Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,187
- 671
kipindi hiki kifupi kuna mambo mengi yamejitokeza
mengine yametushangaza na kutuhunisha na kutuacha vinywa wazi
hivi ni kweli haya tunayoyasikia yanatokea nchini kwetu Tanzania au .....
tumesikia waandishi kutiwa tindi kali kwa wengine baada ya muda mfupi kuhojiwa na tume ya Richmond
huko nyuma baadhi ya wabunge walinena wanatishiwa maisha yao na watu wasiojulikana.
marehemu dada yetu Amina(RIP) pia aliwahi kuteta kuwa kuna watu wanamtishia maisha yake.
leo tunasikia mengine yametokea kiteto hatujatulia vyema sasa mambo yamefika JF
inanikumbusha ile nyimbo yetu ya kitoto
Nyooka huyooo yuko Makunduchi husema na apite
nyoooka huyooo yuko muyuni husema naapite
kidogo kidogo hadi nyoka anakaribia miguuni
na si muda tunapiga kelele mwenzetu lakiwa na nyoka
kwa wale wenye rika kama langu wanaikumbuka vyema nyimbo hii, huyu nyoka sasa naona keshapea na anahatarisha maisha ya watu na nyimbo hii inaonyesha jinsi kuona na apite maadam anapita kwa mbali hatudhuru sie si tatizo.
wakati tunao wa kuamua kusuka au kunyoa.
ni kuamua kwa makusudi kukomesha vitendo hivi na kuwafichua na kuwawajibisha wenye mchezo huu mchafu wa kutishia amani ya taifa letu kipenzi.
hili si suala la vyama maana vyama vyote pia wabunge wao walionesha kuwa wanatishwa na nyoka huyu hata wajumbe wa tume karibuni walieleza kutishwa na nyoka huyu
nyoka huyu tumsakeni na tumuue uwanjani mchana kweupee ili liwe funzo kwa wengine