Tairi bovu
JF-Expert Member
- Sep 28, 2017
- 3,063
- 2,983
najivunia sana kujibiwa na mtu mwenye uelewa mkubwa wa kiwango chako. japo nina uhakika kuwa hujui utofauti na sababu za utofauti uliopo kati ya mtu na mtu. kwakuwa wewe upo hivyo ulivyo unadhani watu wote wanapaswa kuwa hivyo. watu wanatofautiana sana sana na huo ndio ubinadamu wenyeye. mtoto aliyekulia mtwara hawezi kuwa sawa na aliyekulia iringa hata kama wote ni watoto vivyo hivyo kwa watumishi wa ndani hawawezi kufanana. kwa kujua hilo ndo mana kuna orientation kwa kila mtu anayeanza kazi eneo husika.utu wa mtu ni jambo muhimu sana. haya mambo uliyoandika hapa hayana cha zaidi zaidi ya kutweza utu wa mtu. kwamba kwa sababu amrkuja kwako kufanya kazi basi hana utu tena . wakati mwingine kuna taarifa zinatiwa chunvi sana. msichana wa kazi kuuliza hii nyumba haina baba wewe ukaelewa anakutamani!? mtu aliyezoea kupikia kuni kuingiza kipande cha mkaa kwenye wali sio uchawi mkuu ni mazoea na wqkati mwingine ni bahati mbaya tu. yani mtu atoke kwao hakujui humjui ajiandae kukuroga.
pamoja na usomi, usasa na utajiri wenu lakini jitahidini kuwatendea na kuwaona wengine sawa na nyie.