Kusudio la Mpendazoe latupwa; Jaji Mkuu M. Chande aamuru kusudio hilo liondolewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kusudio la Mpendazoe latupwa; Jaji Mkuu M. Chande aamuru kusudio hilo liondolewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gumzo, Sep 11, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=3]JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, ameamuru taarifa ya kusudio la kukata rufaa iliyowasilishwa katika Mahakama ya Rufani na Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fredy Mpendazoe, iondolewe.[/h]
  Mpendazoe aliwasilisha kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, katika kesi yake ya uchaguzi wa Jimbo la Segerea.

  Katika kesi hiyo namba 98 ya mwaka 2010, Mpendazoe alikuwa akipinga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Dk. Makongoro Mahanga, wa Chama cha Mapinduzi (CCM).Mahakama Kuu katika uamuzi wake uliotolewa na Jaji Profesas Ibrahim Jumaa, alimthibitisha Dk Mahanga kuwa ni mbunge halali wa jimbo hilo.

  Alisema Mpendazoe alishindwa kutoa ushahidi wa kuthibtisha madai yake ya kupinga matokeo hayo.
  Kutokana na uamuzi huo, Julai 12, 2012, Mpendazoe kupitia kwa Wakili wak e, Peter Kibatala, aliwasilisha katika Mahakama ya Rufani taarifa ya kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, kutokana na kutokuridhika nayo.

  CHANZO: GUMZO LA JIJI
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Tunawasubiri 2015
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading"]Monday, 10 September 2012 22:15[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]James Magai

  JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, ameamuru taarifa ya kusudio la kukata rufaa iliyowasilishwa katika Mahakama ya Rufani na Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fredy Mpendazoe, iondolewe.

  Mpendazoe aliwasilisha kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, katika kesi yake ya uchaguzi wa Jimbo la Segerea.

  Katika kesi hiyo namba 98 ya mwaka 2010, Mpendazoe alikuwa akipinga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Dk. Makongoro Mahanga, wa Chama cha Mapinduzi (CCM).Mahakama Kuu katika uamuzi wake uliotolewa na Jaji Profesas Ibrahim Jumaa, alimthibitisha Dk Mahanga kuwa ni mbunge halali wa jimbo hilo.

  Alisema Mpendazoe alishindwa kutoa ushahidi wa kuthibtisha madai yake ya kupinga matokeo hayo.
  Kutokana na uamuzi huo, Julai 12, 2012, Mpendazoe kupitia kwa Wakili wake, Peter Kibatala, aliwasilisha katika Mahakama ya Rufani taarifa ya kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, kutokana na kutokuridhika nayo.

  Hata hivyo Jaji Mkuu Othman alimuru taarifa hiyo iondolewe mahakamani hapo chini ya Kanuni ya 89 (1) ya Kanuni za Mahakama ya Rufani za mwaka 2009.

  Jaji Mkuu Othman alitoa amri hiyo Agosti 2, 2012, baada Mpendazoe kuamua kuachana na azma yake ya kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.

  Mpendazoe, kupitia kwa wakili wake, Kibatala ambaye ni Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS), aliwasilisha taarifa hiyo ya kuachana na rufaa hiyo, Mei 7, 2012.Kwa uamuzi huo, Mpendazoe ameamua kuachana na rufaa hiyo na hivyo kumpa nafasi Dk Makongoro kuendelea na wadhifa wake huo hadi muhula uchaguzi mkuu ujao.

  Wakili Kibatala aliliambia Mwananchi jana kuwa, Mpendazoe aliamua kuachana na rufaa hiyo baada ya kushauriana na chama chake, kutokana na ufinyu wa muda uliosalia.

  Alisema kutokana na ufinyu huo wa muda, Mpendazoe aliona kuwa badala ya kupoteza muda kwa ajili ya rufaa hiyo, sasa anajipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

  Katika taarifa yake ya kusudio la kukata rufaa, Mpendazoe alisema kuwa anakusudia kukata rufaa kupinga hukumu yote ya Mahakama Kuu, huku akiiomba mahakama iwapatie nyaraka mbalimbali zianazohusiana na kesi hiyo kwa ajili ya kuandaa hoja za rufaa.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Jaji Mkuu pia anaegemea CCM? Sikujua anaweza kuingilia Masuala ya UBUNGE wakati kuna Majaji wa Mahakama ya RUFAA na JAJI

  KIONGOZI
   
 5. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mpendazoe mwenyewe si ndio kaamua kuittoa kesi?
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwanini Jaji Mkuu AIINGILIE?
   
 7. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Acha kukurupuka soma Habari yote uelewe unafukuzwa na Mr Cameroon nini umekimbilia kulaumu tu.Darasa la Saba mnasumbua mno sasa hivi hapa Jf
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Umesahau kuwa Chande ni rafiki ya Kikwete. Hawezi kupitisha uamuzi ambao utadhuru maslahi ya rafiki yake.
  Kuna topic moja kaanzisha Mheshimiwa Mbunge kuhusu utawala wa kifamilia. Inafaa uitupie macho pia.
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Hata hivyo ni kitendo cha kiungwana kutuokoa na gharama za uchaguzi.
  Hongereni kwa uamuzi huo. Ni kujipanga for next time na kuhakikisha makosa hayarudiwi.
  Hongera Mpendazoe.
   
 10. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Read between the lines
   
 11. i

  iseesa JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Na ndo anakwenda kwa Rufaa ya Kamanda Lema. TAFAKARI
   
 12. S

  Sobangeja Senior Member

  #12
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 184
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Wandugu, ni Mpendazoe mwenyewe aliamua kuachana na kesi hiyo tangu tarehe 17 May,2012 baada ya kushauriana na chama chake kwa kuwa muda umekuwa mfinyu sana.Anajipanga kwa uchaguzi ujao.Jaji mkuu Chande yeye amekubaliana na maamuzi ya Mpendazoe na siyo ameifuta kesi husika kwa matakwa yake yeye.
   
Loading...