Kusita sita kwenda kuanza kibarua

hoop

Member
Mar 16, 2017
45
22
Habarini wakuu!!

Niko dilema kidogo wakuu juu ya hii ajira iliyopo mbele yangu.

Nilikuwa nafanya kazi ktk ofisi moja ya mama wa kihindi ikiwa kama ni kampuni ya familia

Nilifanya kwa muda wa mwezi mmoja bila maelewano yoyote ya mshahara, baada ya mwezi mmoja kuisha alinipa laki moja nilipokea kishingo upande

Niliendelea na kazi baada ya siku kadhaa nilimuuliza kuhusu makubaliano ya mshahara akasema atanipa 150,000, kiukweri nilishindwa kukubaliana nae nikasepa.

Baada ya miaka miwili kuachana nae mwez wa nne kantafuta na kuniambia ananiitaji ofisini nikaenda tukaongea akanipa offer yake ambayo ni 200000 na ku ahidi kuongeza ndani ya miez mitatu

Tatizo lina kuja ni hayo mazingira ya ofisi mambo yanayofanyika humo dah nakosa amani na sina raha kabisa nikiyafikiria matukio hapo nyuma ndani ya mwezi ule niliofanya yananipa wakat mgumu kwenda kuanza iyo kazi. Mambo yenyewe ni

Wanachoma hudi kilasiku

Kulishana vyakula vya ajabu

Mara mtalazimishwa mle nazi as refresher khaa, najiuliza sana vitu kama nazi ofisini inakuwaje

Sometime kutukanwa mbele ya staff wote.

Kufanya kazi siku sita za week kwa pesa madafu.

Na kilicho nichoshaga siku moja niliingia ofsini boss akaja na yy alivokuwa anaingia ndani akaanza kufanya kitendo cha kuesabu esabu ktk ngazi kwa muda kama wa dk tano kama mtu anae chora kitu chini na ukizingatia ni mjini kabisa tena bila uoga, nilichoka

Pia kuna siku member wa familia mmoja ni mdada ni sehemu ya staff akaenda mbele ya mlango na kuanza kufanya kitendo kama cha kutengeneza nywele zake lakin niligundua kuna vitu alikuwa anapaka ktk masikio na ktk nywele zake, nisiwachoshe matukio ni mengi

Nisaidie wadau mm nimechoka kabisa na nashindwa kwenda kuanza hiki kibarua cha huyu mama wa kihindi,,,nijuzeni ni sehemu ya tamaduni zao au ndo ushirikina, sitoweza enjoy na hii kazi kwa mwendo huo. Nipeni mawazo yenu niweze kwenda hatua nyingine, ushauli wenu utanipa mwongozo wa kuamua kwenda kupiga kazi au nimpotezee. poleni kwa kuwachosha kwa urefu wa hii habari

Thanks.
 
Aisee wahindi sio chief lkn kama hauna mchongo wowote inabidi uende tu lkn kataa abuse zozote za kijinga ie kutukanwa ovyoovyo kitu kingine bosi laki 2 maana yake ni bk7/kwa siku,jamani tuacheni ubishoo tufungue hata magenge tutatoka kimaisha
 
Ndugu yangu angalia faida na hasara za kazi yako.

Kama faida ni nyingi kuliko hasara endelea la kama hasara zinazidi faida achana nayo.
 
Yaani miaka miwili iliyopita alikuwa akupe laki na nusu ukakataa, sasa kakuita akupe laki mbili unakubali? unajua kuwa laki na nusu miaka miwili iliyopita inathamani kuliko hata laki mbili ya sasa? alafu miaka yote miwili baada ya kuacha hiyo kazi ulikuwa huna kazi nyingine?
 
Yaani miaka miwili iliyopita alikuwa akupe laki na nusu ukakataa, sasa kakuita akupe laki mbili unakubali? unajua kuwa laki na nusu miaka miwili iliyopita inathamani kuliko hata laki mbili ya sasa? alafu miaka yote miwili baada ya kuacha hiyo kazi ulikuwa huna kazi nyingine?
Nafanya biashara mkuu, but bado haijakaa mkao vizuri sometime tunacheki na kazi ili tuongeze nguvu katka biashara zetu binafsi
 
Aisee wahindi sio chief lkn kama hauna mchongo wowote inabidi uende tu lkn kataa abuse zozote za kijinga ie kutukanwa ovyoovyo kitu kingine bosi laki 2 maana yake ni bk7/kwa siku,jamani tuacheni ubishoo tufungue hata magenge tutatoka kimaisha
Asante sana bro,
 
Kinachofuata hapo ni kutolewa kafara, tafuta kazi nyingine. Miaka 2 unaongezwa 50? Jiongeze
 
Nitumie namba ya huyo, Mimi tutawezana! Yupo sehemu gani kwanza?
 
Back
Top Bottom