Kustaafu kwa hiari iwe ni muda wowote endapo mtumishi wa umma ataamua kufanya hivyo

Sijazungumzia kuacha kazi mkuu. Nimeongelea kustaafu kwa hiari. Kuwacha kazi na kustaafu ni vitu viwili tofaut. Jifunze kuelewa kabla ya kuandika chochote na kuposti

Ni vizuri ungesema hukubaliani Na Mawazo Yao Sio kusema hujaelewa

Ninachokueleza maana ya retirement maana yake Ni kuacha kisheria kufanya kazi kutokana Na sababu za Umri hiyo ndio maana ya kustaafu Sasa unaposema iwe anytime isomeke kastaafu maana yake hata kijana wa Miaka 25 asomeke kastaafu Sasa wakati gani itasomeka kaacha kazi Au unataka neno kuacha kazi liwe sawa Na neno kustaafu?
 
Unaruhusiwa kuacha kazi Muda wowote ukitaka Kwa ama kutoa notisi ya Miezi Mitatu Au kurudisha Mshahara wa Mwezi Mmoja in lieu of notice!

Kustaafu kuna Muda wake ambao Ni Miaka 55-60 Ni Kama ilivyo huruhusiwi kuajiriwa Kama Mtumishi wa kudumu ukishafikisha umri wa Miaka 45!

Ni sawa Na kuomba utambuliwe unapumzika kufanya kazi wakati hujachoka, kupumzika maana yake ni kutofanya jambo Fulani kutokana Na Kuchoka lakin ukiacha jambo kufanya kabla hujachoka hatusemi umepumzika tunasema umeacha kufanya jambo fulani

Mi nna mashaka kama umemuelewa mtoa mada,na kama umemuelewa basi jaribu kuangalia kwa umakini hoja yako kama utakuwa uko sawa!

Anazungumzia kustaafu kwa hiari iwe miaka 45 suala ambalo ni zuri!ukumbuke ukistaafu kwa hiar unapewa mafao yako ila ukiacha kaz sidhan kama utaambulia kitu!!!

Mtoa mada umetoa wazo zuri,wadogo zetu wako mitaani wanarandaranda tu,wangeweka huo muda tungewapisha nao waonje CHUNGU TAMU za utumishi Wa umma!
 
Ni vizuri ungesema hukubaliani Na Mawazo Yao Sio kusema hujaelewa

Ninachokueleza maana ya retirement maana yake Ni kuacha kisheria kufanya kazi kutokana Na sababu za Umri hiyo ndio maana ya kustaafu Sasa unaposema iwe anytime isomeke kastaafu maana yake hata kijana wa Miaka 25 asomeke kastaafu Sasa wakati gani itasomeka kaacha kazi Au unataka neno kuacha kazi liwe sawa Na neno kustaafu?
Kiongozi, hebu kwanza soma Head line ya Uzi . pia Nilichosema Wakati Muafaka SHERIA KUBADILISHWA maana yake Sheria ikibadilishwa then a civil servant atakuwa huru kustaafu time yoyote akiona inafaa siyo kusubiria miaka 55 ndivo hoja yangu ilipo . Sizungumzii Sheria iliyopo sasa naelewa kwamba hairuhusu ndio nikapendekeza ibadilishwe
 
Wanadau, muda umefika sasa Sheria kubadilishwa ili itoe Fursa kwa watumishi wa Umma kustaafu kwa hiari muda wowote endapo Mtumishi huyo ataamua kufanya hivyo kwa hiyari yake mweyewe.

Kwa maoni yangu muda wa miaka 55 uliowekwa na Sheria ya sasa wa kustaafu kwa hiari ni kipindi kirefu Sana na unanyima Watumishi wenye nia ya kustaafu mapema haki yao ya maamuzi sahihi.

Matarajio ya kuishi kwa nchi za kiafrika yameshuka sana miaka hii kwa ajili hiyo umri wa kustaafu kwa hiyari miaka 55 No mrefu mnoo Na kustaafu kwa lazima miaka 60 ni vyema kurekebishwa kwa mujibu wa Sheria.

Itasaidia sana kwa watanzania kwa kutoa fursa za wale wasioajiriwa kuajiriwa kwa kuwa wapo watumishi wa umma wengi tu wanahitaji kustaafu mapema zaidi kabla ya kufika umri huo ili kuwapisha Watanzania wengine waingie katika ajira lakini hawawezi kufanya hivyo kwa kuwa wanabanwa na hitaji la kisheria la miaka 55 kustaafu kwa hiari.

Muda muafaka sasa wakati wowote Mtumishi akiamua kustaafu kwa hiari hata akiwa na miaka 40 au 45 aruhusiwe kisheria. Na huo ndio Uhuru wa kujiamulia mambo wayatakayo katika maisha watanzania.

Ni wajibu wangu kutoa maoni na kwamba katiba ya Tanzania, 1977 inaniruhusu kufanya hivyo.
Huoni itakuwa mzigo kwa serikali kulipa pensheni wakati akiyestaafu mapema anapiga kazi nyingine
 
Kiongozi, hebu kwanza soma Head line ya Uzi . pia Nilichosema Wakati Muafaka SHERIA KUBADILISHWA maana yake Sheria ikibadilishwa then a civil servant atakuwa huru kustaafu time yoyote akiona inafaa siyo kusubiria miaka 55 ndivo hoja yangu ilipo . Sizungumzii Sheria iliyopo sasa naelewa kwamba hairuhusu ndio nikapendekeza ibadilishwe

Let say unaanza kazi Na Miaka 25 baada ya kumaliza masomo , then at 45 unastaafu maana yake umetumikia Kwa Miaka 20 tu then life expectancy yako Ni 65 years maana yake ufanye kazi Kwa 20 years Halafu pension fund ikuhudumie Kwa Miaka 20 unadhan kuna pension fund inaweza ku survive?
 
Nafikiri 50 ni reasonable kwa kuwa angalau kodi uliyoitumia kukufanya ufike hapo ulipo itakuwa imetumika vizuri.
 
Hakuna mabadiliko ya hivyo.Kuna tofauti kubwa kati ya kustaafu nakuacha kazi,wewe hoja yako imejificha kwenye fao lakujitoa ila umelileta kinyume nyume.Sasa ilo la fao lakujitoa ni hoja nyingine ambayo sheria yake inaweza kubadilishwa ila uko sio kustaafu nikuacha kazi kabla ya umri wakustaafu kisheria kufika.
 
Let say unaanza kazi Na Miaka 25 baada ya kumaliza masomo , then at 45 unastaafu maana yake umetumikia Kwa Miaka 20 tu then life expectancy yako Ni 65 years maana yake ufanye kazi Kwa 20 years Halafu pension fund ikuhudumie Kwa Miaka 20 unadhan kuna pension fund inaweza ku survive?
Na vipi wale wanaostaafu miaka 60 then life expectancy ni 61 umewazingatia pia ? Kumbe unakusudia ukilipwa penchen usiishi muda mrefu ? Mtumishi asitie hasara ya bure ? Ajifie haraka? Dah kazi kweli kweli!
 
huo ndio ukweli mchungu... dunia nzima ndio maana yake.. wazungu sio wajinga kutengeneza hii mifuko ya pensheni
 
Wanadau, muda umefika sasa Sheria kubadilishwa ili itoe Fursa kwa watumishi wa Umma kustaafu kwa hiari muda wowote endapo Mtumishi huyo ataamua kufanya hivyo kwa hiyari yake mweyewe.

Kwa maoni yangu muda wa miaka 55 uliowekwa na Sheria ya sasa wa kustaafu kwa hiari ni kipindi kirefu Sana na unanyima Watumishi wenye nia ya kustaafu mapema haki yao ya maamuzi sahihi.

Matarajio ya kuishi kwa nchi za kiafrika yameshuka sana miaka hii kwa ajili hiyo umri wa kustaafu kwa hiyari miaka 55 No mrefu mnoo Na kustaafu kwa lazima miaka 60 ni vyema kurekebishwa kwa mujibu wa Sheria.

Itasaidia sana kwa watanzania kwa kutoa fursa za wale wasioajiriwa kuajiriwa kwa kuwa wapo watumishi wa umma wengi tu wanahitaji kustaafu mapema zaidi kabla ya kufika umri huo ili kuwapisha Watanzania wengine waingie katika ajira lakini hawawezi kufanya hivyo kwa kuwa wanabanwa na hitaji la kisheria la miaka 55 kustaafu kwa hiari.

Muda muafaka sasa wakati wowote Mtumishi akiamua kustaafu kwa hiari hata akiwa na miaka 40 au 45 aruhusiwe kisheria. Na huo ndio Uhuru wa kujiamulia mambo wayatakayo katika maisha watanzania.

Ni wajibu wangu kutoa maoni na kwamba katiba ya Tanzania, 1977 inaniruhusu kufanya hivyo.
Mabadiliko ya sheria iliyopitishwa hivi karibuni ni kuwa baadhi ya watumishi wa serikali hususani madaktari bingwa na wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma umri wa kustaafu kwa hiari ni miaka 60 na ule wa lazima ni 65! Hapo una cha kusema?
 
Logic waliyotumia hawa ni wataalamu wapo wachache sana then imechukua miaka mingi sana kuwaandaa. Tanzania miaka 55 Mtu Ndo anapata UProfesa! Wakati wenzetu miaka 30 Tayari ni Profesa
 
Back
Top Bottom