Torero
Senior Member
- Dec 22, 2017
- 122
- 138
Wanadau, muda umefika sasa Sheria kubadilishwa ili itoe Fursa kwa watumishi wa Umma kustaafu kwa hiari muda wowote endapo Mtumishi huyo ataamua kufanya hivyo kwa hiyari yake mweyewe.
Kwa maoni yangu muda wa miaka 55 uliowekwa na Sheria ya sasa wa kustaafu kwa hiari ni kipindi kirefu Sana na unanyima Watumishi wenye nia ya kustaafu mapema haki yao ya maamuzi sahihi.
Matarajio ya kuishi kwa nchi za kiafrika yameshuka sana miaka hii kwa ajili hiyo umri wa kustaafu kwa hiyari miaka 55 No mrefu mnoo Na kustaafu kwa lazima miaka 60 ni vyema kurekebishwa kwa mujibu wa Sheria.
Itasaidia sana kwa watanzania kwa kutoa fursa za wale wasioajiriwa kuajiriwa kwa kuwa wapo watumishi wa umma wengi tu wanahitaji kustaafu mapema zaidi kabla ya kufika umri huo ili kuwapisha Watanzania wengine waingie katika ajira lakini hawawezi kufanya hivyo kwa kuwa wanabanwa na hitaji la kisheria la miaka 55 kustaafu kwa hiari.
Muda muafaka sasa wakati wowote Mtumishi akiamua kustaafu kwa hiari hata akiwa na miaka 40 au 45 aruhusiwe kisheria. Na huo ndio Uhuru wa kujiamulia mambo wayatakayo katika maisha watanzania.
Ni wajibu wangu kutoa maoni na kwamba katiba ya Tanzania, 1977 inaniruhusu kufanya hivyo.