Kutakuwa na faida gani kurudisha JKT?

PastorPetro

Senior Member
Feb 25, 2008
189
35
Mimi nilipitia JKT Opresheni Nguvu Kazi. Nilikuwa Mlale JKT. Kwa kweli najiuliza kwenye JKT ilinisaidia nini zaidi ya kupoteza mwaka wa maisha yangu. Tulikuwa tunalipa wananchi kwa kutusomesha A level eti? Nilishuhudia mabiniti wakinayayaswa kwa kuwa mboga ya maafande. Nimeona vijana waliojifanya eti wasomi wakisurubiwa hadi kujinyea. Wanasema Jeshi la Kujenga taifa, tulijenga nini?

Kuna mwanablogu Da Chemi ametoa mada kali kuhusu yaliyompata akiwa JKT. Swahili Time: Marudio - Miaka Baada ya tukio kaniomba Msamaha! Nasikia JKT inarudishwa mwakani. Vijana wamekuwa wengi mno sasa hayo makambi yatakuwa wapi? Hela ya kuwalisha itatoka wapi? Idadii ya vijana ni karibu mara 10 ya enzi zetu. Siwezi kuruhusu vijana wangu hasa binti zangu waende jeshini. Hapana.:yell:
 
Hakuna faida
kuna hasara nyingi mno

1.kupoteza pesa
2.wanawake kubakwa
3.kuaandaa majambazi wa kesho
since kutakuwa na mafunzo ya ujasiri na kutumia silaha
4.kuendeleza taifa la watu waoga watiifu
5.....mengine mnaweza ongezea
 
Mimi nilipitia JKT Opresheni Nguvu Kazi. Nilikuwa Mlale JKT. Kwa kweli najiuliza kwenye JKT ilinisaidia nini zaidi ya kupoteza mwaka wa maisha yangu. Tulikuwa tunalipa wananchi kwa kutusomesha A level eti? Nilishuhudia mabiniti wakinayayaswa kwa kuwa mboga ya maafande. Nimeona vijana waliojifanya eti wasomi wakisurubiwa hadi kujinyea. Wanasema Jeshi la Kujenga taifa, tulijenga nini?

Kuna mwanablogu Da Chemi ametoa mada kali kuhusu yaliyompata akiwa JKT. Swahili Time: Marudio - Miaka Baada ya tukio kaniomba Msamaha! Nasikia JKT inarudishwa mwakani. Vijana wamekuwa wengi mno sasa hayo makambi yatakuwa wapi? Hela ya kuwalisha itatoka wapi? Idadii ya vijana ni karibu mara 10 ya enzi zetu. Siwezi kuruhusu vijana wangu hasa binti zangu waende jeshini. Hapana.:yell:

Mm nilikuwa mmoja wapo wanaotaka JKT hirudishwe, sasa kutokana naniliyosoma hapo kwa Da Chemi nimekata shauri kwamba bora mbaya kama vp JKT hiwe ya vijana wa kiume au tuweke sheria kali hasa kwa askari hao watakaojaribu fanya vitendo hivyo lkn sema hata hawa dada zetu wengine mboga kumi watataka vyamtelemko na hawatakuwa tayari kuchapa kazi bali kugawa uroda. Mm naona nchi kwanza ishugulikie maisha ya wananchi halafu badae ndohilete huu mpango wao. Inatia hasira sana hukisoma hapo kwa Da Chemi khaa balaa.
 
[h=2]Tuesday, August 02, 2011[/h][h=3]Marudio - Miaka Baada ya tukio kaniomba Msamaha![/h]

(Pichani Ukaguzi wa Gwaride Mlale JKT Songea - Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)


Naona, kuna 'Anonymous' fulani kagusia hii swala ya yalionipata nikiwa jeshini JKT. Watu wengi wamenitumia e-mail kuulizia details. Nimeamua kuibandika tena. Ni posti ya kutoka April 2006. Lakini mjue enzi za JKT, wasichana wengi walinyanyaswa kijinsia, mimi nilikuwa na bahati maana nafahamu wasichana waliokuwa gang raped. Dada fulani, alimkubali afande, alivyomaliza kaita wenzake kwa kusema, "Njooni, Mboga hii hapa!" Yule dada hakuweza kutembea vizuri kama wmezi baada ya hapo!

*****************************************************************************

Nilipokuwa Jeshi ya Kujenga Taifa (JKT) karibu nibakwe na afande Fulani (jina nahifadhi). Lazima niseme kuwa katika kipindi hicho wanaume wengi waliona makambi ya JKT kama ‘buffet' ya wasichana. Si maafande wa jeshi tu, bali hata viongozi wa serikali walikuwa wanapitia makambi ya JKT kula tani yao!

Mimi nilikuwa Masange JKT, Tabora. Wakati huo huyo jamaa alikuwa ni Kepiteni wa JKT. Nadhani alidhania kwa vile yeye ni kepiteni basi alikuwa na haki ya kutembea na yeyote aliyemtaka. Kwangu aligonga ukuta! Bila shaka alikuwa hajawahi ‘kunyimwa' mpaka siku hiyo alipokutana na mimi.

Miaka baada ya tukio nikiwa nafanya kazi Daily News mara nyingi nilikuwa napishana naye Posta Mpya. Basi ananisemesha, na mimi namnunia halafu napita zangu kimya bila kumjibu kwa hasira. Siku moja kanisimamisha kaniambia, "Chemi, naomba msamaha, nisemahe tafadhali, kweli nilikukosea!" Aliongeza kuwa miaka mingi imepita hivyo sina sababu ya kuwa na hasira naye! Na mimi nilimjibu, "Mshenzi sana wewe!" nikaenda zangu.

Ikapita kama mwaka mwiingine. Jamaa anaendelea kunisalimia kila nikimpita njiani na mimi kwa uchungu bado nikashindwa kusema kitu. Basi nikafikiria alichoniambia Posta Mpya. Lakini niliona kama jambo hilo linamsumbua. Na nikasema kama Bwana Yesu aliweza kusamehe watu kwa madhambi yao kwa nini mimi nisimsamehe. Basi baada ya hapo ikiwa nikimwona na akinisalimia naitika na naendelea zangu na nikaona kidogo hata yeye alikuwa na raha.

Lakini bado najiuliza kama kitendo chake kilimsumbua miaka na miaka kama ilivyonisumbua mimi.Unauliza ilikuaje mpaka nikajikuta kwenye situation ya kubakwa. Au mnasema nilitaka mwenyewe. Ngoja niwaelezee ilivyokuwa.

Nilikuwa mhudumu Officer's Mess, mpishi na msafishaji. Huyo jamaa alikuwa ni mgeni kutoka Makao Makuu ya JKT Dar es Salaam. Kwa kweli sikutaka kufanya kazi pale Mess lakini tulichaguliwa special na Matron, mimi kwa vile niijua kupika vyakula mbalimbali hasa za kizungu. Lakini uzuri wa hiyo kazi ni kuwa uanambulia mabaki ya vyakula (leftovers), na mara nyingine kulikuwa hakuna.

Basi huyo Afande alikaa kambini wiki kadhaa. Katika kumhudumia tukawa tunaongea na mimi nikawa namheshimu kama kaka vile. Wala sikusikia mapenzi yoyote kwake. Basi jioni fulani, kanialika chumbani kwake kunywa soda na biskuti na kwa Maongezi zaidi. Sasa kama ulienda jeshi unajua njaa kali unayokuwa nayo. Nikaenda, kanikaribisha vizuri, nilipewa soda na tukawa tunaongea. Basi nikaona mwenzangu anabadilika ghafla! Mara ananikumbatia kwa nguvu, na kunibusu na mengine. Nikajaribu kuaga lakini jamaa hakuniachia. Baada ya ku-plead naye aniachie, kaniachia. Kaomba msamaha na kaniomba niendelee kukaa nimalize hizo soda alizoninulia.

Kama mjinga nikamwamini, nikakaa nakunywa hizo soda. Tukaendelea na Maongezi, kukaa kidogo huyo kanirukia, najaribu kusimama huyo, kanivuta na kuniangusha kitandani! Mimi saa hizo nikawa naogopa kabisa nia yake!Kaniambia eti, "ukipiga makelele najua nitasema nini! Nyamaza! Huna sababu ya kunikatalia!" LOH! Kanizaba kibao! Nikamwuliza kwa nini anaifanyia hivyo, na mimi nilikuwa namwona kama kaka yangu!Hapo sasa ikaniingia. Nabakwa! Loh!

Nilimpiga mangumi na mateke lakini jamaa alikuwa na nguvu huyo kachana chupi yangu! Baada ya hapo, jamaa kashika miguu yangu huko anafoka kwa sauti kama vile anatoa amri "panua miguu! PANUA MIGUU!" Huko katoa ume wake uliyosimama kwenye suruali! Basi kuona sipanui jamaa kaongeza makofi na kafanikiwa kupanua miguu yangu! Kuona kafanikiwa kupanua huyo kajaribu kupenya. Ilipogusa kwangu nilipiga kelele cha kufa! Nikasema, "Nakuufaaaa!"

Heh! Ghafla jamaa kaniachia kaniambia niende. Alisema, "Nimeigusa na ume wangu, unatosha!" Nenda zako! Na ukimwambia mtu najua nitasema nini!"Loh nilikimbia bwenini na giza lile la Masange huko nalia. Wenzangu wananiuliza vipi, nikashindwa niseme nini! Kwanza niliona haya! Fikiria, niliona haya (shame)!Kesho yake nikaenda dispensary na kujiandikisha mgonjwa. Sikwenda kazini Officer's Mess bali nililala bwenini.

Siku iliyofuatia huyo Afande mshenzi kapita bwenini kwetu kaulizia hali yangu, na mimi huko natetemeka kwa woga nikashindwa niseme nini. Alininunulia Orange squash na biskuti na kuzileta bwenini. Sitasahau alivyonitazama! Ilikuwa kama vile anapanga jinsi gani atanipata. Baada ya hapo alimwopoa msichana mwingine na huyo alimkubali kabisa. Akawa analala kabisa huko Officer's Mess. Hakuna anayemsumbua wakijua ni bibi wa Afisa. Basi, siku za yule jamaa kukaa kambini zikaisha, na yule binti alienda naye Tabora mjini kwa siku kadhaa. Halafu jamaa karudi zake DSM. Yule binti karudi zake kambini! Kumbe alienda bila pass. Alidhania kwa vile yuko na mkubwa hana haja ya pass. Na yule Afande ndo kaondoka kimoja! Maafande waliobakia wacha wamtese huyo binti alivyorudi kambini! Walimtesa kwa Extra drill na mengine mpaka ikabidi Military Police waombe wakuu wamsamehe la sivyo atakufa. Raha yake iliishia kwa suluba! Sijui yule binti alidhania jamaa atamwoa! Kwa nini alimkubali yule mshenzi.

Anyway, kila mtu na vyake. Alivyotoka kwenye suluba tulimwuguza! Siku haizkupita na mimi nilitolewa kazi Officer's Mess na kupelekwa kwenye kikosi cha Ujenzi na lazima nisema hapo nilifurahi sana. Basi miaka ilipita. Mimi nilikuwa mwandishi wa habari Daily News, tena nilijenga jina. Sasa nikawa napishana na yule jamaa huko kapandishwa cheo na yuko JWTZ. Jamaa anajaribu kunisalimia na mimi napita zangu kimya, namnunia kabisa.

Nilimwona mshenzi, mnyama, na kila kitu kibaya ndo ilikuwa yeye! Angefanikiwa kuingiza na kunimwagia uchafu wake ningejiona mchafu mpaka leo! Miaka kama 20 imepita sasa na bado nina uchungu naye.Jamani nyie wanaume nawaambia kubaka kinaathari zake kwa wanawake. Unataka raha ya dakika na unamwachia mwenzio na uchungu wa maisha! Wengine mpaka wanakuwa wagonjwa wa akili.

Kwa nini nimeamua kuzungumzia kubakwa kwangu hapa, ni kwa sababu naona wasichana wengi wanabakwa, halafu wanaamua kunyamaza kimya. Kisa wakienda polisi na hospitali wanahofia kuambiwa ni Malaya au walitaka wenyewe! Hata mwamanke mwenzako anaweza kukufokea kuwa ulitaka mwenyewe. Tanzania, wanaume walikuwa na usemi wao kuhusu wanawake na ngono. Walisema eti ukimwomba mwanamke halafu akijibu ndiyo, manake ndiyo atafanya. Akisema labda, manake atafanya, akisema hapana, manake hapana. Lakini jamani tendo si inakuwa tamu kama wote mmekubali? Na kama angefanikiwa kuingiza si angeniumiza sana!

Wengine wanasema ningemshitaki. Je, ningemshitaki ingekuaje? Kwanza jeshini mimi ningepewa Extra Drill mpaka niumie au kufungwa jela ya jeshi iliyojaa maji na mbu kusudi niteswe. Kumbuka ilikuwa Tanzania na yule alikuwa ni Kepiteni wakati huo na mimi nilikuwa Private. Hakuna ambaye angekuwa tayari kunisikia zaidi ya wenzangu maPrivate, na yeye alijua hivyo. SHENZI TAIPU!


Posted by Chemi Che-Mponda at 4:13 PM

Labels: Jeshi, Jeshi la Kujenga Taifa, JKT, Masange JKT, Matron, Ubakaji
 
Siwezi kuruhusu vijana wangu hasa binti zangu waende jeshini.

