Kutana na James Hobson Injinia anayetengeza characters wa Marvels & DC Comics, video games kuwa halisia


Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
19,826
Points
2,000
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
19,826 2,000
Salute..
Jana hapa JF kulikua na bonge la battle kati ya Injinia profeshino,TO CCNP Engineer na mtaalamu wa HKL Humble African ambapo ile motion yetu pendwa hapa nchini na duniani kwa ujumla "Money is better than Education ilikua inajadiliwa ambapo sisi ambao hata kidato cha pili hatukuvuka tulikua tuna like na kusoma tu. Mshindi akatoka upande unaosapoti pesa mkuu HA huku akimtupa mbaali TO na injinia wetu humu JF bwana @CCNP Engeneer.

Basi bwana usiku nikawa namcheki lecturers wangu namba 2 baada ya JF memba nilio wafolo Professor GOOGLE nikawa napita kuangalia Gadgets and Technology kutoka kwa mainjinia mbalimbali duniani ndipo nikakutana na huyu injinia aliniacha kinywa wazi kwa uwezo wake mkuuubwa wa ubunifu. Ametumia elimu yake kujiajili na kufanya vitu vya tofauti kabisa kwenye jamii (Kamshinda huyu TO wetu)

Anaitwa James Hobson a.k.a Hacksmith ni Injinia,mbunifu na mtengenezaji wa video za YouTube. Hua anachukua idea za uongo kutoka kwenye Video games, movies na Comics mbalinbali. Huyu jamaa hua anatengeneza yale tunayoyaona kwenye movie za avangers,X man, Star war, na games mbalimbali na kutengeneza mfano wake (replica).
Katengeneza vitu hivi
  • Suti ya Iron man
  • Ngao ya Captain America ambayo ina electromagenetic anaweza kuivuta popote,pia suti yake
  • Makucha ya X man ambayo yanazama ndani na kurudi nje
  • Psylocke's psionic Sword (X man Apocalypse)
  • Lightsaber ya kwenye Star wars.
Nyundo ya Thor god of Thunder.
Huyu jamaa kavunja rekodi kabisa baada ya kutengeneza replica ya nyundo ya Thor ambayo anaweza kuinyenyua yeye pekee yake. Kaiwekea Electromagenetic na fingerprints scanner ambayo inamwezesha kunyenyua hiyo nyundo yeye pekee tu.

Huyu jamaa namfananisha na mtaalamu wa uvumbuzi Thomas Edison ambae alimfundisha mke wake wa pili Morse Code ili wawe wanawasiliana kwa ishara ya vidole pindi wazazi wa mke wake wakiwepo.
>>>>Morse code is a method of transmitting text information as a series of on-off tones, lights, or clicks that can be directly understood by a skilled listener or observer without special equipment. It is named for Samuel F. B. Morse, an inventor of the telegraph.Au nimfananishe na bwana Kim ung-yong ambae aliweza kuongea lugha 4 alipokua na miaka 2, aliweza kufanya hesabu za aljebra akiwa na miaka 3, alialikwa wanafunzi wa fizikia chuoni alipokua na miaka 4, alialikwa Marekani kwenye kitengo cha NASA akiwa na miaka 7, alipata PHD yake akiwa na miaka 15, alikua na IQ ya 210.
ikumbukwe mimi nilipokua nina miaka 15 nilikua najifunza jinsi ys kujibu kitabu cha Mabala the Farmer.


Mnaweza kumuangalia Youtube na Facebook huyu Hacksmith muone kazi zake.
Ma-Injinia wa Tanzania upande wa Teknolojia mna lipi la kujifunza toka kwa huyu mbunifu..?
https://www.facebook.com/thehacksmith/
Tchao

Da'Vinci.
 
miminimkulimaakachekasana

miminimkulimaakachekasana

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2017
Messages
1,658
Points
2,000
miminimkulimaakachekasana

miminimkulimaakachekasana

JF-Expert Member
Joined May 29, 2017
1,658 2,000
Antman and the wasps,venom,deadpool, black panther 2 nazisubiria kwa hamu
#marvel_studios
MKUU DC VP HUWAKUBALI?
MI NAISUBIRIA SHAZAM PIA
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
19,826
Points
2,000
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
19,826 2,000
Wick tuwekee vipicha picha mkuu
 

Forum statistics

Threads 1,293,776
Members 497,735
Posts 31,153,158
Top