Kutana na ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia pamoja na maendeleo yake

KANYEGELO

JF-Expert Member
Nov 12, 2019
2,149
4,752
_*Sehemu ya pili.*_

2. Artificial human being

Tangu dunia ianze haijawahi kutokea kipindi ambacho wanadamu wameenda extra mile kama kipindi hiki, tumefikia hatua ya kushindana na Mungu kuumba. Hata kama haupendi au hautaki, tayari kuna watu wameshafika huko, na miaka ya usoni tutarajie wajukuu zetu kuundwa maabara from scratch.

March 2017 wanasayansi ya chuo cha Cambridge waliweza kuunda kiinitete (embryo) ambacho kilidevelop ndani ya 3D scaffold na kuweza kubehave kama human embryo. Haya ni mapinduzi makubwa ktk sayansi ya bioengimeering.

Wanasayansi hao kwasasa wanatafiti juu ya kuweka uhai ktk kiinitete hiko, mwisho wa kila kitu tutashuhudia kiumbe hai aliyetengenezwa maabara, na baadae mika kama 20 au 30 tuone mwanadamu wa kwanza wa maabara atakuaje.

Tayari tuna uwezo wa kuunda viungo vya ndani from scratch, ubongo, moyo, mapafu, ini, figo nk. Teknolojia ya CRISPR imewezesha kampuni ya eGenesis kutengeneza genetic engineered pigs ambao viungo vyao vya ndani vinaweza kuwa transplanted kwenda kwa binadamu bila madhara yoyote kiafya.

Trust me, tutafika ulimwengu ambao mtu anachagua kuwa na mapafu kama ya muogeleaji mashuhuri Phelps ama moyo kama wa mwanariadha Usain Bolt ama ubongo kama wa Prof Steve Hawkings. Cha ajabu viungo hivi haviwezi kushambuliwa na bacteria ama virusi wala uvimbe wa tumor unaosababisha kansa.

Tumeona mwaka jana kampuni ya Organovo ya San Diego walianza kuuza 3D bioprinters za kwanza zenye uwezo wa kuchapisha viungo vya binadamu. Mwishoni mwa mwaka jana tukaona kituo cha utafiti cha Wake forest wameweza kutumia mashine hizo kutengeneza ngozi, misuli,mishipa ya damu na vibofu. Figo waliyoitengeneza imeweza kufanya kazi kwa ufanisi wa juu sana kwenye mwili wa mnyama wa majaribio. Cha ajabu zaidi unatumia dakika 40 kuprint kiungo, yani kama vile mtu anachukua selfie.

Wanasayansi wanamalizia utafiti ambao utawezesha wanadamu wa kawaida kuishi miaka 150.

3. Afya, dawa na matibabu

Hii sekta inakua kwa kasi isiyo ya kawaida, kuna mapinduzi mengi tyr tumeshuhudia na tutarajie kuona maajabu miaka 10-20 ijayo. Acha niorodheshe chap chap baadhi ya vitu tulivyoachieve mpk sana.

(a). Intelligent knife (iKnife)

Watafiti wa tiba wa chuo cha imperial tayari wamegundua na kufanyia utafiti kisu janja cha iKnife. Kisu icho kinatumia teknolojia ya electrosurgery, wakati kinatumika kwenye upasuaji umeme hupita kwa kasi na kuleta joto kwenye tishu za mwili, huku ikiwa na faida ya kupunguza upotevu wa damu, husababisha tishu hizo kutoa mvuke unaoambana na moshi, moshi hua unanyonywa 1 kwa 1 ka kuingia kwenye 'mass spectrometer' kisha kifaa hiko hutoa signals kueleza magonjwa yaliyopo kwenye mwili wa mgonjwa. Zoezi hili hadi kukamilika ni chini ya dakika 10 tu. Ndipo tulipofika huku, mwaka jana wale vijana wa Taiwan walishinda tuzo ya x prize baada ya kugundua kifaa walichokiita Dexter chenye uwezo wa kudetect magonjwa 13 bila haja ya kumuona daktari.

(b). Google brain

Hii nimeizungumzia kidogo lkn kwenye Artificial intelligence, lkn ngoja nitilie msisituzo tena. Google kama Google walimkodi Prof Ray Kurzeil (huyu naweza kusema ndio futurist maarufu zaidi duniani kwa sasa - unaweza kutazama ted talks zake kama getting ready for hybrid thinking). Google brain ni concept ya kuUpload ubongo wa binadamu kwenye computer ili kuweza kutufanya tuishi kidigitali. Kwa mantiki hiyo ubongo wetu utaunganishwa na kompyuta, kisha App ya kuchunguza mwili itakua installed kwenye kompyuta, huvyo kuufanya ubongo kuweza kugundua hali ya afya ya mwili muda wowote ule bila haja ya kumuona daktari... Lets see how fast this might happen, still crossing my fingers.

(c).Tricorder

Dunia inapoelekea yawezekana kusiwe na umuhimu wa kuwa na maabara, madaktari nk. Vifaa kama tricorder vinabadili kabisa jinsi tunavyopata huduma ya afya na matibabu. Mwaka jana tricorder ya kwanza ililetwa kwenye uso wa dunia, kifaa hicho kimeundwa na darubini kali (high power microscope) na simu janja (smart phone), hivyo unaweza kupima magonjwa ya ngozi kutumia tu fingerprint scanner ya simu, unaweza kupima DNA nk. Kifaa hiki bado kinaendelea kusukwa na naamini miaka 10 ijayo hakitakua kama kilivyo leo. Sasa najiuliza physicial, dentist, optician, medical doctor, clinician na manesi watakua na kazi gani hivi vifaa vikiwa yebo yebo.

(d). IBM Watson

IBM baada ya kuunda deep blue iliyomgaragaza bwana Garry, sasa waliamua kutumia muda wao kudesign vitu ambavyo vina tija za moja kwa moja, wana hiki kifaa chenye uwezo wa kung'amua magonjwa kwenye mwili wa mwanadamu bila kufanya vipimo, tena kwa accuracy ya juu kuliko madaktari.
Uwepo wa vitu kama smart contant lens yenye uwezo wa kusimamia magonjwa kama kisukari, kansa na BP vinatuonesha dunia itafananaje miaka 10 ijayo.

Mwaka jana pekee kifaa cha Da Vinci Robot kimefanya upasuaji milioni moja na nusu kwa ufanisi wa asilimia mia bila daktari kusika hata mkasi mmoja.

4.Sector ya Usafiri

Tumeona maendeleo makubwa sana ktk hii sekta, kuanzia enzi za kina nabii Nuhu na Ayubu kutumia farasi hadi , hadi kizazi cha kutumia 4 wheel chariots, hadi mnamo mwaka 1885 ambapo Karl Benz aligundua gari la kwanza, kisha 1905 Wright brothers wakaufundisha ulimwengu jinsi ya kuunda na kurusha ndege. Hapa kati kumekuwa na maboresho mengi sana ktk sekta ya usafiri, lkn bado wanasayansi wamekuwa na kiu kubwa sana ya kuja na teknolojia za kibabe zaidi.

Tumeona ujio wa segway human transporter, tena zimekuja kwa kasi ya ajabu sana. Naamini kabisa miaka 20 ijayo segways zitakua tofauti sana na hizi za leo. Achilia mbali selfdrive cars, hiyi ni kitu ambayo ipo na itashika kasi siku si nyingi sana, na nina imani watoto na wajukuu zetu wataishi katika kizazi ambacho kuondesha gari ni kosa la jinai. Kama asili itaturuhusu kuishi miaka 20 kutoka leo, tutegemee yafuatayo

(a). Hyperloop

Bado hua sina uhakika kama Elon Musk ni mwanadamu mwenzetu ama ana genes za eliens, sielewi!!. Tangu alivyopropose concept ya hyperloop mwaka 2012, mambo yamekuwa moto. makampuni mengi makubwa kama Virgin, Transpod, Arrivo, hyper chariot nayo yameingia kwenye challenge ya kudevelop hyperloop ya uhakika zaidi.

Hii kitu tayari ipo na tuitegemee very soon, najiuliza tu hali itakuaje miaka ya baadad. Aug 28 mwaka jana Elon Musk alipost video kwenye page yake ya IG kuonesha jinsi Hyperloop WARR pod inavyokata upepo na katika 1 ya comments zake alieleza kua ile ni sample ya hyperloop iliyoundwa na mwanafunzi tu wa Tesla tena kwa bajeti ndogo sana, fikiria nini kitatokea katika project kubwa na ambago imetengewa bajeti nono.

Kiufupi hyperloop ni mfumo wa usafirishaji ambao pods ama kontena zilizoungwa na sumaku zinaweza kusafiri kwa kasi kubwa sana ndani ya tubes ama mifereji tupu (vacuum tunnels). Hyperloop inaweza kusafiri kwa speed ya kilomita 1200 kwa lisaa. Sawa na kutumia dakika 52 kutoka Dar - Mwanza.

Tayaru tunnels kadhaa zimeundwa kuikaribisha hiyo teknolojia mfano Vienna - Budapest, Estonia - Finland, Helsinki - Stockholm, Spain - Morocco, Abudhabu, Liverpool - Glasgow, Poland, Cardiff - Glasgo, Germany, US nk. Tayari tumeona hyperloop 1, hyperloop Delft pamoja na Hardt hyperloop, hivyo tutegemee kuona mapinduzi makubwa zaidi na zaidi.

Najiuliza hizi elimu zetu za vyuoni za uhandisi, je wahandisi wetu wataweza kwemda sambamba na hii kasi? Au tunachomeshana tu mafuta?

*_Itaendelea._*

sent from toyota Allex
 
Back
Top Bottom