Kutambuliwa rasmi kwa kiongozi rasmi wa upinzani(official opposition leader) kutafanya nchi itulie na kutoa fursa ya mchango walau sawa

El Roi

Member
May 29, 2020
61
150
Baadhi yetu tumetoa michango hapa juu ya umuhimu wa kurekebisha mifumo inayoendesha nchi hii mf katiba, Sheria na mifumo ya utawala ili kujenga taifa la kisasa,linalokwenda na wakati na taifa inclusive kwa maana ya kuwashirikisha wananchi wake kujitawaka vema.

Kwa mfano Ni Jambo lisilo na mashiko sahihi kumuona. Mfano mgombea nafasi ya urais aliyeshika nafasi ya pili baada ya yule aliyeshinda urais, kukaa tu hivihivi bila kushika nafasi yoyote inayotambuliwa na katiba au Sheria za nchi.

Katika uchaguzi uliopita, mgombea wa upinzani Edward lowassa alipata asilimia 40 dhidi ya 58 za yule aliyeshinda urais. Ajabu baada ya hapo alipotea kabisa ktk nafasi rasmi za uendeshaji nchi kwa pamoja.

Ajabu yeye aliyepata kura milioni sita hakuwa na lolote la kufanya, kazidiwa na mbunge wa Jimbo aliyepata mwingine kura laki moja. Ndo maana baada ya hapo hukumuona lowassa anafanya lolote ambalo lingemfanya kuwa active katika uendeshaji wa nchi kikatiba,au kisheria on his own right.

Ndo maana ninapendekeza, yawepo mabadiliko ambayo yule anayefata kwa wingi wa kura baada ya mshindi wa nafasi ya Rais aingie moja kwa moja bungeni na awe ndo kiongozi wa upinzani rasmi bungeni. Huyo ajulikane Kama official opposition leader. Apewe ofisi yake, staffs na awe ndo kiongozi wa Baraza kivuli la mawaziri. Kwenye seniority ya uongozi wa nchi awepo baada ya waziri mkuu.
Kufanya hivyo kwa maoni yangu nadhani ndo kutasaidia ile dhana ya kumhamishia siasa bungeni kuwezekana.

2) kutaleta utulivu kwa mgombea aliyeshika nafasi ya pili maana anajua kwa hakika kwamba bado ana kazi ya kufanya pamoja na kushindwa urais. Mawazo yake kweli Sasa yatakuwa bungeni maana ataongoza upinzani akiwa Sasa ndani ya bunge na huku nje akitambuliwa Kama moja ya viongozi wakuu katika nchi.

Apewe ulinzi, na mengine. Nawaambia nchi itatulia na wote tutajenga nchi in the so called unity in diversity formula. Narudia haijakaa vizuri kabisa kwa mtu aliyepata mamilioni ya kura, Kama nilivyooneaha hapo mwanzo, kubaki bila kushiriki ktk uongozi wa nchi, na hapa Kuna mtu amepata kura ishirini elfu anakuwa mbunge wa Jimbo, mshahara mzuri, anapigiwa saluti nk eti aliyekuwana mamilioni ya kura nchi nzima anabaki jobless! Tutafakari and let us think bigger!
 

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
11,932
2,000
Mkuu umetoa hoja ya msingi sana hizi siasa zetu za ''winner takes all'' ndio zinaleta vurugu na migogoro nchi nyingi za Afrika, angalau Zanzibar waliunda SUK ikapunguza tension za upinzani na serikali.

Kenya pia kupitia BBI wameona hilo, kuweka mfumo ambapo upinzani hauachwi nje ya uongozi wa Taifa.

Ingependeza hata wizara mbili tatu wapewe hata upinzani waongoze. Kutaleta umoja na mshikamano na kuepusha siasa za chuki za "Ama zangu Ama zako" maana mwisho wa siku wote mnakua na share kwenye keki ya taifa.
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,191
2,000
Katiba ya nchi ya Zanzibar imekaa vizuri kidogo tofauti na huku kwetu tuna katiba ya hovyo sana
Una tegemea spika Ndugai asimamie bunge halafu liwe nawazo jema kama hilo hapo juu. Yeye husubiri maagizo afanye kama ana chunga mbuzi..
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
20,140
2,000
El Roi,

..waTz tulifanya makosa kuchangua utitiri wa wabunge wa ccm.

..tunatakiwa tuwe na ratio ya wabunge inayolazimisha vyama kusikilizana, kuheshimiana, na kupitisha sheria kwa pamoja.

..mapendekezo yako nayaunga mkono, ila ningependa kuongezea hoja ya kuwa na mgawanyo mzuri ktk nafasi za ubunge.
 

El Roi

Member
May 29, 2020
61
150
Tatzo linakuja wanapounga juhudi
Waunga juhudi wanaweza kuwepo ndiyo maana wengine Wana jadi ya usaliti tu hata uwape Nini. Lakini ukweli mkubwa ni kwamba wengine nao wanafikia kuunga juhudi maana wanaachwa nje kabisa wanakosa la kufanya . Mbaya ikiwa na mtu anahisi ana contribution ya kisiasa na mchango ktk kusaidia nchi. Hivi unadhani Kama mfumo ungekuwa unamtambua Lowassa angeondoka opposition? Ni ngumu Sana. Alijikuta hana la kufanya hasa kulingana na CV yake. Na kumbuka upande alikuwa anapata suluba za hapa na pale. Lakini ungekuwa vice versa, angetulia.
 

komamgo

JF-Expert Member
Sep 14, 2012
1,930
2,000
Haiwezekani hata kidogo kumuweka Tundu mjengoni. Hana hadhi hata ya udiwani
 

El Roi

Member
May 29, 2020
61
150
Haiwezekani hata kidogo kumuweka Tundu mjengoni. Hana hadhi hata ya udiwani
Kama umesoma vizuri andiko langu utaona naongea ktk picha kubwa ( big picture) na sija cite mtu hasa. Naomba huo ndo uwe mwekekeo. Tujadili issues na siyo watu. Na Kama unavyojua watu wenye akili kubwa hujadili masuala. Hata hivyo tabia ya profile watu haifai. Maana hata wale unaowaona wewe ni malaika, hao pia ukiwafanyia upasuaji( postmortem) wanaweza kuwa si vile unavyowaona. Tupendane tafadhali na tuheshimiane hata Kama tuwa mitazamo tofauti. Otherwise Asante.
 

kelao

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
7,358
2,000
Hili ni wazo la msingi sana, tena la mwaka!hebu fikiria mtu aliepata kura ml. 6 awe hana kazi ya kiserikali Kama yule alieongoza kwa kupata kura ml. 8. Yaani tofauti ya ml 2
 

komamgo

JF-Expert Member
Sep 14, 2012
1,930
2,000
Kama umesoma vizuri andiko langu utaona naongea ktk picha kubwa ( big picture) na sija cite mtu hasa. Naomba huo ndo uwe mwekekeo. Tujadili issues na siyo watu. Na Kama unavyojua watu wenye akili kubwa hujadili masuala. Hata hivyo tabia ya profile watu haifai. Maana hata wale unaowaona wewe ni malaika, hao pia ukiwafanyia upasuaji( postmortem) wanaweza kuwa si vile unavyowaona. Tupendane tafadhali na tuheshimiane hata Kama tuwa mitazamo tofauti. Otherwise Asante.
Positively captioned
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom