Kutabiria kifo wagombea, Sheikh Yahya akamatwe, ashitakiw

Feb 15, 2009
99
2
by Joseph Mihangwa

HABARI kwamba mnajimu Sheikh Yahya Hussein ametabiri ya kuwa mwana-CCM yeyote atakayejitokeza kuchukua fomu kugombea Urais kumpinga Rais aliye madarakani, Jakaya Kikwete katika uchaguzi ujao, atakufa ghafla, zimeibua hoja na hisia mbali mbali miongoni mwa jamii ya Watanzania.

Wengi wanaona kuwa mnajimu huyo si tu kwamba anatumika kumsafishia njia Rais Kikwete kwa kutumia vitisho, bali pia kwamba Taifa linaingizwa katika mkondo wa aibu wa utamaduni wa kishirikina, hasa pale Serikali inapoamua kunyamazia, na pengine kuunga mkono, utabiri huo.

Watanzania wana kila sababu ya kushituka kwa utamaduni huo kuvamia na kuteka mstakabali wa Taifa na uongozi wa nchi kwa ujumla, wakijua kuwa ushirikina haujengi bali huangamiza jamii. Sote tu mashahidi, kwamba mauaji mengi ya vikongwe Kanda ya Ziwa, na wimbi la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini (albino) yanatokana na imani potofu za kishirikina. Ni balaa iliyoje itakayotokea, kwa Taifa kukumbatia ushirikina katika siasa na uongozi wa nchi?. Ni balaa iliyoje kwa nchi kuongozwa kwa imani za kishirikina?.

Mfalme Sauli, aliyetawala kati ya mwaka 1,000 - 900 Kabla ya Kristo (KK), alijimaliza mwenyewe alipoamua kushirikisha imani potofu za ushirikina na washirikina katika uongozi na utawala wake, kwa sababu imani za kishirikina zinapumbaza na kumfanya mtu kinyago asiyefikiri wala kutenda ila kwa ushauri wa “mganga” wake.

Kwa mujibu wa Biblia, 1 Samwel 15: 10, 11, 16:11, inaelezwa kuwa, kwa kutegemea nguvu za giza badala ya kumtegemea Mungu mwenye haki na upendo kwa watu, Sauli alikosa maono wala ushauri, akapwaya; ufalme wake ukayumba. Na hata alipoomba msaada wa mchawi wa Endori kumpandishia Samweli kuja kushauri, haikusaidia kitu; majeshi ya adui (Wafilisti) yakauangamiza ufalme wake (1 Samweli 28: 1-19).

Vivyo hivyo, taifa lolote linapoongozwa na washirikina (wa aina ya akina Sauli, Mobutu Sese Seko, Idi Amin, Marcias Nguema na wengine) hukosa maono, na hivyo huangamia; taifa linapokosa ushauri bora (ila ushirikina), na pasipo ushauri, taifa hilo huanguka, kama ulivyoanguka ufalme wa Sauli.

Mambo haya hayapashwi kutokea enzi zetu hizi za uhuru, demokrasia, na maendeleo, sayansi na teknolojia inayokomaza fikra na ustaarabu wa binadamu. Nao viongozi wa kitaifa hawapaswi kuyakaribisha haya wala kuyafumbia macho.

Kila kiongozi wa kitaifa ana dini yake yenye kumwamini Mungu mmoja. Ndiyo maana viongozi wakuu huapa kwa misahafu ya dini zao zenye kumtambua Mungu mmoja, ili kuitetea Katiba ya nchi wachukuapo madaraka; wala hawaapi kwa misahafu ya kishirikina inayoongozwa na upigaji ramli au unajimu wa akina Sheikh Yahya.

Katiba ya nchi ambayo viongozi huapa kuilinda na kuitetea ni katiba ya watu iliyotungwa na wananchi kuendesha mustakabali wa taifa lao kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.

Na kwa kuwa watu na taifa ni watu na Taifa la Mungu, yampasa kiongozi anayewaongoza kumtii Mungu kwa mujibu wa imani yake iliyomfanya aape kwa kutumia msahafu wa imani hiyo, ili aweze kufunuliwa maono na ushauri sahihi wa kuongoza; vinginevyo kiapo hakina maana katika suala zima la uongozi.

Na kama kweli viapo vyetu vina maana katika uongozi na si unafiki, basi kitendo chochote cha kuhusisha ushirikina katika uongozi kwa kiwango chochote kile kinaweza kutafsiriwa kuwa ni ukiukaji wa kiapo (perjury) na katiba ya nchi.

Utabiri wa hivi karibuni, wa Sheikh Yahya Hussein umewaacha wengi wakijiuliza maswali mengi: je, Sheikh Yahya katumwa au anatumika; akili ya kawaida inafanya tushindwe kujizuia kuamini kwamba ramli hiyo imekusudiwa kutumika kama silaha ya kisiasa, kama njia moja ya kujenga hofu miongoni mwa umma na kugandisha mchakato wa kisiasa nchini kwa sindano ya ganzi ya kishirikina, hasa katika kipindi hiki ambacho Taifa linahitaji uongozi bora wenye maono kuweza kulikwamua katika matatizo yake.

Ilidhaniwa kwamba Serikali ingeweza kukemea kitendo hicho cha Sheikh Yahya cha kutaka kupenyeza imani za kishirikina katika mkondo wa utawala na siasa za nchi.

Kinyume chake wengi wameshitushwa na tamko la Ikulu, kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Mawasiliano, Salva Rweyemamu, kwamba “maoni ya Sheikh Yahya yanastahili kuheshimiwa” bila shaka kwa maana kwamba yana mantiki kwa kiwango cha msemaji na walengwa, na hivyo kwa jamii ya Kitanzania.

Hatua ya Ikulu ya kuzungumzia kwa staili ya kuutetea utabiri huo haiwezi kutafsiriwa vinginevyo mbali na ile ya utayari wa Ikulu hiyo kukaribisha nguvu za ushirikina kwenye mkondo wa Serikali. Kama isingekuwa hivyo, Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) vingemkana Sheikh Yahya na ramli zake, ikizingatiwa kwamba tunayo sheria inayozuia vitendo kama hiki, kama itakavyoelezwa baadaye kidogo kutoka makala haya kwamba Sheikh huyu alipaswa kukamatwa na kushitakiwa mara moja. Na kama Serikali itaendelea kumkumbatia, basi umma wa Kitanzania utaamini kwamba Taifa limejiteulia mnajimu wake.

Alichotenda Sheikh Yahya ni ushirikina ulio dhahiri ukihusisha “ndumba” au “ndonga”, kwa kujifanya kuwa ana nguvu ya “mizungu” – ukihusisha fumbo au siri; kwa lugha nyingine occult forces...............

Raia Mwema
 
Hii makala nimeipenda sana. Nadhani tumefika mahali ambapo inatubidi kufanya maamuzi magumu. Hatuwezi kuendelea na michezo hii ya karne ya 17 ya kuendesha nchi kwa masharti ya sangoma.

Hii makala pia imenipa majibu ya maswali ambayo nilikuwa najiuliza kwa muda mrefu sana. Inakuwaje mtu mashuhuri kama alivyokuwa Mkapa ahangaike na cheni na mipete mikubwa? Tunahitaji ufumbuzi wa kuwatokomeza hawa akina Shekh Yahya na Maprofresa/madokta wa mitishamba wanaondekeza uchawi katika karne hii ya sayansi ya mambo teknolojia!
 
by Joseph Mihangwa

HABARI kwamba mnajimu Sheikh Yahya Hussein ametabiri ya kuwa mwana-CCM yeyote atakayejitokeza kuchukua fomu kugombea Urais kumpinga Rais aliye madarakani, Jakaya Kikwete katika uchaguzi ujao, atakufa ghafla, zimeibua hoja na hisia mbali mbali miongoni mwa jamii ya Watanzania.

Wengi wanaona kuwa mnajimu huyo si tu kwamba anatumika kumsafishia njia Rais Kikwete kwa kutumia vitisho, bali pia kwamba Taifa linaingizwa katika mkondo wa aibu wa utamaduni wa kishirikina, hasa pale Serikali inapoamua kunyamazia, na pengine kuunga mkono, utabiri huo.

Watanzania wana kila sababu ya kushituka kwa utamaduni huo kuvamia na kuteka mstakabali wa Taifa na uongozi wa nchi kwa ujumla, wakijua kuwa ushirikina haujengi bali huangamiza jamii. Sote tu mashahidi, kwamba mauaji mengi ya vikongwe Kanda ya Ziwa, na wimbi la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini (albino) yanatokana na imani potofu za kishirikina. Ni balaa iliyoje itakayotokea, kwa Taifa kukumbatia ushirikina katika siasa na uongozi wa nchi?. Ni balaa iliyoje kwa nchi kuongozwa kwa imani za kishirikina?.

Mfalme Sauli, aliyetawala kati ya mwaka 1,000 - 900 Kabla ya Kristo (KK), alijimaliza mwenyewe alipoamua kushirikisha imani potofu za ushirikina na washirikina katika uongozi na utawala wake, kwa sababu imani za kishirikina zinapumbaza na kumfanya mtu kinyago asiyefikiri wala kutenda ila kwa ushauri wa “mganga” wake.

Kwa mujibu wa Biblia, 1 Samwel 15: 10, 11, 16:11, inaelezwa kuwa, kwa kutegemea nguvu za giza badala ya kumtegemea Mungu mwenye haki na upendo kwa watu, Sauli alikosa maono wala ushauri, akapwaya; ufalme wake ukayumba. Na hata alipoomba msaada wa mchawi wa Endori kumpandishia Samweli kuja kushauri, haikusaidia kitu; majeshi ya adui (Wafilisti) yakauangamiza ufalme wake (1 Samweli 28: 1-19).

Vivyo hivyo, taifa lolote linapoongozwa na washirikina (wa aina ya akina Sauli, Mobutu Sese Seko, Idi Amin, Marcias Nguema na wengine) hukosa maono, na hivyo huangamia; taifa linapokosa ushauri bora (ila ushirikina), na pasipo ushauri, taifa hilo huanguka, kama ulivyoanguka ufalme wa Sauli.

Mambo haya hayapashwi kutokea enzi zetu hizi za uhuru, demokrasia, na maendeleo, sayansi na teknolojia inayokomaza fikra na ustaarabu wa binadamu. Nao viongozi wa kitaifa hawapaswi kuyakaribisha haya wala kuyafumbia macho.

Kila kiongozi wa kitaifa ana dini yake yenye kumwamini Mungu mmoja. Ndiyo maana viongozi wakuu huapa kwa misahafu ya dini zao zenye kumtambua Mungu mmoja, ili kuitetea Katiba ya nchi wachukuapo madaraka; wala hawaapi kwa misahafu ya kishirikina inayoongozwa na upigaji ramli au unajimu wa akina Sheikh Yahya.

Katiba ya nchi ambayo viongozi huapa kuilinda na kuitetea ni katiba ya watu iliyotungwa na wananchi kuendesha mustakabali wa taifa lao kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.

Na kwa kuwa watu na taifa ni watu na Taifa la Mungu, yampasa kiongozi anayewaongoza kumtii Mungu kwa mujibu wa imani yake iliyomfanya aape kwa kutumia msahafu wa imani hiyo, ili aweze kufunuliwa maono na ushauri sahihi wa kuongoza; vinginevyo kiapo hakina maana katika suala zima la uongozi.

Na kama kweli viapo vyetu vina maana katika uongozi na si unafiki, basi kitendo chochote cha kuhusisha ushirikina katika uongozi kwa kiwango chochote kile kinaweza kutafsiriwa kuwa ni ukiukaji wa kiapo (perjury) na katiba ya nchi.

Utabiri wa hivi karibuni, wa Sheikh Yahya Hussein umewaacha wengi wakijiuliza maswali mengi: je, Sheikh Yahya katumwa au anatumika; akili ya kawaida inafanya tushindwe kujizuia kuamini kwamba ramli hiyo imekusudiwa kutumika kama silaha ya kisiasa, kama njia moja ya kujenga hofu miongoni mwa umma na kugandisha mchakato wa kisiasa nchini kwa sindano ya ganzi ya kishirikina, hasa katika kipindi hiki ambacho Taifa linahitaji uongozi bora wenye maono kuweza kulikwamua katika matatizo yake.

Ilidhaniwa kwamba Serikali ingeweza kukemea kitendo hicho cha Sheikh Yahya cha kutaka kupenyeza imani za kishirikina katika mkondo wa utawala na siasa za nchi.

Kinyume chake wengi wameshitushwa na tamko la Ikulu, kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Mawasiliano, Salva Rweyemamu, kwamba “maoni ya Sheikh Yahya yanastahili kuheshimiwa” bila shaka kwa maana kwamba yana mantiki kwa kiwango cha msemaji na walengwa, na hivyo kwa jamii ya Kitanzania.

Hatua ya Ikulu ya kuzungumzia kwa staili ya kuutetea utabiri huo haiwezi kutafsiriwa vinginevyo mbali na ile ya utayari wa Ikulu hiyo kukaribisha nguvu za ushirikina kwenye mkondo wa Serikali. Kama isingekuwa hivyo, Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) vingemkana Sheikh Yahya na ramli zake, ikizingatiwa kwamba tunayo sheria inayozuia vitendo kama hiki, kama itakavyoelezwa baadaye kidogo kutoka makala haya kwamba Sheikh huyu alipaswa kukamatwa na kushitakiwa mara moja. Na kama Serikali itaendelea kumkumbatia, basi umma wa Kitanzania utaamini kwamba Taifa limejiteulia mnajimu wake.

Alichotenda Sheikh Yahya ni ushirikina ulio dhahiri ukihusisha “ndumba” au “ndonga”, kwa kujifanya kuwa ana nguvu ya “mizungu” – ukihusisha fumbo au siri; kwa lugha nyingine occult forces...............

Raia Mwema

Jamani msiniquote vibaya, kunitupia mawe wala kunipiga... kama ni kweli sheikh yahya kasema hivi then its the most ridiculous thing I have ever heard. Anawaogopesha watu na watu wanaogopa mpaka wana JF ndio maana hakuna hata mmoja anayepinga/kuchangia hii mada ingawa wote tunajua kuwa he is wrong maana mnahisi huko mliko Sheikh atawajua tu na atawaua pia.
 
Huo ni utabiri tuu kama unajua nini maana ya utabiri let the man do so sio kwamba ataenda kumuua huyo mtu ili maneno yake yawe sawa yeye katabiri kama jaumuamini usimsikilize
 
But still, si angenyamaza tu. Kuna sababu gani ya kusema hivyo wakati anajua kuna watu watagombea? si nikuwaogopesha?
 
Back
Top Bottom