Toka awamu ya tatu ya Rais mstaafu, Mh. Benjamin William mkapa, serikali ya JMT imekuwa ikitoa ahadi ya upanuzi wa uwanja wa ndege Mwanza. Uwanja huu umekuwa na hali mbaya, unaweza ufananisha na shule ya kata, serikali ya awamu ya 4 chini ya Mh. Jakaya kikwete ulitoa ahadi ya kuendelea na upanuzi lakini kwa miaka yote kumi hali ya uwanja wa ndege imeendelea kuwa mbaya. Kwa umuhimu wa Kanda ya Ziwa kiuchumi katika taifa hili ingetakiwa uwe na uwanja wa kimataifa wenye hadhi
Kuna maneno kwa muda mrefu kwamba uwanja wa ndege mwanza haupanuliwi kwa makusudi na serikali kwa hofu ya kudhoofisha utalii kaskazini kwani Mwanza ipo karibu zaidi na Serengeti, na uwanja wa ndege wa kimataifa, tunaitaka serikali itoe ufafanuzi kwani mkoa wa Mwanza unachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa nyuma ya Dar es Salaam, kwanini unakosa uwanja wa ndege wenye hadhi ya kimataifa? Au kuna makusudi?