Kutakuwa na tatizo katika usahihishaji wa mtihani wa somo la Elimu ya Dini ya Kiislam Kidato cha Nne

Baraza la mitihani waangalie.
Imekuwaje hakuna wastani mzuri katika somo la Elimu ya Dini ya Kiislam kwenye matokeo ya kidato cha nne?
Kuna walakini katika usahihishaji.
Serikali ifanye uchunguzi.
Ili ukweli ubainike. Kama ni watoto wote waliofanya somo hilo hawana uwezo wa kupata A tujue. Ripoti itolewe na iwe wazi kwa kila mtu kuisoma. Ili wazazi waondoa malalamiko yao baada ya kujua kwamba watoto wao hawana uwezo wa kufaulu grade A ya somo hilo.
Asante
Unapoamini kuwa kuelewa juzuu zile ni lazima bakora za migongoni zitembee hayo ndo matokeo yake.

Kukariri bila kudadavua
 
MAJLISI YA MARHUM SHEIKH ABDALLAH SEIF

Sheikh Abdallah Seif aliyekuwa Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania. Mpenda usomi wa dini ya Islam na ilm duniya na kusisitiza viongozi na waumini kujifunza kwa bidii ili kujiongezea ufahamu na wawe wazi kupokea maswali kutoka kwa waumini pia kujenga mazingira ya uwazi wa kuweza kuhoji na sio kuwa wapokeaji tu ya yale wanaoambiwa bila kujihakishia ukweli na usahihi wa darsa.

Sheikh Abdallah Seifu, upande wa elimu duniya kupitia Bilal Muslim Mission Tanzania amechochea kuwatia hamasa waumini kujiunga na shule za mitaala ya sekula na dini English - Shia Maktab ili kujijengea uwezo capacity building (Maendeleo ya Watu) kupitia taasisi aliyoiongoza Swahili - Shia Maktab

Bilal Muslim Mission
 
Tatizo lipo kwa walimu wa somo,itakua wanawafundisha vitu vyepesi hivyo mnajifaulia tu mitihani ya ndani ila ikija Necta mnachemka

Kuhusu usahihishaji kule hakuna uhuni kama mnavyotaka kuaminisha watu,wasahihishaji ni hao hao wanaofundisha na wanasahihisha kwa utaratibu wa viwango vya juu kabisa
Umewahi kusoma somo la Islamic mkuu ? Unajua kwann walianza kutumia namba za mitihani mbadala wa majina enzi hizo?

Kwanza naishia hapa Kwa mchango wangu siongezi neno maana huwa sichangii mada za aina hii.
 
Umemaliza ndugu yangu,kusoma Islamic juu juu huku lengo ni kyfanya mtihani wake utaishia kulaumu tu
Tatizo nimeambiwa liko kwa walimu wao huwa wakienda wanaenda kuhubiri badala ya kufundisha dini

Wanaenda zaidi kuhubiria watoto na wengine kuwafanya kuwa siasa Kali lakini si kuwafunza Islamic knowledge kipindi kizima wanapiga mahubiri tu kuna mtoto wa kufaulu somo hapo? Haiwezekani
 
Jiheshimu
 
Anaitwa nani huyo mungu wao
Ndio nmeuliza swali hapo kwamba au hao wenzetu wazungu wana mungu wao tofauti na huyu tunaemjua sisi wengine? Maana tunavyojua katika watu ambao hawana time na mambo ya dini wala mungu ni hao wazungu.
 
Nilisoma Madrasa, Quran naifahamu vizuri, Fiqih naifahamu vizuri, Hadith nazifahamu nyingi ( Nipo vizuri mwenye elimu ya dini)

Shule ya msingi na secondary nilikuwa muhudhuriaji mzuri wa vipindi vya dini kwa 95%

Mitihani ya test na ile ya kumaliza muhula kupata "A" ilikuwa ni kawaida sana.

Mtihani wa dini wa Taifa mwaka 2012, hakuna swali ambalo sikulifahamu, nilijibu maswali yote tena kwa kujiamini.

Matokeo yalipotangazwa....Nilikutana na "F" ya Islamic knowledge.

Aisee hadi leo huwa na jiuliza au wasahihishaji walikuwa BUDDHISTS .

Sikuhitaji kukata rufaa kwa sababu zangu binafsi.
Huwa ni hujuma tu ,siunakumbuka kipind kile 2012 ponda alipokiwasha baada ya kubainika hujma ya yule mwanafunz alopata A Islamic akawekewa F wakasema walikosea ,mpk ndalichako akatolewa so ni kawaida
 
Nilisoma Madrasa, Quran naifahamu vizuri, Fiqih naifahamu vizuri, Hadith nazifahamu nyingi ( Nipo vizuri mwenye elimu ya dini)

Shule ya msingi na secondary nilikuwa muhudhuriaji mzuri wa vipindi vya dini kwa 95%

Mitihani ya test na ile ya kumaliza muhula kupata "A" ilikuwa ni kawaida sana.

Mtihani wa dini wa Taifa mwaka 2012, hakuna swali ambalo sikulifahamu, nilijibu maswali yote tena kwa kujiamini.

Matokeo yalipotangazwa....Nilikutana na "F" ya Islamic knowledge.

Aisee hadi leo huwa na jiuliza au wasahihishaji walikuwa BUDDHISTS .

Sikuhitaji kukata rufaa kwa sababu zangu binafsi.
Wewe kubali tu kuwa hukujibu vizuri.Mtihani wa Dini ukikosea kidogo inatakiwa ukoseshwe kwasababu uongo hautakiwi.
 
Ungekuwa unajua namna mitihani inavyotungwa na kusahihishwa usingeleta hii mada yako hapa.
Nikwambie tu kama mtihani una maswali 10, basi utapitiwa na watu wasiopungua 14.
Walimu 10 wanaofundisha hilo somo watasahihisha kila mtu swali lake kwa Chain. Karàtasi ikitoka hapo inapita kwa Checker anakagua kama maswali yote yamepitiwa na alama alizopewa in sahihi. Karatasi inapita kwa mtu wa kutotal alama. Baada ya hapo inaenda computer kujazwa. Baada ya kutoka computer kuna watu tena wanahakiki kama alama za computer ni sawa na zilizo kwenye karatasi. Mchakato n mrefu mno kuonewa sio rahisi kama unavyodhani
Jamaa akubali tu kuwa hakufanya vizuri
 
Nilisoma Madrasa, Quran naifahamu vizuri, Fiqih naifahamu vizuri, Hadith nazifahamu nyingi ( Nipo vizuri mwenye elimu ya dini)

Shule ya msingi na secondary nilikuwa muhudhuriaji mzuri wa vipindi vya dini kwa 95%

Mitihani ya test na ile ya kumaliza muhula kupata "A" ilikuwa ni kawaida sana.

Mtihani wa dini wa Taifa mwaka 2012, hakuna swali ambalo sikulifahamu, nilijibu maswali yote tena kwa kujiamini.

Matokeo yalipotangazwa....Nilikutana na "F" ya Islamic knowledge.

Aisee hadi leo huwa na jiuliza au wasahihishaji walikuwa BUDDHISTS .

Sikuhitaji kukata rufaa kwa sababu zangu binafsi.
Mkuu wanaangalia pia na matendo yako kama yanaendana na hiyo Islamic knowledge...
 
Somo la Islamic Knowledge la 'O' Level, halihataji uwe unajua Kiarabu ili uweze kulifahamu.

Kutegemea Tasfiri huweza kukufanya tegemezi, kufahamu lugha ya ziada husaidia.

Huwezi jua wanaosahihisha mitihani ni wenzetu ma Shia kwa uwazi au bila kufahamika wenye kusisitiza kuonesha ufahamu na umahiri, hivyo kutaka wanafunzi wafanye bidii zaidi kujisomea wasibwete kwani wakipewa alama A au B halafu wanafunzi hao wakienda kimataifa mfano kulinganishwa na wenziwao wa nchi za kiislamu wanaweza kuaibika.

Nia ni kuwa ukipata daraja C nawe ulikuwa unatamani sana kuwa mwanazuoni basi pasina shaka utafanya bidii ya ziada kujisomea ili ufikie lengo lako kama utataka baadaye kuwa imamu, sheikh au mhadhiri ktk chuo cha dini.
 
Mkuu elimu ya dini inayosomeshwa mashuleni ni nyepesi sana ukilinganisha na inayosomeshwa kwenye madrasa za kiislamu, na ndio mana malalamiko yanakua mengi sana kuwa sababu mitihani inakua mepesi lakini grade zinakua zipo chini sana.

Wanafunzi wengi wanaokwenda kimataifa kwa masomo ya dini ni wale waliofanya vizuri kwenye madrsa na sio mashuleni. vyeti vya shule hutumika kama kiingilio tu.
 
Hilo somo liitwe Arabic tribe and taboo kwani maada za humo haziendani na Islam kwani wao wanafundisha kufa kwa ajili ya uisilamu na sio kuishi kwa ajili ya uisilamu. Watoto wangu watasoma Qur'an tu na sio miduni na majini
 
Mkuu elimu ya dini inayosomeshwa mashuleni ni nyepesi sana ukilinganisha na inayosomeshwa kwenye madrasa za kiislamu

Ndo maana wasahishaji hawataki lawama, mfano uliotoa ni sahihi kabisa elimu dini inayopatikana madrasa ni kubwa mno kuliko elimu dini anayopata mwanafunzi wa sekondari kwa miaka 4 halafu kuwa mtahiniwa wa somo la dini O Level.
 
Kuna marks na grading
Unaweza pata marks 90 ila ukawekewa grade D
Yes wanaita kutunuku daraja. Na hiyo kazi hufanywa na watu wachache sana baada ya michakato yote ya usahihishaji kukamilika. Na huko ndiko kwenye shida!
 
Back
Top Bottom