barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,863
Huyu bwana mdogo ni mtoto wa Garang,Juzi kati amefukuzwa kwenye kikao cha baraza la mawaziri la Sudan Kusini baada ya kuingia akiwa amevaa swag zisizo na hadhi ya Uwaziri.Rais akamtimua toka kwenye kikao,dogo alivyotoka nje akawambia waandishi kuwa "badala Rais azingatie ukosefu wa mafuta Sudan Kusini mpaka watu wanapata shida,ye anaangalia mavazi yake".Kapewa Uwaziri wa Wizara ya Maji.
Hapa chini ni Mike Sonko kaandika leo hivi
Ladies and gentlemen, introducing the current Minister for Water Resources and Irrigation in the Republic of South Sudan, Hon Mabior Garang De Mabior, son to Former President, Dr Garang... He is serving in the Unity government courtesy of Dr Riek Machar. All the best Mheshimiwa.... We are African and Africa is our Business..
=========================
Waziri mpya wa maji nchini Sudan Kusini katika serikali mpya ya umoja amedai kwamba alifurushwa katika mkutano wa baraza la mawaziri kutokana na 'bow tie' yake.
Mabior Garang De Mabior alichapisha picha yake katika mtandao wa Facebook iliokuwa na maelezo yafuatayo:Nawasili nyumbani baada ya kufurushwa na rais Salva Kiir katika kikao cha baraza la mawaziri kwa kutovaa inavyohitajika.
Aliandika:Baada ya kurudi nyumbani na kubadilisha ''bow tie'' yangu kutokana na ushauri wa makamu wa rais Riek Machar nilirudi katika kikao hicho kabla ya walinzi wa Salva Kiir kunizuia kuingia.
Garang baada ya kubadilisha na kurudi katika kikao hicho
Bw Mabior ambaye ni mwandani wa aliyekuwa kiongozi wa waasi Riek Machar baadaye alisema hivi:
Ni lazima waelewe kwamba serikali hii ya umoja haitakuwa kama ilivyokuwa awali.Mabadiliko yamekuja.
Serikali ya umoja iliapishwa wiki iliopita kulingana na makubaliano yaliolenga kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza Disemba 2013.
Chanzo: BBC