Kusudio la kuwasilsha Hoja Binafsi Bungeni: Lema amtolea uvivu Hussein Bashe, Zitto amuunga mkono

Mbunge Lema asema aliyoyasema bashe si sawa
Na hayafai kabisa

Pambaneni mpate wabumge wengi bungeni, sio kupiga kelele wakati nyie ndio minority, ndio demokrasia hiyo. Yaani Lema anataka wabunge wa sisiemu wawe kama wabunge wa chadema?? THAT WILL NEVER HAPPEN. Wengi ndio wanafanya maamuzi.

Pia ni wapi INALAZIMIKA kwa mbunge wa sisiemu kwenda kumjulia hali Lissu huko huko??
Lema acha kulia lia, siasa mmezishindwa.
 
Uamuzi aliuchukua bashe ni juhidi zake binafsi za kutka kuleta mabadiliko zaidi, ni uamuzi wa kupongezwa, Bashe sio taasis ya ccm au bunge yeye ana asisi tu huo mchakata agaist all instutions ambazo anaona zimekuwa inaffective, nani ajua anweza kuwa mbegu ya mabadiliko tunayotaka kuyaona? Usitigemee sana taasis yenyewe kubadilika bila juhudi za induviduals.
 
Lema ahoji kama muheshimiwa sio kama mvuta bange. Bashe kachagua njia hiyo, yeye Lema achague njia nyingine au ashauri vinginevyo. Hata bandiko lake ni kama kelele tu bila alternative.
 
Hivi Kumsalimia Lissu ni kitu cha lazima? si utashi wa mtu mbona kila mbunge analiweka swala la kumsalimia Lissu kama ngao kabisa.....maana kuna watu kibao hata wazazi wao wakiungua hawaendi kuwasalimia....kwenda msalimia Lissu au kumpa pole linakuwa ni kama lazima.....
 
Nimemuelewa Lema..

Hata Bashe analifahamu hili, wingi wa wabunge wa CCM pale bungeni umekuwa ni HASARA kubwa badala ya kuwa FARAJA kwa Taifa..

Ukandamizaji wa Demokrasia na Wapinzani umesimamiwa na Wabunge wenyewe wa CCM kupitia vikao vyao vya Party Caucus na Vikao Halali vya ndani vya chama hicho..

Seriousness ya Wabunge wa CCM ilipimwa na wananchi wakati ule Lissu alivyopigwa risasi. Wabunge wote walipaswa kuchachamaa mle ndani bila kujali itikadi zao lakini ilikuwa kinyume chake..

Sioni hoja ya Bashe ikitatua tatizo.
Kwa nini wao wako wachache??
 
Kwa maoni yangu, Bashe is good na level ya hoja za Bashe, Zitto pia ni level hiyo hiyo, wanatanguliza mbele maslahi ya taifa, vision yao ni broader perspective. Lema ni level nyingine, ili Lema aweze kufikia levels za uelewa hoja za mtu kama Zitto au Bashe, hakuna jinsi nyingine yoyote ni shule tuu!. Lema kwenye uhamasishaji he is very good na anakubalika sana kwa machalee wa Arachuga, tatizo lake ni moja tuu, shule!.

Kuna wabunge wengi wana tatizo hili la shule, wale wanaojitambua na kujikubali, utawasikia wamejinyamazia, na wale wasiojitambua type kama ya Kibajaji, atawasikia jinsi walivyo madebe matupu!. Ushauri kwa Mhe. Lema asiwe mwepesi ku react kwenye hoja zinazomzidi kimo.

P
Nakubaliana na wewe Mkuu Pasco.
Mdomo kila mtu anao, lakini kwa kutumia akili Lema awapishe wenye uwezo wa kuzitumia.
 
Ungeenda umbali zaidi. Kwamba hili la Bashe linahitaji mjadala wa walioelimika zaidi, siyo (kwa kiwango gani,labda?). Unafikiri hili la hoja ya Bashe litakuwa geni Bwana Paskali. Hebu kabla hujampuuza Lema kwa hoja ya elimu, nenda kamuulize Adadi Rajab kama Bunge liko tayari kuzungumzia mambo haya, kwa maana ya kuutafuta ukweli wenyewe. Paskali anayehusudu wasomi wa aina ya Zitto anajifanya hajui kuwa, "wajinga" wa aina ya Lema wanajua kuwa wasomi wa aina ya Zitto ni wepesi mno kwenye masuala kama haya yanayoshirikisha akili (ambazo siyo lazima ziwe za shule) kuyashughulikia!

Swali langu kwa Paskali: Kama wasomi wa aina ya Bashe na Zitto wakifanikiwa kulifikisha jambo hili bungeni na likaenda kuishia huko huko, litaibukia wapi wapi tena? Tunahitaji kutumia Bunge letu dhaifu hili kwenda kuisafisha serikali ya CCM?
Kumbe wangefanyaje kina Bashe? ndicho Lema alitakiwa aseme! Hata kama hoja ya Bashe itapotea huko bungeni hakutakuwa na hatua za kuchukua kwa umoja wetu?
 
hata mimi namuunga mkono Lema na kila mara uwa namsifu sana Lema kwani hoja zake huwa zina mashiko makubwa, hivi watanzania tuna hakili kweli? eti tuunde tume ya kuchunguza kufifia kwa demokrasia ndani ya vyama wakati aliyezuia mikutano ya vyama anajulikana,waliozuia bunge live wanajulikana na hata wanaosababisha kurudia chaguzi wanajulikana huu ni upuuzi wa hali ya juu
 
Hoja ya bashe yaweza kua ina mashiko tatizo likaja kwa wazee wa kutumia wingi bungeni wakahujumu
 
Hapana Lema naye ana matatizo makubwa ya kiungozi.
Ni mwanaharakati asie na suluhisho.

Ni mpingaji wa kila kitu bila kuleta solution ya mjadala.
Mara nyingi ni mbishi na hupenda kuponda wenzake kuwaita wanafiki.
Wakati yeye anashindwa hata kuleta hoja mbadala bungeni.

Amekuwa mbunge Arusha muda mrefu sio kwa sababu ni hodari sana bali kutokana na jimbo lake kuwa la upinzani.

Bashe kuleta hoja bungeni ya kudai uchunguzi sio unafiki. Yeye mwenyewe amewahi kutekwa na kuwekwa rumande wakati wa mkutano wa ccm wa kubadilisha katiba.
Naye kama kada anajua yupo katika hali gani kipindi hichi.
Hivyo lema inatakiwa aelewe hayo

Inatakiwa atoe ushauri wa namna wa kuiboresha hoja yake. Anatakiwa aunge mkono.
Mwambieni ajurekebishe na ubunge wake umekua wa kutoa hadithi za biblia tu...ajue yeye mbunge wa Wa Arusha wa dini zote.

Akiwa ana hamu kueneza biblia afungue kanisa awe mchungaji.
 
Lema, napatwa wasiwasi kwa nini anakwepa na anaipinga hoja ya Bashe kwa nguvu zote. Nini anakiogopa? Au anaogopa ukweli utawekwa bayana na baadhi ya watu wataumbuka? Au naye Lema ni facilitator wa haya matukio?
Usiwe na wasiwasi na Huyo KIDAMPA Wa KISONGO!
 
Lema, napatwa wasiwasi kwa nini anakwepa na anaipinga hoja ya Bashe kwa nguvu zote. Nini anakiogopa? Au anaogopa ukweli utawekwa bayana na baadhi ya watu wataumbuka? Au naye Lema ni facilitator wa haya matukio?
Wewe na chakubnga na bashe wote nihanga wa kupigishwa pushapu.
Bunge lipi limechunguza lipi likawa jema kwa hawa nguruwe wenu?
 
Pambaneni mpate wabumge wengi bungeni, sio kupiga kelele wakati nyie ndio minority, ndio demokrasia hiyo. Yaani Lema anataka wabimge wa aiaiemu wawe kama wabunge wa chadema?? THAT WILL NEVER HAPPEN. Wengi ndio wanafanya maamuzi. Pia ni wapi INALAZIMIKA kwa mbunge wa sisiemu kwenda kumjulia hali Lissu huko huko?? Lema acha kulia lia, siasa mmezishindwa.

