Kutafuta mafanikio kwa njia ya mkato ndio chanzo cha kutapeliwa

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,915
3,407
Matapeli na wezi wengine ambao wanakushawishi wewe uwape fedha au mali zako, huwa wanatumia njia hii ya mkato. Matapeli hawa wanajua kabisa watu wengi wanatafuta njia ya mkato, hawataki kuweka juhudi na wanataka kupata zaidi kwa gharama kidogo.

Hivyo huandaa mazingira ya aina hii ambayo ni rahisi kumshawishi mtu aone ni njia ya kweli ya mkato.
Ndio maana ukiuliza mtu yeyote ambaye amewahi kutapeliwa, hadithi za utapeli huwa zinafanana, mtu ana madini lakini hajui akauze wapi, anakuambia umsaidie na atakupa nusu ya fedha, baadaye anakwambia ulipie gharama fulani halafu mkishauza madini atakurudishia gharama hizo pamoja na faida kubwa.

Ukishatoa gharama unaachwa kwenye mataa huku ukiwa umebeba vyupa unavyofikiri ni madini. Sasa kama na wewe unatafuta njia ya mkato halafu ukakutana na watu hawa, ni rahisi sana kutapeliwa. Hivyo kama unataka usitapeliwe, acha kutafuta njia ya mkato.

Jua kabisa chochote kizuri kinakuja baada ya kuweka kazi kwa juhudi na kuwa mvumilivu. Akitokea mtu yeyote na kukuambia kuna njia rahisi ya kufanikiwa au ya kushinda au ya kutajirika, wala usimuulize njia hiyo ikoje, utajikuta umeshashawishika kwamba kuna njia ya aina hiyo na ukaenda kupoteza muda wako na fedha zako pia.

Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani
 
Ahsante Makirita. Umeongea ukweli. Pale mwishoni unaonaje ungeondoa maneno "kocha wako"? Ni ushauri tu nautoa kwa nia nzuri.
 
Hilo la Kocha wako linazuia nini mkuu?
Naona palipo na anaeitwa au kujiita coach pana anaekuwa coached. Sasa kwa sababu hapa kilichopo ni "sharing" ya yale tunayoyafahamu pengine kuna baadhi ya watu ambao tunaweza kuwa tunaona ugumu wa kukubali kwamba fulani ni "kocha wangu". Pengine naweza kuwa siko sahihi lakini hayo ndiyo mawazo au mtazamo wangu kwa sasa.
 
Sawa,
Kwa mtu aliye chanya na aliye tayari kujifunza hawezi kuona tatizo la neno Kocha.
Ila kwa mwenye mtazamo wa tofauti hilo litamsumbua.
 
Lakini hata hivyo ukisubiri upate mafanikio kwa njia ya halali unaweza zeeka unatafuta angalia wazee wetu wakulima kule vijijini linganisha na hawa wanasiasa janja janja wakati mwingine inabidi uwe mbunifu na ujaribu kuibiwa ni kujifunza.
 
Usijidanganye kwa hili,
Mafanikio ambayo siyo kwa njia ya halali hayadumu.
 
Back
Top Bottom