Kutana na fundi mahiri wa ujenzi wa nyumba

Ewaaa,
Sahihi kabisa.

Nilimuita nikampa kazi. Nilimuona siku ya kwanza na ya mwisho wakati wa kuchukua hela tu.

Kwa kipindi chote Cha ujenzi zimekuja batch kama nne hivi tofauti. Yaani wanakuja Hawa Leo, kesho au keshokutwa hawarudi wanakuja wengine, amenipa hasara ya kubomoa nyumba na kuijenga upya. Maana nyumba ilikua dhaifu sana.
Hata mimi alinisababishia hasara huyu jamaa. Ukuta ulipinda.
 
Huyu Mzee hashindi saiti. Mkishapatana tu humuoni bali vibarua wake wa kuokoteza okoteza. Utakuja kumuona siku mafundi wameshalipua wanataka Chao
Ukimpa hela ya vifaa ndio utajuta zaidi na hata ukiacha vifaa huwa vinaishia kuuzwa usipokuwepo.
 
IMG_20230208_182339.jpg
IMG_20230208_182339.jpg
 
Changia kwa hekima kosoa kwa hekima

Jamii forums imetoa uhuru wa kutumia utambulisho bandia kwa akili ya kulinda maslahi binafsi ya mwanachama.. Lakini kupewa huo uhuru haina maana uwatweze wengine kwa vile tu hujulikani utambulisho wako halisi

Ndani ya huu mtandao kuna mwanachama wa aina mbili au tatu
1. Wanaotumia utambulisho halisi
2. Wanaotumia utambulisho bandia
3. Wanaotumia utambulisho halisi na bandia
Watu wanakutana hapa hawafahamiani lakini kutokana na mahitaji ya kimaisha na maslahi ya kila mmoja ama ya upande mmoja watu hufikia hatua ya kufahamiana zaidi nje ya huu mtandao

Kuna wajinga wachache wenye uono kimo cha mbilikimo wanaodhani kwa kutumia utambulisho bandia basi wanaweza kufanya lolote na wasijulikane popote bila kujua ya kwamba maandishi hayafitiki.. Ni kupitia maandishi yako ya jana ama hitaji lako la mbeleni unaweza kujifunua na kubaki uchi kabisa

Heshima sana maandiko ya wengine hasa wale ambao inaishia kuwaona jukwaani lakini hamjawahi hata kuonana.. Hata kama maandiko yake hukubaliani nayo kosoa kwa adabu kosoa kwa heshima..Kosoa kwa hoja jadilifu na si vioja, kashfa, dharau au kejeli!

Heshima muda wake aliotumia kuandika hiyo mada, kifurushi chake, ujumbe na maudhui yake..! Si lazima ukubaliane naye.. Hivyo mpinge kwa hoja zenye mantiki ama mpotezee.. Sometimes kuna kipengele cha kukubaliana kutokubaliana na kinyume chake!

Ukiona mada imeruhusiwa kuwa hewani na kupata wachangiaji... Iheshimu sana kwa maana ina kibali cha kanuni na sheria za jukwaa! Kwa maana ya kwamba imekidhi vigezo vyote vya kuruhusiwa kuwepo hai.. Watu wanaweka mada na hazichukui round zinaliwa kichwa na kutupwa jalalani..

Mada inayoachwa hewani iheshimu sana kulingana na jukwaa lake husika..kitendo cha kuiita ya kipuuzi ama ya kipumbavu si kwamba umemtusi na kumkejeli mtoa mada tu, bali hata wachangiaji wengine na hata walioiruhusu iwepo .

Usiwe ndezi kiasi Hicho una background that can be traced to the maximum... Maandishi yako mwenyewe ya awali yanaweza kuwaongoza watu mpaka ulipo na wakakufikia bila shida na wakakufanya chochote watakacho hasa kama hawana hofu na Mungu aliye hai

Kikubwa unapotumia utambulisho bandia usidhani ndio umeyawezea maisha.. Kumbuka bado unaishi na shida hazikomi.. Lakini pia kumbuka una background ambayo kwa namna iwayo yote huwezi kuifuta na watu wanayo mkononi..
Unapoamua kumchafua mtu, jichunguze wewe kwanza.
Tazama unapomnyoshe mtu kidole vidole vitatu hukugeukia wewe.

Ni hayo tu.
Cc#mshana jr
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom