Kusitishwa kwa maandamano ya chadema mkoa wa morogoro. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kusitishwa kwa maandamano ya chadema mkoa wa morogoro.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shembago, Mar 5, 2012.

 1. S

  Shembago JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu hii ni Taarifa iliyotolewa na BAVICHA kwa vyombo vya habari nawakilisha kwa maelekezo ya mkuu wangu wa kazi!

  Baraza la Vijanala Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, (BAVICHA) Mkoa wa Morogorolimesitisha maandamano ya amani yaliyoandaliwa na Baraza hilo.Maandamano hayoyalipangwa kufanyika tarehe 5/3/2012 katika Mkoa wa Morogoro.Madhumuni yamaandamano hayo yalikuwa kupinga vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na Jeshila Polisi dhidi ya Wananchi wasio na hatia na Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA ).Lengo kuulilikuwa kufikisha ujumbe kwa Serikali na Jeshi la Polisi kiujumla juu yavitendo hivyo vya unyanyasaji ambayo vimekuwa chanzo cha mauaji ya wananchiwasio na hatia na hivyo kuhatarisha amani ya nchi.Hata hivyo, BAVICHA Mkoawa Morogoro imeamua kusitisha maandamano hayo kufuatia kikao cha pamojakilichofanyika tarehe 02/03/2012 kati ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mh. JoelBendera na viongozi wa BAVICHA mkoa na Wilaya ya Morogoro.Katika Kikaohicho kilichofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa CHADEMA iliwakilishwa na Mwenyekiti BAVICHA Mkoa, Mh. BonifaceNgonyani na Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya, Mh. Innocent Zawadi.Kikao hichokilifuatia wito wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mh. Joel Bendera kukutana naviongozi hao kwa lengo la kujadiliana juu ya mambo mbalimbali kabla yamaandamano hayo kufanyika.Hata hivyo,katika kikao hicho, imekubaliwa kuwa uongozi wa BAVICHA Mkoa wa Morogorouwasilishe kwanza kwa Mkuu wa Mkoa kero mbalimbali kwa lengo la kufanyiwa kazina Serikali Mkoa.Mkuu wa Mkoaalieleza kuwa Serikali ( kwa ujumla ) haijashindwa kutatua kerozinazolalamikiwa na BAVICHA hivyo ni busara zikawasilishwa kwake kwanza iliziweze kufanyiwa kazi.Hivyo,imekubaliwa kuwa Viongozi wa BAVICHA Mkoa wa Morogoro watakutana tena na Mkuuhuyo wa Mkoa tarehe 08/03/2012, saa 4.00 Asubuhi katika ukumbi wa Mikutano waOfisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kuwasilisha kero hizo.TAHADHARI:
  BAVICHA Mkoa waMorogoro imekubaliana na maombi ya Mkuu wa Mkoa ya kutaka kusitishwa kwaMaandamano hayo na kuwalisishiwa kero mbalimbali kwa njia aliyoona inafaa nahivyo kutangaza rasmi kusitisha maandamano ya tarehe 05/03/2012. Hata hivyo, BAVICHAinapenda kutoa tahadhari kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro (Serikali ya Mkoa )kushughulikia ipasavyo kero mbalimbali za kijamii zitakazowakilishwa kwake.Iwapoitashindikana, BAVICHA itafufua upya mpango wake wa kuandaa maandamano makubwana ya amani Mkoani Morogoro hadi palekero hizo zitakapopatiwa ufumbuzi.Aidha, BAVICHAinatoa wito kwa Wafuasi wa CHADEMA Mkoa wa Morogoro kuwa watulivu baada yakusitishwa kwa maandamano hayo na kwamba kila hatua ya mazungumzo kati ya Mkuuwa Mkoa na viongozi wao watajulishwa.MWENYEKITIBAVICHA MKOA WA MOROGORO.BONIFACENGONYANI
   
 2. I

  Isango R I P

  #2
  Mar 5, 2012
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Boniface Ngonyani nakuunga mkono, hongera kwa busara uliyotumia, ila serikali yetu inatuona kana kwamba sisi ni mazezeta, wanatufanyia vitu vya kijinga siku hadi siku. Naona Mkuu wa Mkoa wako ana nafuu ndo maana amekubali mnakaa meza moja kujadiliana, wa upande wangu tunaogopana, tunatishiana, tunajibizana katika mikutano ya hadhara, na juzi walitaka kunibip kwa kumkamata Katibu wetu wa CHADEMA Mkoa wa Singida, tuliwaonya wajaribu, naona wamesita. Tunataka kuondoa ukatili, tunataka kuongozwa na serikali isiyofikiri kwa fikra za kikaburu kukandamiza wananchi. Polisi wetu ni ovyo zaidi. Usikate tamaa, singida tumekuunga Mkono.
   
 3. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sana kwa busara yenu BAVICHA, tuko pamoja!!
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  :eyebrows::eyebrows:
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Hongereni makamanda!! Hizi ndiyo njia mhimu za kutatu solution. We have only three stages of solving a problem (a) You pass through normal door (b) If (a)fails, us use the window (c) If the first two fail, then you can pass through the wall (Maandamano).
   
Loading...