Kutana na Mmasai aliyekimbia mifugo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutana na Mmasai aliyekimbia mifugo

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Apr 13, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  <table align="right" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0" width="310"><tbody><tr><td class="formStyle" align="left" valign="top">
  </td> </tr><tr><td><table align="left" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0" width="99%"><tbody><tr><td class="Headline" align="left" valign="top">


  </td> </tr> <tr> <td class="kaziBody" align="left" valign="top"> <table align="right" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0" width="310"> <tbody><tr> <td align="right" valign="top"> [​IMG]
  </td> </tr> <tr> <td class="formStyle" align="left" valign="top"><table align="right" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0" width="98%"> <tbody><tr> <td class="formStyle" align="left" valign="top">
  </td> </tr> </tbody></table>
  </td> </tr><tr> <td><table align="right" bgcolor="#eaedff" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0" width="98%"> <tbody> <tr> <td class="Marquee" align="left" valign="top">
  </td> </tr> </tbody></table></td> </tr> <tr> <td>
  </td> </tr> </tbody></table> WAMASAI Bongo wamekuwa wakifahamika kwa umaarufu katika shughuli za ulinzi na ususi katika miaka ya karibuni, ingawa kiasili wanafahamika zaidi kwa ufugaji Tanzania.

  Lakini ukweli ni kwamba Wamasai sio maarufu kwa shughuli hizo pekee, kwani wapo ambao wamepiga hatua kubwa hata katika michezo.

  Mchezaji gofu wa kulipwa nchini Olais Mollel kutoka Klabu ya Gymkhana Arusha (AGC) ni miongoni mwa Wamasai ambao wamepata mafanikio katika mchezo wa gofu na kuiletea heshima Tanzania.

  Lakini haikuishia kwa huyo kwani sasa ameibuka Mmasai mwingine Michael Makala ambaye amepania makubwa katika mchezo huo, ingawa swali ni je, ataweza kufikia angalau historia ya Mollel?

  Makala, ambaye amechaguliwa kwenye timu ya taifa ya gofu Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka huu, alifanya mahojiano na HabariLeo hivi karibuni na kuelezea mtazamo wake katika mchezo huo.

  Mchezaji huyo ambaye alizaliwa Arusha mwaka 1978 akiwa mtoto wa nne kwenye familia yao, anasema amefarijika mno kuchaguliwa kwenye timu ya taifa.

  Yeye na wenzake saba watakuwa na mtihani wa kupeperusha vema bendera ya Tanzania kwenye michuano ya kanda ya Sita Afrika itakayotimua vumbi kuanzia Aprili 12 hadi 16 Gaborone, Botswana.

  “Kwanza kabisa nimefurahi kuitwa timu ya taifa ingawa naamini kwamba huo ni mtihani mkubwa. “Kwa sababu lengo la kila mchezaji ni siku moja kuchezea timu ya taifa, haya nahesabu ni mafanikio yangu makubwa katika miaka yangu 12 ya kucheza gofu,” anasema.

  Makala anaongeza kwamba yupo tayari kujituma na kuhakikisha anatoa mchango mzuri kwa timu Botswana ili kupeperusha vema bendera ya Tanzania.

  “Nafahamu nimeitwa kwenye timu kutokana na kiwango kizuri, ni kweli hata binafsi najiamini zaidi kwa sasa na nimebadilika mno, ingawa bado kuna matatizo kidogo ambayo yanaweza kurekebika ili kuimarika zaidi.”

  Anasema chini ya kocha chipukizi Farayi Chitengwa kutoka Zimbabwe anaamini wachezaji wa Tanzania watanufaika kwa kipindi watakachokuwa naye.

  “Chitengwa ni kocha mzuri, ni mtu ambaye anafahamu haraka tatizo la mchezaji na hilo ni jambo muhimu,” anasema Makala ambaye sio muongeaji.

