Kutana na Visa/Mikasa/Vioja na Mambo ya Wasichana wa kazi/Housemaids huyu wangu ni balaa

Kajinga sana hakajaomba dawa wamtoe kafara ndugu yao ili watajirike kanachukua dawa kugombanisha watu
 
wadau habarini za siku kadhaa.. nimeona niweze kushare nanyi mambo kadhaa kuhusiana na wadada wa nyumbani/wadada wa kazi/house maids n.k na pengine tuweze pia kushirikishana uzoefu mbalimbali kupitia JF na katika Thread hii.

toka nimeoa ni muda mrefu sana tumekuwa na wadada wa kazi wa aina tofaut tofaut na kutoka mikoa tofaut tofaut pamoja na dini. binafsi nimekuwa sijali suala la dini au kabila. hutoa uhuru pia wa kuabudu mtu ambaye ninaye kwa dini yake. mwezi mmoja uliopita nilipata dada wa kazi toka mkoani mtwara. siku ambayo amefika mimi sikuwepo kikazi kwa muda wa week moja zaidi mbeleni.

wife anashangaa kuwa baada ya siku ya kwanza na ya pili yule dada alimuuliza "humu ndani hamna baba" wife akamuuliza "we si ulisema unaishi na baba na mama yako huko kwenu?sasa huku umekuja tena kutafuta baba? " anasema akamwamwuliza "umekuja kutafuta baba au kufanya kazi?" yule binti aliinama kwa unyonge sana akajibu "kufanya kazi" basi wakaendelea ila inasemekana alikuwa so curious akiangalia picha za pale sebuleni na kuniona mimi.. wakati flani anakaa kutizama picha na akaja kumwuliza mtoto kuwa baba alienda wapi ndo mtoto kumwambia kuwa nilisafiri.

baada ya week nikarudi. kiukweli alifurahi sana..alinipokea kwa bashasha,nderemo na vifijo.wife anasema yule binti alianza kubadilika.kujipenda na kuwa kila napokuw sebuleni alikuwa anapenda kuja kukaa na kunitizama sana.binafsi sikuwa namtilia maanani.

jana wife wakati anapita nyuma ya dirisha lake anasema alisikia sauti ya kitu kinachomwa...hajui kama ni udi,ubani au sijui nini..hayuko familiar na harufu za vitu hivyo.ila alishtuka kidogo aliposikia jina langu linatajwa huku pia maneno kadhaa yakisemwa.anasema hilo lilimshtua sababu alitaka kujua huyo dada yupo na nani kule chumbani.hakuwa na mazoea ya kufungua mlango na inaonekana siku hiyo aliweza sikia mlango sababu yule dada alisahau kurudisha madirisha ya vioo ikawa imebaki nyavu tu hivyo harufu ikatoka nje.

aliposikiliza akasikia maneno mengi yakitamkwa na moja wapo ni kuwa mle ndani mimi na wife tuachane..halafu nimpende yeye aje awe mke wangu.alisikiliza sana na mwishowe zoezi lilipoisha wife alimtizama kupitia dirishani alimwona akiwa uchi anatokea kwenye khanga aliyokuwa amejifunika...mkononi ameshika karatasi na chini ana kama kibakuli cha udongo.

haraka akarudi ndani kwenda kusali na baadaye kumwita yule binti.baada ya muda akatoka sasa akiwa amevaa nguo.ndo kuanza kumhoji... baada ya kumhoji yule binti alizungumza yote. kuwa alipokuwa anatoka kwao mtwara aliambiwa na wazazi wake na shangazi zake kuwa anakuja mjini aje kupata mume mwenye pesa na mzuri amwoe.wakampeleka kwa mganga ambako alienda kutengenezewa ile dawa. masharti yalikuwa kuwa usiku aoge saa nne na asubuhi kabla hajaonana nami awe amejivukizia ile dawa na kuita jina langu mara 5. alindikiwa maneno kadhaa ya kiarabu kwa damu nyekundu ambayo kila anpofanya hivyo lile karatasi aliwekee kwenye ule moshi wa anachochoma.

then wakati wa kuandaa chakula akiandaa aweke na majivu yanayotokana na kipande kidogo cha lile karatasi hasa baada ya kujaza sehemu za wazi jina langu.so anachana sehemu flani anachomea udi/ubani halafu unga wake ananichanganyia kwenye chakula.ila nile mimi peke yangu tu chakula hicho.

