Kusudio la Kuwashitaki DHL TANZANIA kwa ucheleweshaji wa kutoa mizigo uliokubuhu

Majaribu2013

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
952
1,043
Wadau,

Nahitaji mawazo na ushauri wa kisheria nataka niwashitaki DHL TANZANIA kwa kuchelewesha kutoa mizigo yangu ambayo ilifika Dar es slaam tangu tarehe 8 April, 2020 lakini hadi leo tunaongea hakuna mzigo uliotoka.

Kwanza kabisa hawakunijulisha taarifa za mzigo kuwa umefika mpaka siku saba zikawa zimeisha. Hadi nilipofanya jitihada za kuwatafuta ndipo walipoanza kushughulikia lakini kama wanalazimishwa.

Nimeshalipa kila kitu na nimewasiliana nao hadi nimechoka hakuna kipya kinachotekelezwa.

Je, naweza kuwashitaki kwa kunisababishia hasara za ucheleweshaji wa utoaji mzigo na kuniongezea gharama zaidi ambazo sikupaswa kuzilipa?
 
Duh. Mimi nina positive experience tu na DHL kwa mizigo minne niliyoagiza from US.

Wale jamaa wana tracking. Ilikuaje? Mzigo wako umeclear customs?
 
Duh. Mimi nina positive experience tu na DHL kwa mizigo minne niliyoagiza from US.

Wale jamaa wana tracking. Ilikuaje? Mzigo wako umeclear customs?
Mzigo haukuwa wa kulipia. Maana upikuwa wa kwenda kutengenezwa na kurudi. So kila kitu kilikuwa kwao. Wanahuduma mbovu sana hawa jamaa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom