Kutamka alfabeti a, b, c, d,...x, y, z kwa kiswahili

Jayfour

Senior Member
Feb 20, 2011
115
0
Nisaidieni wataalam wa lugha yetu kutamka herufi hizo kwa kiswahili...nakumbuka shuleni tulifundishwa ila sasa nimeshasahau kwasababu sijasikia wengine wakitumia. Ninazozikumbuka tulizofundishwa ni: a, be, che, de.
Natamani nijue matamshi ya herufi zote ili niwe natumia kutamka vifupisho kama BBC, TBC, . ITV, AU, CCP, tlp, cndd, cnn, n.k kwa kujiamini.
 

Vinci

JF-Expert Member
Jul 6, 2009
2,644
2,000
aa, be,che, de, ee,fe,he...mkuu vipi..hukupitia chekechekea nini!!!
 

Jayfour

Senior Member
Feb 20, 2011
115
0
aa, be,che, de, ee,fe,he...mkuu vipi..hukupitia chekechekea nini!!!
teh teh teh ungemalizia mpaka z bana, au na wewe umesahau? Mimi nilijifunza hizo chekechea wakati ule tunaita ''shule ya vidudu'' lakini nimesahau. kama unakumbuka na j, k, l, m, n, o, p, r, s, t, v, w, n.k basi nikumbushe ili niwe nazitumia katika lugha yetu ya kiswahili. Kwasababu kuna maneno ya kiswahili lakini yakifupishwa tunalazimika kutamka kwa lugha ya kigeni wakati tuna lugha yetu inayojitosheleza.
Maneno kama ''chama cha waalimu'' cwt, ''jeshi la wananchi tanzania'' jwtz, ''shirika la umma'' su, ''chama cha mapinduzi'' ccm, nk si tungeweza kutumia lugha yetu tu bila kulazimika kutumia kiingereza!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom