Kusokotwa na tumbo

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,608
2,000
Tumbo huuma wanawake wanapoenda mwezini, virusi na mchanganyiko wa vyakula ambavyo hugeuka na kuwa sumu.Unaweza kuzuia kuumwa na tumbo na kuhara kwa kutotumia vyakula vinavyotoa harufu mbaya ya kuchacha.
Ukiumwa na tumbo unaweza kujitibu:
Damu ya hedhi

 • Ukiwa mwezini meza tembe kama Panadol au utakayoambiwa na daktari ili kupoteza maumivu.
 • Tumia sodo kwa utulivu wako.
Virusi vya tumboni

 • Unapotapika, kuwa na homa, kichwa kuuma, misuli kuuma, na viungo vya mwili.Hizi dalili hudumu kwa muda wa masaa 24.
 • Ikiwa unaendesha usimeze dawa ya kujaribu kuzuia kwa muda wa masaa 2-3.
 • Pumzika zaidi.
 • Kula vyakula vyepesi, ndizi, wali, na vinywaji vya matunda.
 • Usile vyakula vilivyo na mafuta mengi, vinzari au bidhaa zozote kutokana na maziwa, pombe, kahawa n.k.
Mchanganyiko wa vyakula vibaya.
Unaweza kutapika, kuhara, kuwa na homa au kupungukiwa na maji mwilini.

 • Ukiwa unaendesha unapoumwa na tumbo, usimeze dawa masaa 2-3, inawekana kuwa uchafu uliokuwa tumboni unatoka.
 • Baada ya masaa kadhaa unaweza kumeza madawa ya kuzuia kuendesha Kama “Valoid”, utaipata katika maduka ya kuuza madawa.
 • Kunywa maji mengi sana ama vitu vioewevu kama vile chai isiyo na majani mengi, sharubet ya matofaa ama vinywaji vyovyote visivyolewesha ili urudishe mwilini maji uliyoyapoteza wakati ulipokuwa ukiendesha.Pia tangawizi husaidia kutuliza tumbo.Iwapo una wasiwasi kuwa huenda mwili ukanyauka kwa kupoteza maji,basi tumia dawa ya “Redidrat” ya kurudisha maji mwilini.
 • Iwapo utapata hamu ya chakula, kula ule mkate mwembamba au mweupe , ndizi na wali ,vitakusaidia katika kufungisha kuendesha.Usile vyakula vizito vyenye mafuta mengi , vyakula vitokanavyo na maziwa au vile ambavyo ni vya nyuzinyuzi (matunda mabichi ,mboga vyakula vya afya bora vya ngano) wakati ambapo tumbo limevurugika au unaendesha.
 • Pumzika vya kutosha.
Muite daktari wako iwapo:

 • Kwa ghafla tu unaanza kuendesha na tumbo kuvurugika ama uwe na joto la zaidi ya digirii 38oC .
 • Hali ya tumbo kuvurugika husikika upande wa chini wa kulia wa tumbo yako. (unaweza kuhitajika kuhudumiwa katika chumba cha huduma za dharura iwapo zipo katika sehemu hii.
 • Tumbo linaweza kuvurugika mara kwa mara na kuacha , kasha unaweza kupata mojawapo za ishara hizi au hata mbili au zaidi , kushtuka, mtu kuwa dhaifu, kipigo cha moyo kupiga kwa haraka haraka , kuhisi baridi kali, kuumwa na kifua ,midomo kukauka ,kutapika ,tumbo kufura, tumbo kujaa hewa nyingi na hata mtu kushindwa kutoa hiyo hewa ama kufunga choo, mtu kuwa mnyonge ama kuona kizunguzungu,kwenda haja kubwa nyeusi au iliyo na damu, ukiwa na joto kali, ya zaidi ya digirii 38oC ama hewa inayotoka mdomoni kunuka .
 • Hali ya tumbo kuvurugika huwa haishi iwapo utaitibu mwenyewe kwa siku 2 au 3.
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,608
2,000
Kutapika

Kutapika kwa kawaida ni dalili ya kuonyesha kuwa, kuna shida tumboni, umekula chakula kilichoharibika au una mafua.
Unapoumwa sana na kichwa na kupata shida zingine za kiafya, au uja uzito, vinaweza kumfanya mtu atapike. Mara nyingi kutapika sio hoja lakini nyakati zingine, ni muhimu mtu aende atazamwe na daktari.Kuna uwezekano kwamba, unapotapika sana unaweza kuishiwa na maji ya kutosha mwilini.
Namna ya kutibu kutapika:

