Kutana na James Hobson, Injinia anayetengeza characters wa Marvels & DC Comics, video games kuwa halisia

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,432
105,854
Salute..



Anaitwa James Hobson a.k.a Hacksmith ni Injinia,mbunifu na mtengenezaji wa video za YouTube. Hua anachukua idea za uongo kutoka kwenye Video games, movies na Comics mbalinbali. Huyu jamaa hua anatengeneza yale tunayoyaona kwenye movie za avangers,X man, Star war, na games mbalimbali na kutengeneza mfano wake (replica).
Katengeneza vitu hivi
  • Suti ya Iron man
  • Ngao ya Captain America ambayo ina electromagenetic anaweza kuivuta popote,pia suti yake
  • Makucha ya X man ambayo yanazama ndani na kurudi nje
  • Psylocke's psionic Sword (X man Apocalypse)
  • Lightsaber ya kwenye Star wars.
Nyundo ya Thor god of Thunder
Huyu jamaa kavunja rekodi kabisa baada ya kutengeneza replica ya nyundo ya Thor ambayo anaweza kuinyenyua yeye pekee yake. Kaiwekea Electromagenetic na fingerprints scanner ambayo inamwezesha kunyenyua hiyo nyundo yeye pekee tu.

Huyu jamaa namfananisha na mtaalamu wa uvumbuzi Thomas Edison ambae alimfundisha mke wake wa pili Morse Code ili wawe wanawasiliana kwa ishara ya vidole pindi wazazi wa mke wake wakiwepo.


>>>Morse code is a method of transmitting text information as a series of on-off tones, lights, or clicks that can be directly understood by a skilled listener or observer without special equipment. It is named for Samuel F. B. Morse, an inventor of the telegraph.

Au nimfananishe na bwana Kim ung-yong ambae aliweza kuongea lugha 4 alipokua na miaka 2, aliweza kufanya hesabu za aljebra akiwa na miaka 3, alialikwa wanafunzi wa fizikia chuoni alipokua na miaka 4, alialikwa Marekani kwenye kitengo cha NASA akiwa na miaka 7, alipata PHD yake akiwa na miaka 15, alikua na IQ ya 210.

Ikumbukwe mimi nilipokua nina miaka 15 nilikua najifunza jinsi ys kujibu kitabu cha Mabala the Farmer.

Mnaweza kumuangalia Youtube na Facebook huyu Hacksmith muone kazi zake.


Ma-Injinia wa Tanzania upande wa Teknolojia mna lipi la kujifunza toka kwa huyu mbunifu?

The Hacksmith
Tchao

Da'Vinci.
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom