Kutana na ‘Jeshi la Machinga’ lisilo na silaha linavyoitetemesha Serikali hadi inajificha uvunguni

Wana Jf,

Ukisikia kila mkoa una majeshi ya serikali, lakini jeshi butu lisilo na siraha wala chombo chochote hatarishi, jeshi la machinga lilijijengea nguvu za kutisha kiasi kwamba linaogopeka sana.

Jeshi hili nimeshuhudia pale Kariakoo wakiondoa magari yanayoegeshwa kwa ajili ya parking system watumishi wakitishiwa na wateja wa maduka wakiondoa garibaldi nao. Ukikaidi kuondoa basi kama tairi haitatatobolewa basi utakuta hakuna upepo.

Jeshi la machinga limethubutu kuifanya mwendokasi akifika maeneo yao atembee mwendo wa kinyoga sana huku akiwakwepa kwa umahili. Tanesco wanashangaa nguo kupangwa kwenye transforma

Tanroads hasa ndio kabisa nguzo za kuongozea taa zinazibwa.

Hivi hawa wanaodaiwa ndio wapiga kura hivi ndio walipa kodi wakubwa kiasi hicho cha kupendelewa?

View attachment 1941877
Nimatokeo ya Sera mbovu 'ineffective policies"
 
😁😁😁
AMK5Se.png
 
Uchungu walionao wafanyabiashara tunatengeneza bomu la kukosa kodi. Kuwepa kodi rukusa kwa machinga lakini kwa wafanyabiashara halali mateso
 
Machinga ni wale wanatembeza bidhaa ambazo zinatumika in an instant kama vile soft drinks, bites , handkerchief, miwani, saa, earphones.
Lakini sasa unakuta mtu anauza vyombo, mashuka, nguo, viatu, matunda ya kwenda kumenya nyumbani, mama ntilie, mafundi simu/ pc n.k na ameweka kibanda cha kudumu kwenye eneo la barabara dah! Sababu ya ushenzi wa siasa.
Umachinga unapaswa kuwa kama ule wa Bakhresa kuwanunulia watu wake vibaiskeli vya kuuza ice cream na vibegi vyenye coolbox vya kuuza 'ukwaju', hii ya mabanda barabarani na kwenye mitaro ni uchafu!!!
Kweli kabisa uchafuzi wa ujenzi wa vibanda haufai. Mamantilie maji wanayooshea vyombo ukiona inaweza itapike
 
Shida ipo kwetu sote. Tunapenda vitu vya chini, bei ya chini, sarurasarura. Wamechinga wanaenda nasisi.
Anayewaterea machinga pia anawafurahisha wateja wao.
Wake up!

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Wamachinga wanapewa super power kuliko intellectuals? Kioja sana hiki...Graduates almost 250,000 wanamwagwa mtaani kila mwaka sidhani hii number ni ya kupuuzwa!
Mkuu, sasa kati ya haoe machinga walioamua kutumia mtaji kiduchu walionao kujitafutia kipato kidogo na hao unaowaita graduates ( waliobweteka nyumbani) wanaoisubiri serikali iwape ajira nani asaidiwe?.

Alafu husichokielewa Kuna idadi kubwa sana ya Graduates ambao ni machinga.

Serikali haijawaajiri, haijawatengenezea mazingira wezeshi ya kujiajiri kibiashara rasmi na imeamua kuwafukuzia mbali kutoka maeneo yasiyo rasmi ambayo walijiingiza kwenye umachinga.

Tujiandae kuwa na wimbi kubwa la vibaka,wezi,machangudoa na mateja.
 
Kweli kabisa uchafuzi wa ujenzi wa vibanda haufai. Mamantilie maji wanayooshea vyombo ukiona inaweza itapike
Machinga ni kundi muhimu sana kwenye jamii na uchumi wa nchi, lakini wanapaswa kufanya biashara zao kwa utaratibu mzuri wasilete kero kwa watumiaji barabara na miundombinu mingine. Machinga wapo wengi tu marekani na ulaya pia, ila wanafanya biashara zao kwa utaratibu!
 
Unawamwambafai tu mbina sehem kibao wanakomaliwa na hawapangi biashara? wakikikuta tehe tehe ndio wanapanga mbele yabeneo lako au maferem.
 
Back
Top Bottom