nikakumbuka kuna siku niliona kuna kama majivu kwenye wali nikakataa kule wali na nilishangaa wali unakuaje na majivu wakati unapikwa kwa rice cooker.sikula...actually sikudhania ushirikina. na kuna siku kwenye mboga ya majani pia nlishindwa kula kutokana tu na kuwa iliungwa na nyanya nami sipendi mboga ya majani iungwe na nyanya. siku kadhaa nazo nilikataa kula nyama sababu ya nyanya na vitunguu kuonekana kwenye mboga binafsi huwa sipendi.nikamwambia wife sitaki dada anipikie.

jambo hili anasema lilimhuzunisha sababu mara zote tatu napokuja kula chakula cha usiku nagoma kula kwa sababu moja au nyingine.nakumbuka tu nlimwambia wife sipendi na sitak kula chakula cha yule binti maana si mpish mzuri. binti mwenyewe hakuwa mbaya au mchafu.amemaliza form four so anajua kujikeep clean and smart.mpaka perfume na lotion alikuwa anatumia.

akaongea mengi jinsi gani alikuwa ana nyunyizia dawa ya mafarakano ambayo hiyo ingefanya mimi na wife tufarakane halafu wife aondoke home.ila nimbakishe binti na hapo kwa kuwa tayari ninampenda basi nianze mahusiano naye. na kuwa ningempenda sana mpaka mwishowe kumwoa.wife nami tulimwita na kumwambia kama anataka kazi basi achome vile vitu vyake vyote aombewe then aendelee na kazi.alikataa kwa sababu kwa imani yake anasema haruhusiwi kuombewa sababu ana majini ambayo ni walinzi wake. tukamwondoa kwa amani akarudi kwao Mtwara.

wadau kumekuwa na mengi sana kuhusiana na wadada wa kazi . ni vizuri tukapeana uzoefu ili watu wengine pia waweze kujifunza kutokana na haya mambo. inawezekana kabisa mkaleta dada wa kazi na soon mkajikuta ndani hamwelewani.. ni ugomv kila mara , chuki kwa wana ndoa n.k hali hii wakati mwingine huchangiwa na hawa wadada.nlishawahi kuambiwa kuna watu wanakuwa na madawa ya namna hii ili wao wapendwe na mwishowe kuolewa.

utu wa mtu ni jambo muhimu sana. haya mambo uliyoandika hapa hayana cha zaidi zaidi ya kutweza utu wa mtu. kwamba kwa sababu amrkuja kwako kufanya kazi basi hana utu tena . wakati mwingine kuna taarifa zinatiwa chunvi sana. msichana wa kazi kuuliza hii nyumba haina baba wewe ukaelewa anakutamani!? mtu aliyezoea kupikia kuni kuingiza kipande cha mkaa kwenye wali sio uchawi mkuu ni mazoea na wqkati mwingine ni bahati mbaya tu. yani mtu atoke kwao hakujui humjui ajiandae kukuroga.
pamoja na usomi, usasa na utajiri wenu lakini jitahidini kuwatendea na kuwaona wengine sawa na nyie.
 
Mkuu kuwa makini sana,hapo kuna mambo mawili na yapo kama ifuatavyo
1.Yawezakuwa kweli housemaid wenu ana mambo ya kishirikina
2.Huenda wife wako ana mashaka na huyo housemaid so,ameona ni vyema amfanyie visa ili aondoke be care!
 
Daah, hatari sana!!
Tulikutana na binti mmoja wa Iringa ukiamka asubuhi kafanya kazi zote, kafua, kapiga deki, madirisha na milango imefutwa kwa ustadi mkubwa, uji wa mtoto umepikwa , vyombo visafi hatari ila mchana anajivuta vuta tu na kusinzia!!asubuhi sa moja kazi zimekwisha'' kasheshe kwa mtoto tangu binti aje mtoto anashtuka usiku analia usiku kucha!!kuja kuomba kwa Bidii tukafunuliwa ktk hilo, binti kumrejesha mtoto katulia.
***mabinti wengine wakitokaga kwao wanabeba na madawa ya kuwasaidia kazi ama kuwaita ndugu zao kimazingara kumsaidia kazi.
 
hakuna kitu kibaya sana kama kujisikia inferior. hili ni jambo baya sana. utakuwa na akili za kipuuzi kama utakuta kipande cha mkaa kwenye wali unaopikiwa na rice cooker ukasema ni kawaida tu... utakuwa taahira. mazoea ya ajabu mtu anapikia gesi au rice cooker then akatafute mkaa huko aweke ndani. inaonekana hujaelewa au una uelewa mdogo sana. kama nimeandika kwa kiswahili hiki chepesi na hujaelewa nitakuwa najikosea sana kusema niendelee kukujibu... ntakuwa sijitendei haki kabisa.

utu wa mtu ni jambo muhimu sana. haya mambo uliyoandika hapa hayana cha zaidi zaidi ya kutweza utu wa mtu. kwamba kwa sababu amrkuja kwako kufanya kazi basi hana utu tena . wakati mwingine kuna taarifa zinatiwa chunvi sana. msichana wa kazi kuuliza hii nyumba haina baba wewe ukaelewa anakutamani!? mtu aliyezoea kupikia kuni kuingiza kipande cha mkaa kwenye wali sio uchawi mkuu ni mazoea na wqkati mwingine ni bahati mbaya tu. yani mtu atoke kwao hakujui humjui ajiandae kukuroga.
pamoja na usomi, usasa na utajiri wenu lakini jitahidini kuwatendea na kuwaona wengine sawa na nyie.
 
Pole na hongera kwa mkeo hapo mkeo alikuwa anakuombea kwakweli na kuiombea ndoa yake
 
haya mambo wengi wanasimulia yapo.... kama mtu ana familia na amekuwa akitumia wadada zaidi ya miaka mitano wa aina tofaut ni rahisi kukutana na wadada wenye mambo maovu.
Daah, hatari sana!!
Tulikutana na binti mmoja wa Iringa ukiamka asubuhi kafanya kazi zote, kafua, kapiga deki, madirisha na milango imefutwa kwa ustadi mkubwa, uji wa mtoto umepikwa , vyombo visafi hatari ila mchana anajivuta vuta tu na kusinzia!!asubuhi sa moja kazi zimekwisha'' kasheshe kwa mtoto tangu binti aje mtoto anashtuka usiku analia usiku kucha!!kuja kuomba kwa Bidii tukafunuliwa ktk hilo, binti kumrejesha mtoto katulia.
***mabinti wengine wakitokaga kwao wanabeba na madawa ya kuwasaidia kazi ama kuwaita ndugu zao kimazingara kumsaidia kazi.
 
ha ha ha.. unajua ameshakaa nao sana anawafaham sometime. pia ana penda sana kunilinda nimeshagombana naye sana asinilinde hivyo ila hawezi jizuia..so ninapoguswa mimi ... anakuwa so mean.... ila nimemwelewa na tunaelewana.

wife wako yuko mean kishenzi. eti "baba si ulimuacha kwenu, umekuja kazini au kufuata baba"
 
Inategemea na mizimu ya kwenu, kama ipo fiti ujinga ujinga kama huo hauwezi kukupata kamwe.
 
ha ha ha.. unajua ameshakaa nao sana anawafaham sometime. pia ana penda sana kunilinda nimeshagombana naye sana asinilinde hivyo ila hawezi jizuia..so ninapoguswa mimi ... anakuwa so mean.... ila nimemwelewa na tunaelewana.
Hawezi kuacha kukulinda sasa hapo angepuuzia kila kitu kinge haribika mpaka mje kukaa sawa hakuna hata moja la maana
 
hakuna kitu kibaya sana kama kujisikia inferior. hili ni jambo baya sana. utakuwa na akili za kipuuzi kama utakuta kipande cha mkaa kwenye wali unaopikiwa na rice cooker ukasema ni kawaida tu... utakuwa taahira. mazoea ya ajabu mtu anapikia gesi au rice cooker then akatafute mkaa huko aweke ndani. inaonekana hujaelewa au una uelewa mdogo sana. kama nimeandika kwa kiswahili hiki chepesi na hujaelewa nitakuwa najikosea sana kusema niendelee kukujibu... ntakuwa sijitendei haki kabisa.

Kweli kabisa mkuu! yawezekana hajakuelewa!
 
Hatari sana,usiache kufanya maombi maana hujui hapo ameacha nini,na pia kama jina lako lilishatajwa inatakiwa liombewe ili lifutwe huko lilikoandikwa,vinginevyo mkuu unaweza kuanza kumsaka ili yatimie malengo yake...
 
Back
Top Bottom