 • Nusu saa au saa moja baada ya kutapika, kunywa maji kidogo kidogo ama vinywaji visivyo vileo.Usinywe mara moja au kwa wakati mmoja.
 • Pumzika vya kutosha
 • Baada ya tumbo kutulia jaribu kula vyakula vigumuvigumu kama vile mkate mkavu ,ndizi au kitu kizitozito na kitamu kama halua.
 • Meza dawa ya kuzuia joto na maumivu ya mwili ya Panadol au Tylenol.
Muite daktari iwapo:

 • Unaishiwa na maji mwilini.Ukisikia kiu sana , midomo kukauka, mgonjwa kukojoa mkojo uliokolea na huwa anahisi usingizi au kizunguzungu ama huhisi kichwa kikiwa chepesi mno.
 • Shingo kuwa gumu lisiweze kugeuka
 • Unatapika zaidi ya mara kumi kaw siku ama ushindwe kumeza maji yoyote pasipo kutapika.
 • Unahisi maumivu makali ya kifua
 • Utapike damu ama vitu vinavyofanana na kahawa iliyosagwa.
 • Unatapika ukiwa na joto jingi la nyusi 38oc au zaidi ya hapo kwa zaidi ya siku mbili.
 • Unatapika kwa zaidi ya Juma moja .
 • Unashtukia tu ukiwa na maumivu makali ya tumbo ambayo huendelea kuwa machungu.
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,608
2,000
Kuumwa na kichwa / kipandauso

Maumivu ya kawaida ya kichwa huweza kutulizwa na dawa za kuzuia maumivu za aina ya Panadol au aspirini.Iwapo unahisi hayo maumivu kwenye kipji cha uso wako, mashavuni na sehemu zilizo karibu na macho zikifura, kuna uwezekano kuwa umeambukizwa sehemu za kukaza pumzi puani.Iwapo utashikwa na maumivu makali ya kichwa ambayo hayapoi, haikosi kuna uwezekano kuwa umeanza kushikwa na ule ugonjwa sugu wa kipandauso.
Kipandauso (migraine) kina maumivu zaidi kuliko kuumwa kichwa kwa kawaida.Kipandauso huathiri upande mmoja wa kichwa na kuleta kisunzi,au kutaka kutapika.Iwapo unahisi kipandauso unaweza kuona vimulimuli kutokana na muangaza.Pia unaweza kuhisi maumivu makali kwenye jicho moja mara kwa mara.
Ukipatwa na kipandauso, muone daktari wako akuchunguze ili akupe ushauri .Unapopatwa na kipandauso lala chini palipo na utulivu katika chumba kilicho giza kuzuia miale ya jua yanayosababisha kichwa kiume zaidi.
Jaribu usinywe kakao, pombe ama kinywaji chochote kilicho na kakao.Hivi vinaweza kusababisha kipandauso, kunywa maji mengi kila siku.
Utahitajika kumuona daktari ikiwa:

 • Unaumwa na kichwa na hakipoi kwa muda wa juma moja ingawa umemeza dawa za kuzuia maumivu.
Utahitajika kwenda kwa chumba cha dharura ikiwa:

 • Una matatizo unapozungumza, au unasikia kizunguzungu, miguu haina nguvu. Kuna uwezekano kwamba umeanza kupatwa na ugonjwa wa pigo.
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,608
2,000
Mafua

Dalili za homa na mafua ni zilezile.Hivyo basi huenda ikawa vigumu kutambua unachouugua.Kumbuka kuwa iwapo una homa joto la mwili hupanda juu.Hiyo homa pia itakufanya uwe mgonjwa zaidi na hata kuhatarisha maisha ya watu wengine.
"Homa ya kawaida "iko chini ya virusi vimelea vinavyofanya watu wagonjwa .Ni kawaida kwa watu kushikwa mara kadhaa na mafua kwa mwaka.
Dalili za mafua:

 • Kuwashwa na kuumwa na koo
 • Kukohoa
 • Makamasi mengi sana au mazito
 • Kuchemua
 • Kuumwa na kichwa
 • Kuwa na joto mwilini
 • Kukosa hamu ya kula chakula
 • Makohozi ya kimanjano kutoka puani au kwenye koo.Mengine huwa ya kijanikijani hivi.
 • Makohozi ya kimanjano au kijanijani kutoka kwenye pua au kooni.
Namna ya kutibu mafua:

 • Unaweza kunywa dawa baridi, itakayoweza kufungua pua lililoziba na kuumwa na kichwa.
 • Pua likifura na kuwa jekundu paka mafuta ya Vaseline.
 • Tia puani mwako maji ya chumvi ili kuondoa hali ya kukauka inayotokea wakati ambapo unatumia dawa baridi
 • Ili kukabiliana na koo linalowasha, tumia dawa ya kutibu kikohozi pamoja na asali.
 • Kunywa vitu vioevu Kama maji Safi, ama vinywaji ambavyo havina pombe ili kusafisha mwili wako.
 • Pumzika vya kutosha.
Muite daktari iwapo una dalili zifuatazo:

 • Makamasi ya rangi ya kijani au manjano ambayo yamedumu kwa zaidi ya siku kumi
 • Joto la zaidi ya digirii 38oc ambalo lnadumu kwa zaidi ya siku tano
 • Kuumwa na kifua, baridi kali, kupumua harakaharaka.
 • Midomo ya samawati, ngozi au makucha.
 • Kukosa hamu ya kula chakula kwa zaidi ya siku moja
 • Kupoteza maji mengi mwilini
 • Kuhisi maumivu masikioni ambayo inaweza kuwa ishara kuwa hilo sikio limeambukizwa.
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,608
2,000
Ugonjwa wa mapindi

Makamasi yanapojaa puani kutokana na mafua au mzio, kufunguka kwa mifupa ya uso wako unaweza kuhisi kuwa kuna msukumo mkubwa wa nguvu usoni mwako ilihali si vyo .Unaweza pia kusikia uchungu iwapo utaamua kushika mashavu yako au hata popote karibu na pua. Unaweza kutokwa na makamasi ya kijani au kimanjano ambayo huenda yasinuke vizuri, kidonda kooni, kukohoa kupata shida sana unapopumua na kuhisi baridi.
Iwapo mapindi si mabaya sana, unaweza kujihudumia nyumbani.

 • Meza vidonge vya kuyayusha makamasi vilivyo na dawa ya "pseudoephedrine" ndani yake.Vidonge hivi vitamaliza kabisa mapindi na utapumua bila shida.Unaweza pia kutumia dawa ya kupulizia mapua kukabiliana na hali hii.
 • Unaweza pia kupumua mvuke wa moto au maji moto ili mapua yafunguke.
 • Unaweza kumeza dawa za kupunguza maumivu, kuweka kitambaa moto usoni kupunguza uchungu.
 • Kunywa vinywaji moto kama chai, maji moto yaliyo na ndimu isiwe kahawa kwani itafanya mapindi yaume zaidi.
 • Penga pua lako kwa utaratibu
 • Viungo kama tagawizi na kitunguu saumu vinaweza kumaliza kabisa mapindi.
Unahitaji kumuona daktari ikiwa:

 • Unatokwa na makamasi ya kijani au kimanjano
 • Homa yako isipopoa baada ya juma moja
 • Una uvimbe na maumivu kandokando ya jicho lako
 • Una maumivu makali ya kichwa na hata baada ya kumeza dawa ya Tylenol au aspirin hayaishi.
 • Una joto zaidi ya nyusi 38oc
 • Huoni vizuri
 • Unajihudumia nyumbani lakini baada ya siku tatu huoni mabadiliko.
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,608
2,000
Vidonda vya koo

Uvimbe kooni husababishwa na mambo mengi na mara nyingi huwa haisababishi shida kubwa sana.Ukifungana mapua, makamasi hupitia kooni na hivyo basi kusababisha uvimbe.Baridi kavu inaweza pia kufanya koo likauke na mtu ahisi likiwashawasha.Unaposhikwa na mafua, pia unaweza kusababisha kidonda kooni kinachoweza tu kutibiwa na dawa.
Jinsi ya kutibu vidonda vya kooni:

 • Sukutua maji ya chumvi yaliyo vuguvugu
 • Mumunya dawa za koo, usiwape watoto inaweza kumnyonga akimeza kwa bahati mbaya.
 • Muulize mfamasia wako akuuzie kipulizo (spray) cha kutuliza uchungu kooni.
 • Ikiwa koo linawasha au limekauka, pumua mvuke wa maji moto itakusaidia.
Muite daktari ikiwa:

 • Umefura tezi za limfu shingoni.
 • Una mabakabaka meupe huko nyuma ya koo lako.
 • Kwa gafla tu unashikwa na kuumwa na koo huku ukiwa na joto jingi.
 • Koo linavimba na kuuma zaidi ya juma moja.
 • Ukishindwa kunywa chochote umu hatarini mwa kuishiwa maji mwilini.
 • Huku mbele kwa shingo lako pia kumevimba pamoja na koo lako.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom