Kutafuta Ajira Kunavyoweza Kumuathiri Mtu Kisaikolojia! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutafuta Ajira Kunavyoweza Kumuathiri Mtu Kisaikolojia!

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Yona F. Maro, Jul 4, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jul 4, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Wengi wao wamekuwa wakikumbana na vikwazo vingi na manyanyaso ambayo yamewaathiri kisaikolojia na kujikuta wakijiingiza katika tabia mbaya au kuwa watu waliochanganyikiwa akili.

  Utafutaji kazi si suala jepesi katika nchi kama hii ambayo ajira ni ngumu. Hatua iliyopo sasa ni kwa vijana wengi kuona ni rahisi kusoma kuliko kupata ajira. Pengine huu ni ukweli ambao umewafikisha wengi katika tabia za ukahaba na uvutaji bangi kutokana na kukosa ajira licha ya kupata elimu.

  Inahuzunisha na kukatisha tamaa pale kijana anapoingia ndani ya ofisi na kukumbana na majibu ya hovyo kutoka kwa katibu muhtasi wa meneja aliyemwendea kuomba ajira.

  Kwa mfano msomi mwenye vyeti na taaluma anapojibiwa hivi! “Aliyekuambia hapa kuna kazi nani, wee unafikiri kwa cheti chako hiki unaweza kupata kazi hapa, labda ya kufagia.

  “Kaka nimekuambia hakuna kazi hebu ondoka wapishe wenye shida za maana wamuone bosi, unaganda kama ruba?”
  Ni wazi kwamba maneno ya namna hii yanapomwingia akilini kijana huku akiwa na ufahamu kuwa kuna vijana wenzake aliokuwa akiwazidi alama shuleni wameajiriwa kwenye ofisi nyeti za serikali, itamuathiri sana kisaikolojia na kitakachotokea ni ukataji tamaa.

  Pengine kwa kufahamu hilo na kuwa mmoja kati ya mshauri niliyekutana na makundi ya vijana wasomi ambao wamegeuka walevi na ombaomba, nimelazimika kuandika makala haya ili kuwaimarisha kisaikolojia.

  Kwa upembuzi wangu ambao umeshibishwa na makala ya Jay Crawford wa Marekani iliyoitwa “Tips on what Not to do when seeking employiment, nimelazimika kuandika makala haya ili niwape dokezo kadhaa vijana wenzangu wanaosaka ajira. Zifuatazo ni dondoo chache za muongozo!

  UCHUNGUZI NI MUHIMU
  Ofisi nyingi na hasa zisizohitaji wasomi wenye taaluma zimejiwekea utaratibu wake wa kufuata katika kuwapatia kazi za muda watu. Hivyo ni muhimu kwa msaka kazi kwenye eneo la aina hiyo akafanya uchunguzi kupitia kwa rafiki zake waliomtangulia hapo, ili ajue la kufanya atakapofika kuomba nafasi ya kuwa kibarua wa wiki au siku. Hii ni kwa wale ambao hawana taaluma. Maana si busara kukurupuka na kumwingilia bosi ofisini bila kufahamu utaratibu, unaweza kufukuzwa badala ya kusikilizwa.

  UTUNZE NA KUUKUZA UJUZI WAKO
  Inashauriwa kuwa, mtu anapomaliza masomo na kupata taaluma yake ni bora akautunza ujuzi wake kwa kujisomea na kujikumbusha kile alichosomea. Hii itamsaidia kushinda katika usaili wakati akisaka kazi. Hivyo ni bora kwa msaka ajira kukubali kufanya kazi za muda ili kujizoeza, si busara kukaa nyumbani na vyeti ukisubiri ajira. Fahamu kuwa wakati ukijitolea ni rahisi kufahamika na watu na hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata ajira.

  USITAFUTE AJIRA KWA PUPA
  Watafutaji wengi wa ajira huwa na kasoro ya kufanya mambo kwa pupa, hujikuta wakikusanya nguvu nyingi kwa wakati mmoja na kukimbia huku na kule kutwa nzima kutafuta kazi. Mara nyingi watu wa aina hii huwa kama wendawazimu wakipita hata kwenye maofisi ambayo hayaajiri watu wenye taaluma zao.

  Jambo hili ni baya kwani huwaondolea umakini na linachosha kwa kiasi kikubwa. Kinachotakiwa ni utulivu na ufuataji wa taratibu zilizopo za kutafuta kazi. Kwa mfano, mbali na matangazo ya kazi kutolewa kuwaruhusu watu wenye sifa kuandika barua za maombi, nchini kwetu kuna njia ya kutumia marefa ambao wamo ndani au karibu na waajiriwa. Njia hizi ni bora na zinaheshima.

  Kwa mujibu wa wataalam wa masuala ya kisaikolojia watu wengi wanaofanya mambo yao kwa pupa hukabiliwa na hatari kubwa ya kukata tamaa hasa wanapokutana na mikwamo.

  Ni rahisi kwa mwenye pupa kukosa njia mbadala ya kupambana na kikwazo, kutokana na ukweli kwamba wakati akishindana katika hatua za awali alitumia kiwango kikubwa cha nguvu, hivyo anapotafakari juhudi za kuongeza hujikuta akigota katika jibu la haiwezekani kushinda.

  KUBALI MATOKEO YA HASI
  Watafuta kazi wengi huwa hawako tayari kukubaliana na matokeo hasi. Mara nyingi wanapojaribu na kukosa hujiona kama ni watu wenye mikosi. Lakini ukweli unabaki kuwa kuthubutu ndiyo mwanzo wa ushindi wa kila jambo.

  Hivyo ni busara kujaribu kuomba kazi na kuwa tayari kupata jibu la umeshindwa. Hakuna ubaya pale mtu anapokosa baada ya kujaribu, kwani kushinda ni zao la majaribio.

  USIJILINGANISHE NA WENGINE
  Watu wengi wamejikuta wakiathirika kisaikoloji kutokana na kasumba ya kujilinganisha na wengine. Ni hatari kubwa kumchukua mtu uliyekuwa ukimshinda masomo darasani na kumuingiza katika kipimo chako cha kukosa! Utajikuta ukiibuka na maswali mengi magumu, yatakayokufanya ujione kama ni mtu usiyestahili kupata mafanikio.

  Siku zote unapotafuta ajira simama kama wewe hata kama umemkuta rafiki yako mbumbu akiwa ofisa, usiangalie nyuma, weka mbele bahati yako na usiilalie mlango wazi ya mwenzako.

  GLOBALPUBLISHERS
   
 2. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  wale masekretari wana kauli mbaya sana....
   
 3. K

  Kokolo JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2008
  Joined: Mar 20, 2008
  Messages: 487
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Kuwa na masters siyo sababu, inabidi ujiajili
   
 4. N

  Nzinyangwas New Member

  #4
  Sep 22, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli uliyosema ila Mwenyezi Mungu ndio wa kumtanguliza. Unatakiwa kuwa na Subira na kuwa mvumilivu. Kusoma wakati unatafuta kazi ni muhimu sana kwani Elimu ni tofauti na vitu vingine, 'elimu usipoitumia inachakaa!'
   
 5. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Its killing,humuliating,discouraging,degradeful and disgusting once you have no godfather or godmother!
   
 6. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ingependeza kama kungekuwepo na wakala wa serikali wa kuwatafutia watu kazi wakati ule wanapomaliza vyuo.
   
 7. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Shy..Nakubaliana na wewe na hasa kwenye kipengere cha kukubali matokeo hasi na kujilinganisha na wengine...Ni mambo magumu ambayo kama huna roho ya ujasiri inaweza kukupotezea hata umakini katika mikakati yako ya kutafuta ajira... Kwani kuna jamaa niliosoma nao class moja Chuo na walikuwa wabovu kupindukia lakini huwezii kuamini wote wamepata kazi nzuri TRA wanakula maisha....
   
 8. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #8
  Sep 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Kuna ndugu yangu alienda TRA akaambiwa akitaka kazi atoe ml 5 eti zinanunuliwa na sehemu nyingi sana za kazi sikuhizi wanafanya hivyo kuuza kaazi
   
 9. m

  muasisi Member

  #9
  Sep 22, 2008
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shy iyo article kuhusu ajira ipo safi sana na kiukweli mimi kama jobseeker imenijenga sana,siunajua ndo kwanza nimemaliza chuo thanx bro!
   
Loading...