Kusoma alama za nyakati ni muhimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kusoma alama za nyakati ni muhimu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kisendi, Feb 3, 2011.

 1. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  An Extract from Tanzania Daima of Today!

  Katika hatua inayoashiria kuzidi kuungwa mkono kwa CHADEMA na viongozi wake, jana Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alikuwa kivutio katika sherehe ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambayo rais Jakaya Kikwete alikuwa mgeni rasmi.

  Mbowe alikuwa kivutio wakati akiinuka kwenye kiti alichokaa kuelekea kwenye ngazi za Mahakama Kuu kupiga picha na viongozi mbalimbali wa serikali na mahakama ambao ni watumishi wa mahakama, mawakili na wananchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hiyo.

  Watumishi wa mahakama pamoja na wananchi hao walisikika wakimshangilia kwa sauti ya juu “Mbowe Mbowe, Mbowe” na kiongozi huyo kulazimika kuwapungia mkono na kutabasamu.

  Akitoa hotuba yake katika sherehe hizo, Rais Kikwete aliutaka mhimili wa mahakama kushirikiana na vyombo vya habari kutoa elimu kwa umma kuhusu utendaji kazi na muundo wa mahakama ukoje kwani kwa kufanya hivyo kutamuondolea adha anayoipata hivi sasa ya wananchi kufika Ikulu na kumtaka atengue hukumu mbalimbali wakilalamika kutotendewa haki.

  “Wananchi wamekuwa wakijazana pale ofisini wakitaka nitengue hukumu zilizokwishatolewa na mahakama na mimi nimekuwa nikiwaambia sina mamlaka ya kufanya hivyo… wananchi hao wamekuwa wakinijibu kama siwezi kufanya hivyo watamchagua rais anayeweza kufanya hivyo na kwamba ndiyo maana wanataka katiba mpya…lakini yote hii inasababishwa na umma kuwa na uelewa finyu wa sheria na muundo wa mahakama,” alisema Kikwete na kusababisha watu kuangua vicheko. [Hivi Rais anamwogopa nani kama MD wa Dowans?, na huyu Rostam urafiki umegeuka na kumfanya Rais wa nchi mtumwa, ni nani hasa na ana kitu gani sooo special kwa jamaa yetu?????]

  Wakati huo huo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga juzi alilazimika kutumia salamu za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kuwashawishi wanafunzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya (MIST) waweze kumsikiliza.

  Kitwanga alilazimika kukikubali japo kwa muda Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kutokana na hatua ya wanafunzi wa chuo hicho kuguna kila alipoitaja ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi wakati akizungumza nao kuhusu inavyotekeleza sera ya elimu.

  Waziri huyo alilazimika kuwasalimia wanafunzi hao akisema “CHADEMA hoyee!!, na ukumbi mzima ulizizima kwa mayowe na vifijo vya wanafunzi waliopaza sauti zao wakimjibu “Oyeeee” huku kila mmoja akimpungia alama ya vema kwa kuonyesha vidole viwili. { Ni suala la muda tu wenyewe watakiri kuwa sisiemu yao si ya wananchi na watasema kile wananchi wanachotaka bila kupenda!}!

  Kitendo cha Waziri Kitwanga kutumia jina la CHADEMA katika kibwagizo hicho kilitokana na hatua ya wanafunzi hao kuguna pale alipoanza kujibu maswali yao kwa kusema “katika Ilani ya ya CCM…..” bila kumalizia kusema alishtushwa na miguno.
   
 2. K

  Kisendi JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 700
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Unajua Serikali imeshindwa hata kuzibiti bei za bidhaaa jamani ingawa sitaki maandamano wala kuchochea vurugu si nzuri maana hatutaweza hata kuja kazini na WATZ wengi tumezoea shida na kununua vya bei ya juu ili hali mifukoni mwetu si pazuri sana, Gesi ilipopanda Tsh 70000 kuna dada mmoja akasema hata ikifika laki mimi nanunua tu. lakini hii ni kutokuwa na akili maana sisi tunapenda sifa ndio maana viongozi wanaanzisha business zao harafu wanatutumia sisi kuchuma
   
 3. M

  MushyNoel Senior Member

  #3
  Feb 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bado hujawa mwanamageuzi.Kwa wakati kama huu ambapo mambo ni magumu basi haki na idaiwe sasa.isiombwe tena kwani haitapatikana.
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Feb 3, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,132
  Trophy Points: 280
  Kweli wana wakati mgumu!
   
 5. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  aksante kwa extract njema sana! nimejisikia kutokwa na machozi ya furaha! bado kidogo tu..tutafika!
   
Loading...