Acha kuwaonea Lema Mkuu, be fair. Kumbuka wingi wa wabunge wa CCM sio matokeo ya kupambana katika fair competition. Kwanza ni matokeo ya kihistoria, kwamba huko nyuma CCM ndio kilikuwa chama cha kushika hatamu na kilikuwa chini ya kiongozi mpendwa wa watu Nyerere, pili ni kwa ajili ya u- semi-illiterate wa wapiga kura Watanzania, na tatu ni utumiaji mbaya wa madaraka wa CCM kama chama tawala katika process ya uchaguzi Tanzania.

Lakini kwa mtu yeyote mwenye akili, kutia ndani sisi tusio na mfungamano wowote wa kisiasa, anajua kwamba kuwa na demokrasia iliyo fair ya vyama vya upinzani nchini kuna manufaa kwa maendeleo ya Taifa katika kuweka checks and balances za uongozi. Na as long as CCM wataendelea kutoona faida hii kwa kuwa hawana uwezo wa kuona mbali, basi ni kweli unavyosema, kuwa na checks na balances za uongozi zitakazosaidia Tanzania kuendelea, THAT WILL NEVER HAPPEN. Sasa nani anapata hasara?

Kumbuka kwamba wengi tunakiri Magufuli ana nia njema kabisa na taifa hili, lakini hata hivyo ni lazima kuwe na namna ya kumdhibiti katika mambo fulani fulani kwa niaba ya Watanzania wote. Watu wamemuita Magufuli dictator, lakini sidhani kama ni extreme dictator. Ni kweli sometimes anakuwa pretty arrogant katika kuongoza, lakini hayuko katika extremes za u- dictator. Sasa jiulize, ikitokea Tanzania tunakuwa na extreme dictator, tuna mfumo wa kiuongozi ambao unaweza kumdhibiti (check and balance)?

Mfumo uliopo ni kwa ajili ya kuwanufaisha CCM, na lazima ukiri for as long as CCM mnatoa kiongozi mzalendo wa kweli, haitakuwa tatizo kubwa sana kuwa na mfumo usio haki unaokandamiza upinzani. Lakini siku ikitokea tukawa na extreme dictator ambaye hasikii la mtu iwe wa CCM au wa upinzani, mtajuta kuukandamiza upinzani nchini, kuudhoofisha na kuufanya usiimarike. Wapo kina Bashe ambao wanaona reality lakini ni wachache sana kuleta mabadiliko yanayotakiwa katika kufikiri kwa CCM. Huu u-semi-dictator wa Magufuli unapaswa uwe wake up call kwenu nyie CCM, maana hata tulio nje ya chama chenu tunaona unaathiri mambo na maamuzi fulani fulani ndani ya chama chenu. Na sijui awamu ya pili itakuwaje, maana wengi tunajua kwa sasa anakwenda kwa breki kidogo kwa kuwa bado kuna uchaguzi kwa ajili yake ya pili. Angalia msije mkalia awamu yake ya pili wakati ataonyesha his true colours. Msiwabeze watu wa upinzani wakati hamjui what tomorrow will bring.
 
Bashe hatakiwi kuaminiwa hata kidogo,

Kumuamini mtu yeyote anayetoka chama tawala ni sawa na kusubiri meli uwanja wa ndege,

Hawa watu wameonyesha udhaifu mkubwa sana wa kuisimamia serikali,

Kiuhalisia wanatakiwa wakutane na adhabu kali sana

Lowasa na sumaye mliwaamini,walitokea chama gani:D
 
Wananchi wanahitaji afya bora kule Nzega!!
Je Bashe ana takwimu za watu waliowahi kupotea au kuuawa jimboni Nzega?
kwa kuwa taarifa hazionyeshi mtu wa nzega kutekwa, maoni yako ni kwamba bashe anyamaze tu.
 
Back
Top Bottom