Kusomesha watoto sana, ni njia ya kujiongezea upweke huko uzeeni

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,189
39,954
Wazazi wengi, wanajitahidi sana kusomesha watoto wao ili huko mbeleni wawe na maisha mazuri au wasiwe tegemezi.

Watoto wakishahitimu, uanzisha maisha yao, kwa kujitegemea pamoja na kuwa mbali na wazazi wao; wakuoa wataoa, na wakuolewa wataolewa.

Changamoto inayojitokeza, ni wazazi kubaki wenyewe, na kukosa watu wa kuwafariji pale wanapohitaji faraja. Wengi hubaki na vijana wakazi, ambao kwa namna moja au nyingine hawawezi kuumaliza msongo wa mawazo wa wahusika.

Uzee ni umri unaohitaji kuwa karibu sana na uzao wako, kwa kufurahi pamoja na kupeana faraja; ingawa wazee wengi hawapati hiyo fursa kutokana na uzao wao kuwa mbali nao, hii inawapelekea kujutia uzao wao.

Wenzetu wa Asia wamejaribu kudhibiti hii hali, kwa kuishi na uzao wao kwenye boma moja, lengo kuu ni kudhibiti hali ya upweke huko uzeeni.​

Karibuni wakuu, kwa maoni.
 
Kuhitaji mtoto akufariji ni kukosa kujipanga vizuri katika maisha.

Umeshindwa kujiwekea akiba ya uzeeni? umeshindwa kujipanga kupata mwenza wa kuwa naye uzeeni?

Unazaa mtoto, unamsomesha, anakua mkubwa, na yeye inakuwa zamu yake ya kuzaa na kusomesha akipenda. Mwache naye aishi maisha yake, akiamua kusaidia wazazi sawa, akiamua kuwa busy na maisha yake sawa.

Wewe baba au mama unayehitaji sana mtoto wako aache ku focus kwenye familia anayoianzisha, halafu a focus sana kwako wewe mzazi, ni mbinafsi na umeshindwa kujipanga na maisha yako mwenyewe ya uzeeni.

Nimeona hii tabia ya wazazi kuwatumia watoto wao kama mbadala wa mfumo wa mafao ya uzeeni, au wazazi kudai matunzo uzeeni kwa sababi waliwalea watoto wakiwa wadogo. Huu ni ubinafsi wa hali ya juu.
 
Ni kweli,hiyo situation imetokea kwa bi mkubwa wangu mara baada ya sisi watoto wake kuwa na maisha yetu na kuishi mbali na nyumbani na mzee kufariki. Tunajitahidi kumtafutia watu wa kukaa naye ambao ni wafanyakazi na watoto wa ndugu ila changamoto zimekuwa Ni nyingi hivyo hujikuta anabaki mwenyewe.Hii imenifanya nifikiri sana maisha yangu yatakavyokuwa baada ya watoto wangu wote kuondoka nyumbani na kwenda kujitegemea.
Ili kukabiliana na hii hali nimeamua kuanzisha vitega uchumi ndani ya eneo langu la makazi maana ninaishi kwenye mojawapo ya majiji hapa nchini.Kati ya hivyo vitega uchumi nitafungua ofisi ambayo itanifanya nikutane na watu Mara kwa mara na hizo ofisi nyingine nitazipangisha hivyo muda mwingi nitakuwa na communicate na watu.Ikifika muda nikawa mzee sana kiasi Cha kushindwa kutoka hata nje ya nyumba basi watoto wangu itabidi wabebe jukumu la kujua nitaishije maana nitakuwa nimepoteza nguvu na uwezo wa kufikiri.
 
Wazazi wengi, wanajitahidi sana kusomesha watoto wao ili huko mbeleni wawe na maisha mazuri au wasiwe tegemezi.

Watoto wakishahitimu, uanzisha maisha yao, kwa kujitegemea pamoja na kuwa mbali na wazazi wao; wakuoa wataoa, na wakuolewa wataolewa.

Changamoto inayojitokeza, ni wazazi kubaki wenyewe, na kukosa watu wa kuwafariji pale wanapohitaji faraja. Wengi hubaki na vijana wakazi, ambao kwa namna moja au nyingine hawawezi kuumaliza msongo wa mawazo wa wahusika.

Uzee ni umri unaohitaji kuwa karibu sana na uzao wako, kwa kufurahi pamoja na kupeana faraja; ingawa wazee wengi hawapati hiyo fursa kutokana na uzao wao kuwa mbali nao, hii inawapelekea kujutia uzao wao.

Wenzetu wa Asia wamejaribu kudhibiti hii hali, kwa kuishi na uzao wao kwenye boma moja, lengo kuu ni kudhibiti hali ya upweke huko uzeeni.​

Karibuni wakuu, kwa maoni.
Kwani watoto wa nje umezuiwa kuwa nao?
 
Tatizo la kusikitisha zaidi kadri mtt anavyoelimika zaidi ndio ndio hali ya kutomjari mzazi wake inavyoongezeka tena km ubahatike asifike huko ulaya ndo basi tena ht akirudi anawqzaga kmy kimya km bora akupeleke kwenye makambi ya wazee usimsumbue
 
Wazazi wengi, wanajitahidi sana kusomesha watoto wao ili huko mbeleni wawe na maisha mazuri au wasiwe tegemezi.

Watoto wakishahitimu, uanzisha maisha yao, kwa kujitegemea pamoja na kuwa mbali na wazazi wao; wakuoa wataoa, na wakuolewa wataolewa.

Changamoto inayojitokeza, ni wazazi kubaki wenyewe, na kukosa watu wa kuwafariji pale wanapohitaji faraja. Wengi hubaki na vijana wakazi, ambao kwa namna moja au nyingine hawawezi kuumaliza msongo wa mawazo wa wahusika.

Uzee ni umri unaohitaji kuwa karibu sana na uzao wako, kwa kufurahi pamoja na kupeana faraja; ingawa wazee wengi hawapati hiyo fursa kutokana na uzao wao kuwa mbali nao, hii inawapelekea kujutia uzao wao.

Wenzetu wa Asia wamejaribu kudhibiti hii hali, kwa kuishi na uzao wao kwenye boma moja, lengo kuu ni kudhibiti hali ya upweke huko uzeeni.​

Karibuni wakuu, kwa maoni.
Ni kweli tupu mimi nilifikiri hali ya upweke kwa wazazi ni tatizo la Ulaya na lingechukua muda mrefu sana kufika Africa lakini tayari lipo sana tena linakuwa hatari kuliko hata Ulaya kwani umaskini hulifanya tatizo hilo kuwa kubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom