demokrasia na Uchaguzi Huru, ilishazoea kubuni na kuhodhi ajenda za 'makundi asilia' ya vijana, wafanyakazi, wanawake, wazee, wanafunzi nk. Kwahiyo sasa wanataka wafanye hivyo pia kupitia uchifu.

CCM inataka kubuni na kuhodhi ajenda za makabila kupitia "dhambi ya ukabila" (J. K. Nyerere).

Kwa kifupi mwelekeo huu kwenye 'Bunge la Washikadau' utakuwa mgeni hapa TZ. Lakini napenda kusema huu si mfumo mgeni kwa wenzetu.

Kwa mujibu wa katiba ya Austria Bunge lao ni Bunge la (stakeholders), Washikadau. Kwa maana kwamba wabunge wanachaguliwa kupitia wadau kama nilivyowataja hapa juu pamoja na vyama vya siasa vyenyewe!

Sio rahisi kwa wengi wetu kuuelewa mfumo huu wa Austria kutokana na tofauti nyingi pamoja na za kihistoria kati ya sisi na Austria.

Lakini ninachotaka kuweka mezani ni ni SWALI tu

Kwamba baada ya CCM kuvuruga mfumo wa Bunge la uwakilishi wa majimbo kupitia vyama rasmi vya siasa; na CCM yenyewe kuanza kusalimu amri kwa pressure groups au social groups kama wamachinga na huko mbele kulazimika kusalimu amri kwa makundi mengine ya kimkakati; tutegemee makundi hayo ambayo ni wadau wa kisiasa, kuendelea kuwekwa nje ya mfumo wa utawala hasa kupitia Bunge?

Nasema hivyo kwasababu kama lengo la CCM la kufuta mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa litatimia. CCM itake isitake 'makundi mkakati' inayoyalenga ili kuyabunia ajenda na kuyatumia kisiasa "mwisho wa siku" yatadai kushirikishwa kwenye mfumo wa utawala.

Na kwakuwa CCM imezoea kupitisha mambo yake kwa nguvu za polisi, na vyombo vya Dola, na kwakuwa katika suala la wamachinga CCM wamejifunza kwamba mbele ya makundi mkakati inayoyakumatia badala ya (au ku-side step) wapinzani wake.

Ni kwamba hatimae makundi hayo yanakuwa na nguvu dhidi ya viongozi wa Serikali na vyombo vya Dola.

Na ni wazi kwamba mbele ya safari CCM ijiandae kupokea ajenda za wadau kupitia mfumo mpya wa ushirikishwaji katika Bunge hilo jipya. BUNGE LA WADAU.
 
Pole yako, kikubwa ni lengo la kuwaondoa sehemu zisizoruhusiwa lishafanikiwa, hizo zako ni porojo tuu. Na kama ukipata hata senti tano kwenye hizo 5bl njoo hapa utuambie.
 
Mkuu unashangaa CCM kuwachangia wamachinga ambao wengi wana matatizo makubwa ya kimaisha, lkn hapo hapo ulishindwa kutushangaa sisi wananchi na wanachama masikini tuliokichangia chama chetu na mwenyekiti wetu mwenye mamilioni ya shilingi alizokusanya kutoka kwa wabunge waliokuwa wanakatwa kila mwezi, na hapo sijazungumzia ruzuku ya chama na misaada ya wahisani.

Kwahiyo na sisi tuseme ushindi umeenda kwa mwenyekiti na genge lake. Ama kweli wajinga ndio waliwao.

2528007_20200919_173148.jpg
 
Kuwapa pesa ni jambo moja na kuuza au bidhaa zao kupata soko ni jambo lingine

Unaweza mkopesha kisha ulipompeleka akakosa soko la bidhaa na kufilisika.

kisha kuanza kukimbia madeni sasa hapo unakuwa umemsaidia machinga au umemfanya kuwa adui wa mkopeshaji na serikari?

Jambo hilo lazima ufanyike utafiti wa kutosha kuliko kujipa sifa badae ikawa balaa.

Kumbukeni pia wamachinga wanategemea wateja wa kutoka nje ya nchi na wa kutoka mikoani sasa mtakapowaweka kutakuwa na hao wageni au ndo kutaka kuwafilisi kisha washuke mitaani kukaba watu?
 
Tukimwambia juzi kwamba machinga na boda boda bi mtaji mkubwa Sana kwenye siasa za Tanzania. Wakichelewa kuna mtu ndoto ya 2025 ataisikia tu
 
Back
Top Bottom