Wakitaka kuwa mboga hata wakienda misikitini watawakuta walafi watawashambuliatu, tatizo hao wanao wahadithia hawataki kuwaambia jinsi hao mabinti wanavyopenda kutumia miili yao kupata urahisi wa maisha. Wengine tuliopita huko tunajua jisni maafande walivyokuwa displini na vijana walivyo jifunza kutoka kwao. Big up maafande wote wa JKT Makokola pale TBR bila nyinyi pengine ningekuwa marehemu sasa hivi.
 
Dah! Nilikuwa nashadadie twende jeshini tukimaliza fm6, ila mmh! Naanza ku dought!
 
Ktk nchi ambayo viongozi wenyewe siyo wazalendo, unategemea products zake( vijana wa JKT ) wawe wazalendo?JKT y Nyerere ilitengeneza watu wazalendo kwa kuwa naye alikuwa mzalendo- "like the father like the son".
Tujiandae kuwa na kundi kubwa la vijana wenye mafunzo na ujasiri hata wa kupindua nchi!
 
..Hussein Mwinyi alikwepa kujiunga na JKT.

..sijui amepata wapi ujasiri wa kurudisha sheria hii.
 
Teh teh teh' vijana wa Chadema mjiandae kuwa wanajeshi kamili maana kama tunafanya mambo haya katika harakati za kukomboa taifa letu bila ya kujengewa moyo wa ujasiri wa kijeshi tukipitia JKT Hata uwezo wetu katika kukabiliana na polisi wakati wa maandamano utaongezeka na uoga wetu utaisha kabisa.VIJANA CHUO KIKUU WAKIAMUA KUDAI HAKI ZAO HAO ETI 'FFU' HAWATAFUA DAFU SI VIJANA WATAKUWA WANAJESHI? Na kwa wale watakaokosa kazi watajiajili wenyewe ikiwemo kutumia utaalamu wao wa siraha na mbinu za kijeshi kuibia wenye nazo,HAPO POLIS WA MWEMA WATAKIPATA CHA MTEMA KUNI maana watakuwa wanakabiliana na wanajeshi.Kiujumla jambo hili lina faida na hasara ila hasara ndio nyingi ukizingatia ufinyu wa bajeti ya sekali ya ccm na uwezo wake wa kutoa ajira ambao unaweza kuzalisha majambazi wenye ujuzi wa kivita.
 
Mm nilikuwa mmoja wapo wanaotaka JKT hirudishwe, sasa kutokana naniliyosoma hapo kwa Da Chemi nimekata shauri kwamba bora mbaya kama vp JKT hiwe ya vijana wa kiume au tuweke sheria kali hasa kwa askari hao watakaojaribu fanya vitendo hivyo lkn sema hata hawa dada zetu wengine mboga kumi watataka vyamtelemko na hawatakuwa tayari kuchapa kazi bali kugawa uroda. Mm naona nchi kwanza ishugulikie maisha ya wananchi halafu badae ndohilete huu mpango wao. Inatia hasira sana hukisoma hapo kwa Da Chemi khaa balaa.

Umesahau kuwa kuna mambo ya ushoga siku hizi?
 
Ktk nchi ambayo viongozi wenyewe siyo wazalendo, unategemea products zake( vijana wa JKT ) wawe wazalendo?JKT y Nyerere ilitengeneza watu wazalendo kwa kuwa naye alikuwa mzalendo- "like the father like the son".
Tujiandae kuwa na kundi kubwa la vijana wenye mafunzo na ujasiri hata wa kupindua nchi!

Aaah wapi? JKT ya Nyerere si ndiyo iliwapika hawa akina Lowassa, Sitta, Mahalu na mafisadi wengine? Kama umeshindwa kujenga uzalendo kwa mtu tokea akiwa mtoto mdogo hauwezi kuujenga kwa mwaka mmoja atakapokuwa JKT.
 
Tunaongelea zaidi mabaya ya JKT which is not fair, nadhani tunahitaji kuongelea na the good side of JKT baada ya hapo tupime.

Sidhani kama JKT ilikuwa imefutwa kabisa, kwasababu kuna vijana wengi sana ambao wapo JKT mpaka sasa, wao watakuwa mashuhuda wazuri sana wa yanayosemwa hapa kwenye forum.

Inawezekana yalikuwa yanatokea huko nyuma, ila kwa ulimwengu wa technolojia ya sasa itakuwa ngumu sana kuamini kuwa JKT wanaweza kuwatendea unyama huo vijana wetu.

Nadhani JKT ni sehemu nzuri sana kwa vijana wetu kujifunza uzalendo, uchapakazi, kujituma na nidhamu.

Napenda nione vijana wa kitanzania wakienda JKT
 
Hakuna faida
kuna hasara nyingi mno

1.kupoteza pesa
2.wanawake kubakwa
3.kuaandaa majambazi wa kesho
since kutakuwa na mafunzo ya ujasiri na kutumia silaha
4.kuendeleza taifa la watu waoga watiifu
5.....mengine mnaweza ongezea

Usiongee kitu hauna uhakika ndugu yangu, usipotoshe jamii - mimi nimepitia JKT na kipindi chote hakuna aliyebakwa, dada zetu wenyewe walikuwa wanawapa maafande kwa hiari yao: hadi baadhi ya maafande tukawa tunawaita mashemeji:

JKT ilikuwa na mapungufu yake sawa, ila hili la kubakwa halikuwepo.
 
JKT inahitajika kwa ajili ya kulinda uzalendo wa nchi yetu!!

Tatizo hapa ni namna ya kuliendesha kwa maslahi ya taifa, kwani naimani hiyo taasisi ikiundwa vizuri itasaidia sana kuweka mshikamano katika nchi yetu. Tatizo lingine ni kuiga iga kila kitu kutoka mataifa mengine!! " We must define our own rules and direction for the future of our country" siyo kung'ang'ana tu, eti kwa sababu marekani au jumuia ya ulaya imesema hivi basi tuache yetu mazuri na kufanya yanayowapendeza donors. Lazima tukubali US, EU na nchi zingine, hawata furahia kutuona tunajitegemea kwani utakuwa mwanzo wa wao kusambaratika.

Kuna nchi moja, iliwaaambia watalaamu wote kaeni chini mjadili nini kifanyike kwa ajili ya hiyo nchi! wanataaluma, na wasio wanataaluma walikaa wakadraft mipango yote A - Z, hadi leo vijana wa kiume (under 22yrs old) wanapiga jeshi miaka 2 then anarudi kuendelea na maisha yake, na kama akipenda kuajiriwa jeshini is up to him.

Kwa hiyo, mimi naona ni muundo tu wa mitaala (training program) inatakiwa kuwekwa vizuri, na kuweka uwazi katika inshu nzima ya namna ya training zinavyfanyika, faida yake pamoja na mambo ya kiusalama. Mfano: Kama ni kucheza mpira basi kikosi kitakachokuwa kinafanya hiyo shughuli kiweke maslahi ya taifa mbele siyo ujomba jomba, kuitana itana tu bila mpango.
 
Dah! Nilikuwa nashadadie twende jeshini tukimaliza fm6, ila mmh! Naanza ku dought!
<br />
<br />
a ha ha a wee kijana lines zako ni chachee bt u hv just make me lough out loudly almost break ma ribs. .usiogope mtu jasir z tht one acomplish unspeakable mision. .huku JF wapo watu wakilala,wakiamka wanawaza kuikosoa serikali in everthng. .nenda kawe the part of saga.
 
Kwa mazingira ya sasa JKT inaweza kuzaa 'janga la kitaifa'. Sishauri irudishwe hata kidogo badala yake serikali itumie hiyo hela kuanzisha 'vocational trainings' vyuo vya fundi stadi vingi na watoe mafunzo yanayoweza kuwafanya vijana wetu wajiariri wenyewe na watengeneze products zinazokubalika kimataifa.
 
Kwa mtu aliyepitia JKT na kushuhudia yaliyokuwa yakitendeka, maana hayo aliyoandika huyu dada ni sawa na tone la maji katika bahari tuliokuwa huko tunajua mengi zaidi ya hayo. Kwa mtu makini, hawezi kumruhusu binti yake hata mwanae wa kiume aende JKT. Kipindi kile kulikuwa ukimwa kidogo sana, lakini kwa sasa hivi ni kujiongezea janga. Hatupaswi kwenda huko!
 
Hapo hapo JKT Masange nakumbuka kuna msichana mmoja tuliyekuwa tunaishi naye, alichukuliwa na mkuu mmoja ambaye alikuwa na mwili mnene sana kisha akamtia mimba, tatizo likatokea kipindi ambacho binti ilitakiwa kutoa ile Mimba ili aendelee na mafunzo kwani aliumwa sana kiasi cha kutaka kupoteza uhai. Mungu alimjalia yule binti alipona lakini afande alifariki kabla ya binti kutoka hospitali kwani alilazwa kwa zaidi ya miezi mitatu na alivyopona hakawa hana uwezo tena wa kuzaa mpaka hivi sasa. Hivyo yule binti naye amekuwa na kumbukumbu mbaya ya JKT maishani mwake maana ilishindikana hata kurudi tena JKT.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom