Kusomea Sheria ni kusomea utamaduni wa Uingereza, hakuna kingine!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Na huo ndiyo ukweli wenyewe ingawaje wengi wao wanaojiita Wanasheria labda hawalielewi hili, hakuna kitu kingine unachojifunza zaidi ya maisha ya Muingereza!

Na ndiyo maana nchi zote zinazojitambua Duniani zina Sheria zao, kuna Sheria za Uchina, Ujapani, Ufaransa, Ujerumani, Urusi, hata vinchi vidogo kama Lithuania au Qatar vina Sheria zao, nchi za Kiarabu wana zao pia za Kiislamu lkn Mwafrika hatuna Sheria zetu!

Kwa wasiofahamu British common law ambayo ndiyo Sheria zetu imetokana na maisha ya kila siku ya Watu wa Uingereza ndiyo kutokana na maisha yao wakaamua kutengeneza utaratibu wa kuwaongoza, cha ajabu utaratibu huo ndiyo tunaojivunia nao lkn tofauti ni kwamba sisi kama Watanzania hatujapitia hayo maisha ya Waingereza hivyo kwa hali ya kawaida British common law haikupaswa kuwa Sheria yetu Tanzania, na ndiyo maana Wanasheria wote Tanzania ni Waingereza kuliko Watanzania kwani hakuna kingine wanachosomea zaidi ya Utamaduni wa Muingereza ...
 
Tangu uluvyosema Raisi Jammeh Hawezi kupindukiwa na majeshi ya muungano wa ECOWAS nakuona mpuuzi tu usiejielewa
Heshima Mkuu.

Kwanini usingeijibu hoja yake kwa kuzingatia mantiki na badala yake unamtusi mleta mada?.Matusi kama "Mpuuzi tu usiejielewa" ya kazi gani?.

Uluvyosema=Ulivyosema.
Raisi=***
Kupindukiwa=Kupinduliwa.

Tujirekebishe wakuu.Tunaishusha hadhi Jamiiforums.
 
Na huo ndiyo ukweli wenyewe ingawaje wengi wao wanaojiita Wanasheria labda hawalielewi hili, hakuna kitu kingine unachojifunza zaidi ya maisha ya Muingereza!

Na ndiyo maana nchi zote zinazojitambua Duniani zina Sheria zao, kuna Sheria za Uchina, Ujapani, Ufaransa, Ujerumani, Urusi, hata vinchi vidogo kama Lithuania au Qatar vina Sheria zao, nchi za Kiarabu wana zao pia za Kiislamu lkn Mwafrika hatuna Sheria zetu!

Kwa wasiofahamu British common law ambayo ndiyo Sheria zetu imetokana na maisha ya kila siku ya Watu wa Uingereza ndiyo kutokana na maisha yao wakaamua kutengeneza utaratibu wa kuwaongoza, cha ajabu utaratibu huo ndiyo tunaojivunia nao lkn tofauti ni kwamba sisi kama Watanzania hatujapitia hayo maisha ya Waingereza hivyo kwa hali ya kawaida British common law haikupaswa kuwa Sheria yetu Tanzania, na ndiyo maana Wanasheria wote Tanzania ni Waingereza kuliko Watanzania kwani hakuna kingine wanachosomea zaidi ya Utamaduni wa Muingereza ...
Mbali na hicho ulichokisema, yapaswa utambue kuwa, mila zetu ni sehemu ya sheria ama chanzo sheria kama zilivyo sheria nyingine zenye hadhi ktk mfumo wa sheria na utoaji haki. Soma kesi ya Mahagwi Gimito V. Gibeno Werema. Ambapo mahakama ilisema sheria za kimila zina hadhi sawa kama zilivyosheria nyingine za nchi. Ukisoma Customary law declaration of 1920 utaelewa juu hadhi ya sheria za kimila ktk mfumo wetu wa sheria na utoaji haki. Sheria ya kimila hutumika ktk masuala kama vile ndoa , mirathi na mengineyo. Sheria zote hizo katika hadhi yake na matumizi zipo chini ya sheria mama ambayo ni katiba.

Soma vizuri sheria kisha utakuja na mapendekezo sahihi ya hicho ulichokisema ambacho binafsi nachukulia ni maoni yako na hakina usahihi katika jicho la kisheria kwa kuzingatia hoja zangu na nyingine nyingi za kisheria.
 
Je kusoma sayansi mfn (Phys.., Chem.. & Bio..)
Je kutumia madawa na vifaa tiba, ect
Je kutumia devices km simu, komputa, runinga ect
Je kutumia vyombo vya mto (gari, pikpk, ndege) etc

Je kula kwa vijiko, uma, stick, etc
Je kujipata mafuta (ya viwandan) baada ya kuoga etc
Je kuvaa nguo za cotton, sufi, etc

Na mengine kedekede je huo co utamaduni wa mwingereza???

Cuture is dynamic not static!.
 
Hayo yote ulioyaorodhesha siyo Utamaduni wa Uingereza, bali yanatokana na tamaduni mbali mbali Dinia nzima, ila Sheria yetu ni Utamaduni wa Uingereza!
 
Mbali na hicho ulichokisema, yapaswa utambue kuwa, mila zetu ni sehemu ya sheria ama chanzo sheria kama zilivyo sheria nyingine zenye hadhi ktk mfumo wa sheria na utoaji haki. Soma kesi ya Mahagwi Gimito V. Gibeno Werema. Ambapo mahakama ilisema sheria za kimila zina hadhi sawa kama zilivyosheria nyingine za nchi. Ukisoma Customary law declaration of 1920 utaelewa juu hadhi ya sheria za kimila ktk mfumo wetu wa sheria na utoaji haki. Sheria ya kimila hutumika ktk masuala kama vile ndoa , mirathi na mengineyo. Sheria zote hizo katika hadhi yake na matumizi zipo chini ya sheria mama ambayo ni katiba.

Soma vizuri sheria kisha utakuja na mapendekezo sahihi ya hicho ulichokisema ambacho binafsi nachukulia ni maoni yako na hakina usahihi katika jicho la kisheria kwa kuzingatia hoja zangu na nyingine nyingi za kisheria.

Hahah na huo ndiyo ujinga wenyewe, kwa hiyo Utamaduni wetu unaingizwa kwenye mambo ya ndoa na mirathi tu? Ngoja nikuulize, Je kuna Mwanasheria Tanzania aliyesomea hiyo unayoiita customary law? Yaani mtaalamu wa Sheria za Kimila?
 
Labda nikwambie hivi, vyanzo vya sheria ama sources of law in Tanzania ni common law (received laws), Customary laws, Constitution and Statututes( sheria zilizotungwa na bunge).

Hakuna mwanasheria ambaye hafahamu hadhi ya customary law au hajasoma lolote kuhusu sheria za kimila, yapo maamuzi mengi ama mazingira mengi ya kisheria yahitaji matumizi ya sheria za kimila na yapo maamuzi yameamuliwa kwa sheria za kimila mfano ni kesi tajwa hapo (landmark case) ambapo ilitoa msingi wa hadhi na matumizi ya sheria ya kimila.

Soma sheria nilizokuambia hapo, utaelewa vzr, Soma undani wa legal system za ulimwenguni ikiwemo 'Inqusitorial na adversarial'.

Suala lako limezungumziwa kwa kina na mapendekezo mengi ukisoma machipisho yaani Dissertation za PhD, LLM na hata Llb. Soma ama uliza ufundishwe kwa nini tumetumia common law na si mifumo ya sheria za kimila perse? utapata jibu ila ukiendelea kushikilia msimamo bila kutafiti sababu za kisheria hautaelewa na hoja yako utaifanya au kuiona ni hitimisho.
 
Lkn hata hiyo inayoitwa customary law bado siyo ya kwetu kwa maana kama umesema ilianza mwaka 1920 ina maana ni Mzungu ndiye aliyeiweka na ndiye aliyechagua kipi tujifunze na kipi tusijifunze, hivyo kwangu mimi bado ni British common law tu, kwani imeanzishwa na Mzungu, na hivyo basi hata lengo la kuanzishwa kwake analijua Mzungu kama yalivyo mambo mengi kwenye jamii yetu ambayo tumeyarithi tu, na ndiyo yanayotusumbua mpaka leo hii, tunashindwa kwenda mbele, kwani tuna mfumo wa Kizungu lkn sisi siyo Wazungu na wala hatuishi Kizungu!
 
We Barbarosa acha uchuro kama huwezi kujenga hoja za msingi.
Mosi wanasheria hawajiiti wanasheria ila ni wanasheria kweli.
Mbili, sheria siyo za Uingereza tu ambazo waafrika wanasomea.
Hii inayoita sheria ya Uingereza ni mfumo unaoitwa Common Law Legal system ambayo inatumiwa na nchi zote zilizotawaliwa na Mwingeza, siyo nchi za Africa tu bali hata za mabara mengine.
Pia kuna mfumo mwingine unaoitwa Civil Law legal system ambao ni mfumo wa sheria wa nchi has za continental Europe na hata baadhi ya nchi za Asia na Latin Amerika. Na nchi nyingi za Kiarabu wanao mfumo wao wa sheria. Je wewe ulitaka tuwe na mfumo upi?
 
Back
Top Bottom