  Anaongeza kuwa Chitengwa atakuwa msaada mkubwa kwake na wengine kutimiza ndoto zao katika mazingira magumu ya kuendelea kimichezo Tanzania.

  Akimuelezea kocha wa zamani wa taifa Mkenya Charles Farrar, Makala anasema hana maoni zaidi kwa sababu hakuwa chaguo la kocha huyo. “Unajua Farrar tulikuwa naye kwa miaka miwili hapa Dar (2007 na 2008) lakini sio wote tuliobahatika kuingia kwenye programu yake kwa hiyo ilikuwa vigumu kunufaika.”

  Makala mwenye umri wa miaka 32 anasema alianza kucheza gofu mwaka 1998 kwenye Klabu ya TPC Moshi. Lakini anasema baadaye alihamia Dar es Salaam mwaka 2004 na kuendelea kujishughulisha na mchezo huo akifanya kazi ya usaidizi wa wachezaji gofu (Caddy) kwenye klabu hiyo kabla ya kuwa mwanachama wa Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam (DGC) mwaka jana.

  Anasema alivutiwa na mchezo huo kutokana na marafiki zake waliokuwa wakicheza kwenye viwanja vya TPC Moshi. “Niliona rafiki zangu wanacheza nami nikavutiwa kujiunga na kweli naupenda mchezo huu,” anasema.

  Makala anaongeza kuwa amekuwa akicheza na wachezaji wa zamani wa timu ya taifa Yassin Salehe na Hassan Kadio ambao kwa sasa ni wachezaji wa kulipwa DGC tangu akiwa TPC. Akieleza sababu ya yeye kuchelewa kuingia kwenye ngazi ya taifa kama wenzake anasema katika maisha kila mmoja ana bahati yake.

  “Unajua mnaweza kuwa pamoja, lakini mwenzako anaweza kuwa na bahati ya kufanikiwa haraka, muhimu ni kufika unakotarajia.”

  Hata hivyo, alikiri mgumu wa maisha na uwezo wa kifedha ni moja ya sababu zilizomchelewesha au kumrudisha nyuma na ni hali inayowakabili wachezaji wengi.

  Anasema malengo yake ni kuwa mchezaji wa kulipwa baadaye kiwango chake kitakapoimarika zaidi. Alipoulizwa iwapo anafahamu ugumu wa kuwa mchezaji wa kulipwa katika nchi kama Tanzania kwa kuangalia mifano ya waliomtangulia anasema: “Kila kitu kinawezekana ukiwa na malengo na kujituma, naamini ukiwa na mchezo mzuri lazima utafanikiwa.”

  Akielezea baadhi ya mafanikio ambayo amepata katika mchezo wa gofu ni kushinda michuano mbalimbali ya taifa na klabu ikiwepo ya Lugalo Open mwaka 2007, Northern Province Open na Match Play mwaka 2009.

  “Yapo mafanikio mengi na hayo ni baadhi tu ya yale niliyofanikisha katika mchezo.” Kwa upande wa matatizo anasema ni ya kawaida, lakini zaidi ilikuwa ni vifaa ambavyo kwa sasa sio tatizo tena.

  “Tatizo langu kubwa lilikuwa vifaa, lakini tayari Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU), Dioniz Malinzi amenipatia hivyo, ndio sababu sasa hata mchezo wangu unabadilika.”

  Makala, ambaye alimaliza shule ya msingi mwaka 1995 Langasani Moshi na baadaye kuchukua mafunzo ya ujenzi VETA Moshi anasema bado ana hamu ya kurudi shuleni pamoja na kuweka mtazamo kwenye gofu.

  Amewashauri wachezaji wenzake kuwa makini na kujituma kwenye mazoezi iwapo wanataka kufanikiwa.

  </td> </tr> <tr> <td class="Text" align="left" valign="top">
  </td></tr></tbody></table></td></tr><tr><td>
  </td></tr></tbody></table>
   
Loading...