Kusomesha shule za ada kubwa na kawaida nini faida

Maisha hayana kubembeleza, Maisha ni mchaka mchaka, maisha ni mapambano. Endeleeni kuwaonyesha watoto na wajukuu zenu ufahari na kiburi cha fedha mlizonazo lakini mwisho wake upo karibu zaidi.Mtoto hajui kugombea chakula, hajui kugombea daladala, hajui kuzipga kavu kavu bila refa, mtoto hajui kumkoromea mwenzake, mtoto njaa kwake ni msamiati.Mtoto hajui kuuza kokoto wala kuuza karanga. Chanzo cha ubunifu wowote duniani ni changamoto ambazo mtu anapitia, hakuna ubunifu ukiwa umekulia katika meza ya mfalme. Imekuwa inatisha namna ambavyo wazazi wamekuwa wakitumia kiasi kikubwa cha fedha kulipa ada za shule wengine wakiwa hali zao ni duni lakini wakifuata mkumbo.
aisee kama hiyo nadharia yako ni ya kweli basi wazungu tungekuwa tushawapita ubunifu, maana maisha soft wao wameanza kuish karne ya 19,lakini ndio wanaaongoza kwa ubunifu
hata kibongo bongo tu watu kama akina Mo Dewji ambao wameishi maisha yasiyo ya tabu ndio anazidi kupeleka utajiri wa familia next level, yupo agressive kulio watoto waliokulia kwenye umasikini
 
Kwa taarifa yako mtoto wa Mhe job ndugai 'spika wa bunge ' alisomea tabora boys, baba yake aliona amuache hapo hapo tabora boys kuliko kumpeleka 'feza boys ', sasa unakuta mtu anasoma shule ya milioni 5 Halafu anatoka na division three, kuna shule Mwanao akichaguliwa especially kwa 'advanced level ' muache aende wala usimpeleke huko kwenye Ada za milioni 5, kwa mfano kuna dogo mmoja hivi wakishua sana alifaulu 'kibaha boys ' baba yake akataka kumpeleka 'shule za milioni 5' dogo akagoma kamaliza vizuri tu form 6 na division one nzuri tu tena kwa gharama ya '140,000/-' Wakati kuna wengine wametoka na division three kwa milioni 10
====
Kwa taarifa yako, wale wabunge wote mjengoni watoto wao hawasomi shule za public.... Kama wapo ni wachache ambao wameenda shule zinazoitwa maalum. Waziri wa elimu na wakurugenzi wa elimu pale wizarani hawasomeshi watoto wao shule za public...

Kwa maana wanachakachua mchuzi mle nyie, wao wanakula madikodiko kwa jirani. akili za kuambiwa, changanya na zako....
 
Ili mtoto wa nursery aonekane anasoma shuke ya gharama ada inatakiwa sh ngapi? Goes to primary student, nazitafuta kumsomesha shuke ya gharama sasa hivi tunalipa ada 1.3m tunaenda shule saa 3 au saa 2 asubuhi au saa 1(anyway mda atakaoamka huwa simuamshi) tunarudi saa 11 ana miaka 3.
 
====
Kwa taarifa yako, wale wabunge wote mjengoni watoto wao hawasomi shule za public.... Kama wapo ni wachache ambao wameenda shule zinazoitwa maalum. Waziri wa elimu na wakurugenzi wa elimu pale wizarani hawasomeshi watoto wao shule za public...

Kwa maana wanachakachua mchuzi mle nyie, wao wanakula madikodiko kwa jirani. akili za kuambiwa, changanya na zako....
Hahahaahaaaaaaaaa
 
Ni utafauti wa kipato...

Ni sawa na kusafiri first class na mwingine akasafiri business au economic class wote mtafika sababu mpo kwenye same flight..


Cc: mahondaw
 
Ume
MKUU TUNATOFAUTIANA KIPATO.
Mtu mwenye uwezo wa kumsomesha mtoto shule nzuri hawezi kamwe kumpeleka kayumbaz.Ukiona watoto wako wako kayumbas kuwa mpole mkuu najua hupendi ila imekubidi
Umeuwaa....jibu kuntu 👌
 
Mazingira hayapo sawa na hayatakuja kuwa sawa

Mazingira hayako sawa
International schools Zina wanafunzi toka mataifa mbalimbali .Mtoto anakuwa exposed kwenye international environment .Pia anajifunza mambo mengi ya kimataifa michezo yao unakuta cricket,swimming,golf,table tennis,michezo ya baharini nk Huwezi mlinganisha na anayesoma magomeni na Watoto wenzie wa magomeni shule haina hata kiwanja Cha michezo



Mimi nipo mtaani na jamaa wengine hawaijui hata JF wote tunapiga Story za makuzi mademumademu ila niingia JF exposure nayoipata ni tofauti japo tupo mtaa mmoja...The same To your question.
Nimewapata! Hata mimi ninachoamini kwamba ktk shule zetu tulizonazo TZ zimegawanyika.
1. Zipo zinazoandaa wapigiwa kura.
2. Zipo zinazoandaa wapiga kura.
Au
1. Zipo zinazoandaa watawala.
2. Zipo zinazoandaa watawaliwa.
 
Mm nadhani mnatumia nguvu nyingi kubishana kitu ambacho unaweza kufanya tafiti ndogo kwa wkt huu tulionao kupitia makampuni na mashirika makubwa...Jiulize CEO wa Aitel kwa mfano back ground ya elimu yake ikoje? Vodacom,Tigo ,CRDB,Azania Bank na makampuni na mashirika mengine makubwa...Wale top layer/Cream ya watendaji wakuu elimu zao na back ground zao zikoje? Hapa utapata jibu ambalo litahitimisha mjadala huu.

Sihitaji vyeo vya serikalini kwakua huko hakuhitaji good result per personal life time.Kwahiyo huwezi kupima result ya mtu alopewa mamlaka/madaraka/cheo kirahisi.
Hivi Said S. Bakhresa alisomaga wapi?,,,vp nae yupo layer ipi?
 
Sema tu wewe hujaamini ila unamzidi mambo mengi sana..... but only you are obsessed with his money
Hivi mtu akikuzidi kipato utafurukuta kwa lipi kudhihirisha wewe upo vzr kushinda yeye?
Mkuu asikwambie mtu uongo ila kutengeneza pesa mtaani inahitaji umahili wa hali ya juu sana.
 
Napenda kujua hv mtoto kusoma shule hz za kulipia ada kubwa kuanzia 5m n.k na hizi za ada laki 5 harafu wote mnakutana mlimani au st joseph nini faida zake....
Faida yake ndio hii ukiwa presidaa wewe ni hasira na visasi tu. Kama Jiwe angesoma shule za Ada kubwa ungeona kazi na Bata maana yake.

Kama hujaelewa mwangalie Kenyata na Jiwe uone tofauti ya mbingu na Ardhi. Hata Nyerere hawakwambii tu kama alikuwa mtoto wa chief.
 
Matoto yalosoma shule nzuri za gharama huwa yana confidence sana tofauti na sisi Kayumba.
 
Back
Top Bottom