El Roi
JF-Expert Member
- May 29, 2020
- 262
- 497
Baadhi yetu tumetoa michango hapa juu ya umuhimu wa kurekebisha mifumo inayoendesha nchi hii mf katiba, Sheria na mifumo ya utawala ili kujenga taifa la kisasa,linalokwenda na wakati na taifa inclusive kwa maana ya kuwashirikisha wananchi wake kujitawaka vema.
Kwa mfano Ni Jambo lisilo na mashiko sahihi kumuona. Mfano mgombea nafasi ya urais aliyeshika nafasi ya pili baada ya yule aliyeshinda urais, kukaa tu hivihivi bila kushika nafasi yoyote inayotambuliwa na katiba au Sheria za nchi.
Katika uchaguzi uliopita, mgombea wa upinzani Edward lowassa alipata asilimia 40 dhidi ya 58 za yule aliyeshinda urais. Ajabu baada ya hapo alipotea kabisa ktk nafasi rasmi za uendeshaji nchi kwa pamoja.
Ajabu yeye aliyepata kura milioni sita hakuwa na lolote la kufanya, kazidiwa na mbunge wa Jimbo aliyepata mwingine kura laki moja. Ndo maana baada ya hapo hukumuona lowassa anafanya lolote ambalo lingemfanya kuwa active katika uendeshaji wa nchi kikatiba,au kisheria on his own right.
Ndo maana ninapendekeza, yawepo mabadiliko ambayo yule anayefata kwa wingi wa kura baada ya mshindi wa nafasi ya Rais aingie moja kwa moja bungeni na awe ndo kiongozi wa upinzani rasmi bungeni. Huyo ajulikane Kama official opposition leader. Apewe ofisi yake, staffs na awe ndo kiongozi wa Baraza kivuli la mawaziri. Kwenye seniority ya uongozi wa nchi awepo baada ya waziri mkuu.
Kufanya hivyo kwa maoni yangu nadhani ndo kutasaidia ile dhana ya kumhamishia siasa bungeni kuwezekana.
2) kutaleta utulivu kwa mgombea aliyeshika nafasi ya pili maana anajua kwa hakika kwamba bado ana kazi ya kufanya pamoja na kushindwa urais. Mawazo yake kweli Sasa yatakuwa bungeni maana ataongoza upinzani akiwa Sasa ndani ya bunge na huku nje akitambuliwa Kama moja ya viongozi wakuu katika nchi.
Apewe ulinzi, na mengine. Nawaambia nchi itatulia na wote tutajenga nchi in the so called unity in diversity formula. Narudia haijakaa vizuri kabisa kwa mtu aliyepata mamilioni ya kura, Kama nilivyooneaha hapo mwanzo, kubaki bila kushiriki ktk uongozi wa nchi, na hapa Kuna mtu amepata kura ishirini elfu anakuwa mbunge wa Jimbo, mshahara mzuri, anapigiwa saluti nk eti aliyekuwana mamilioni ya kura nchi nzima anabaki jobless! Tutafakari and let us think bigger!