BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Pongezi za CCM kwa Richard wa BBA 2 zimetushangaza
Tahariri
Tanzania Daima
TUMESHANGAZWA na kitendo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuibuka haraka haraka kumpongeza mshindi wa shindano la Big Brother 2, Richard Bezuidenhout, ambaye Jumapili iliyopita alijinyakulia kitita cha dola 100,000 za Marekani (zaidi ya sh milioni 100) kutokana na ushindi huo.
Tutangulie kueleza mapema kuwa, mshangao wetu huu haumhusu hata punje Richard, bali unaihusu CCM tu. Haumhusu Richard kwa sababu yeye alikwenda kwenye shindano, haijalishi kama shindano hilo lilikuwa likiendana na mila na desturi za Kitanzania, alichokifuata huko ugenini ni kusaka fedha.
Kamwe hatumshangai kushiriki na kushinda shindano hilo, hata kama alilazimika kufanya vitendo ambavyo haviendani na utamaduni wa Kitanzania na vilivyohatarisha ndoa yake, hayo ni matakwa yake binafsi na familia yake ilimuunga mkono.
Hatumshangai Richard kwa sababu wapo Watanzania wengi wanaotumia staili inayofanana na aliyoitumia yeye ndani ya jumba la Big Brother kusaka fedha, baadhi yao ni dada zetu wanaojihusisha na mambo ya urembo ambao hulazimika kutembea uchi mbele ya kadamnasi, lengo likiwa kusaka fedha.
Watanzania watakubaliana na sisi kuwa mashindano ya urembo ambayo hapo awali warembo walikuwa wakijitokeza mbele ya watu wakiwa na vichupi tu yalikuwa yakipingana na utamaduni wa Kitanzania.
Hili lilipigiwa kelele, likapigwa marufuku, lakini bado dada zetu wanaotuwakilisha katika mashindano makubwa ya urembo duniani, husimama mbele ya kadamnasi wakiwa na vichupi tu, jambo ambalo mbali na kukiuka utamaduni wetu, pia linawadhalilisha wao wenyewe mbele ya jamii ya Watanzania.
Tunaamini kuwa, kama shindano la Big Brother lingekuwa linafanyikia nchini, basi lingekwisha kupigwa marufuku na serikali kwa sababu si utamaduni kuangalia watu wakiwa watupu, wakioga au wakifanya vitendo vya mapenzi.
CCM, chama kinachounda serikali yetu, moja ya mambo ambayo kimekuwa kikihubiri ni kudumisha utamaduni wa Watanzania.
Akiwa ndani ya jumba la Big Brother, Richard, kijana mwenye mke, alikuwa akitazamwa na mamilioni ya watu duniani akioga uchi na akifanya mapenzi na mwanamke ambaye si mkewe.
Vitendo hivi vya Richard vilitosha kabisa kumkera mkewe, ambaye kwa mujibu wa vyombo vya habari, alilazimika kutimkia kwao mara tu aliposhuhudia vitendo hivyo vya mumewe kupitia televisheni.
Hata siku akitazama fainali hizo nyumbani kwa baba mkwe wake, alijikuta akitofautiana naye, baada ya kumsikia Richard akilitaja jina la hawara yake huyo mara tu alipotangazwa mshindi, alimtukana (Richard) akatimka ukweni kwake.
Sisi tulitegemea kuwa, CCM, ambayo serikali yake iko katika mapambano makali ya kupunguza makali ya maambukizi ya ukimwi, kamwe isingeshabikia vitendo vya ngono vilivyokuwa vikifanywa na Richard, mume wa mtu, ndani ya jumba hilo.
Ni jambo la kushangaza kwa taasisi ambayo viongozi wake wanahubiri kupambana na ukimwi, wanapanda majukwaani kupima virusi vya maambukizi ya ukimwi, kushabikia ushindi wa mume wa mtu uliochangiwa na vitendo vya mapenzi.
Tunadhani CCM imepotoka, na tunaamini kuwa tabia hii ya kudandia kila aina ya ushindi au mafanikio wanayopata Watanzania, hata kama yana walakini unaweza kuigharimu.
Turejee nyuma kidogo, tuikumbushe CCM kuwa, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ilijitokeza mbele wakati wa mapokezi yake, huku ikijua kuwa Dk. Migiro hakuteuliwa kama kiongozi wa CCM, bali wa Watanzania.
Kwa hili la Richard, CCM imetushangaza, kwa sababu mbali na ukweli kwamba haikupaswa kwa namna yoyote kushabikia ushindi huo ambao umesababisha mfarakano wa ndoa ya Mtanzania mwenzetu huyu, ni serikali ya CCM yenye dhamana ya kulinda utamaduni wa Watanzania na kuhakikisha kuwa wanaishi katika maadili mema.
CCM inapopongeza ushindi uliopatikana kwa kuonyesha uhodari wa kufanya mapenzi, tunadhani inakwenda kinyume cha misingi iliyojiwekea, inapaswa kujiangalia upya.