Kutakuwa na tatizo katika usahihishaji wa mtihani wa somo la Elimu ya Dini ya Kiislam Kidato cha Nne

Kuna waziri mmoja wa miaka ya nyuma alikomalia suala la matumizi ya namba badala ya majina ktk mitihani. Ilipokubalika idadi ya waislamu wanaofaulu ikaanza kuongezeka. Inawezekana na kwenye Islamic knowledge kukawa na shida fulani.
Saiv wanatumia nn??
 
Baraza la mitihani waangalie.
Imekuwaje hakuna wastani mzuri katika somo la Elimu ya Dini ya Kiislam kwenye matokeo ya kidato cha nne?
Kuna walakini katika usahihishaji.
Serikali ifanye uchunguzi.
Ili ukweli ubainike. Kama ni watoto wote waliofanya somo hilo hawana uwezo wa kupata A tujue. Ripoti itolewe na iwe wazi kwa kila mtu kuisoma. Ili wazazi waondoa malalamiko yao baada ya kujua kwamba watoto wao hawana uwezo wa kufaulu grade A ya somo hilo.
Asante
waliosahihisha huo mtihani si ndio wale walimu wao waliowafundisha? Mmeanza kale katabia kenu kakulalamika ovyo siyo?
 
Islamic Knowledge ni ngumu kuliko Rocket Science, ieleweke hivyo

Na wanazuoni waliokamilika katika ilmu ya dini ya Islam wanasisitiza uewe mahiri katika lugha ya Kiarabu ili upate kitu sahihi toka katika Quran Takatifu, hadithi za Mtume na maswahaba wake ukizingatia kufahamu mazingira, utamaduni, desturi, mila na lugha ya kipindi hicho Quran ilipoteremshwa na maandiko mbalimbali ya maswahaba wa mtume waliyeishi naye .

Ndiyo maana unaona maimamu, masheikh hufuata utaratibu wa aya zisomwe kwanza ktk lugha ikiyotumika wakati Kitabu Kitakatifu kilipoteremshwa halafu tafsiri hufuata kwa Kiswahili, Kiingereza, Kireno n.k ili kuepuka maana ya neno au aya nzima kunukuliwa vibaya.

Tatizo sisi waTanzania tunachukulia lugha mzahamzaha iwe hata Kiswahili chenyewe hatukimanyi vizuri iwe kwa kuandika maandishi sahihi, kutamka na hata kufahamu maana kadhaa katika mukstadha wa matumizi yake.

Hapo basi tumefeli kupata mabingwa wengi wa kuuzungumza na kutumia lugha kwa usahihi iwe katika dini, mawakili wabobezi ktk huduma za kisheria katika lugha za Kiswahili, Kiingereza na Kiarabu wakati wa kufundisha, kusomesha, kutoa elimu ya dini au hata kufanya uwakilishi mzuri wa hoja katika mahakama kwa upande wa Mawakili.
 
Nilisoma Madrasa, Quran naifahamu vizuri, Fiqih naifahamu vizuri, Hadith nazifahamu nyingi ( Nipo vizuri mwenye elimu ya dini)

Shule ya msingi na secondary nilikuwa muhudhuriaji mzuri wa vipindi vya dini kwa 95%

Mitihani ya test na ile ya kumaliza muhula kupata "A" ilikuwa ni kawaida sana.

Mtihani wa dini wa Taifa mwaka 2012, hakuna swali ambalo sikulifahamu, nilijibu maswali yote tena kwa kujiamini.

Matokeo yalipotangazwa....Nilikutana na "F" ya Islamic knowledge.

Aisee hadi leo huwa na jiuliza au wasahihishaji walikuwa BUDDHISTS .

Sikuhitaji kukata rufaa kwa sababu zangu binafsi.
Mkuu hizi dini ni project za watu , na wana watu wao wanawaitaji kwa malengo ya baadae so shukuru ulichojifunza ,maana A au F haikupunguzii chochote
 
Nilisoma Madrasa, Quran naifahamu vizuri, Fiqih naifahamu vizuri, Hadith nazifahamu nyingi ( Nipo vizuri mwenye elimu ya dini)

Shule ya msingi na secondary nilikuwa muhudhuriaji mzuri wa vipindi vya dini kwa 95%

Mitihani ya test na ile ya kumaliza muhula kupata "A" ilikuwa ni kawaida sana.

Mtihani wa dini wa Taifa mwaka 2012, hakuna swali ambalo sikulifahamu, nilijibu maswali yote tena kwa kujiamini.

Matokeo yalipotangazwa....Nilikutana na "F" ya Islamic knowledge.

Aisee hadi leo huwa na jiuliza au wasahihishaji walikuwa BUDDHISTS .

Sikuhitaji kukata rufaa kwa sababu zangu binafsi.
Itakuwa wanasahihisha manaswara ambao wao wenyewe hawajui maswali wala majibu!
 
Na wanazuoni waliokamilika katika ilmu ya dini ya Islam wanasisitiza uewe mahiri katika lugha ya Kiarabu ili upate kitu sahihi toka katika Quran Takatifu, hadithi za Mtume na maswahaba wake ukizingatia kufahamu mazingira, utamaduni, desturi, mila na lugha ya kipindi hicho Quran ilipoteremshwa na maandiko mbalimbali ya maswahaba wa mtume waliyeishi naye .

Ndiyo maana unaona maimamu, masheikh hufuata utaratibu wa aya zisomwe kwanza ktk lugha ikiyotumika wakati Kitabu Kitakatifu kilipoteremshwa halafu tafsiri hufuata kwa Kiswahili, Kiingereza, Kireno n.k ili kuepuka maana ya neno au aya nzima kunukuliwa vibaya.

Tatizo sisi waTanzania tunachukulia lugha mzahamzaha iwe hata Kiswahili chenyewe hatukimanyi vizuri iwe kwa kuandika maandishi sahihi, kutamka na hata kufahamu maana kadhaa katika mukstadha wa matumizi yake.

Hapo basi tumefeli kupata mabingwa wengi wa kuuzungumza na kutumia lugha kwa usahihi iwe katika dini, mawakili wabobezi ktk huduma za kisheria katika lugha za Kiswahili, Kiingereza na Kiarabu wakati wa kufundisha, kusomesha, kutoa elimu ya dini au hata kufanya uwakilishi mzuri wa hoja katika mahakama kwa upande wa Mawakili.

Somo la Islamic Knowledge la 'O' Level, halihataji uwe unajua Kiarabu ili uweze kulifahamu.
 
Hii kitu ipo Sana .......matokeo ya somo hili huwa ndo Ivo ...ukijitahid ukapata C we n mtabe sijui ni mini kinafanyika ....japo watu wanakaa kimya but naamini kuna kitu hakipo sawa.

Tatizo lipo kwa walimu wa somo,itakua wanawafundisha vitu vyepesi hivyo mnajifaulia tu mitihani ya ndani ila ikija Necta mnachemka

Kuhusu usahihishaji kule hakuna uhuni kama mnavyotaka kuaminisha watu,wasahihishaji ni hao hao wanaofundisha na wanasahihisha kwa utaratibu wa viwango vya juu kabisa
 
Duh , akil za waislam bn , wao wanahisigi serikali nzima ni wakristu au waislam ambao wapo kweny system hawaupend uislam , too funny

Saizi wamejaa serikalini kuanzia Rais hadi mawaziri ila bado wanalalamika kuonewa
 
Back
Top Bottom