kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,990
- 17,869
Kusimamishwa uuzaji wa mafuta ya Iran, ni ukweli au ndoto?
Mei 02, 2019 12:00 UTC
Waziri wa Mafuta wa Iran amesema, hata kama kukatwa kabisa na kufikishwa katika kiwango cha sufuri uuzaji nje wa mafuta ya Iran ni matarjio ya Marekani na nchi mbili jirani na Iran, lakini jambo hilo halitekelezeki kivitendo.
Akizungumza jana Jumatano katika ufunguzi wa Maonyesho ya 24 ya Kimataifa ya Mafuta, Gesi, Usafishaji na Petrokemikali hapa mjini Tehran, Bijan Namdar Zangeneh, Waziri wa Mafuta wa Iran amesema: 'Kila mtaalamu anafahamu vyema kwamba nchi mbili jirani na Iran zinasema uongo kuhusu uwezo na akiba yao ya mafuta, hivyo haziwezi kujaza pengo linaloachwa wazi na mafuta ya Iran kwa kutumia mbinu za kimaonyesho na kisaikolojia.'
Tarehe 22 Aprili mwaka huu, Marekani ilitangaza kwamba haitarefusha muda wa kibali ilichotoa kwa ajili ya baadhi ya nchi kuendelea kuagiza mafuta kutoka Iran. Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema kwamba Saudi Arabia na Imarati zimetoa ahadi ya kujaza pengo litakaloachwa wazi na marufuku ya mafuta ya Iran katika soko la kimataifa. Siasa za Washington kutoa 'mashinikizo makali zaidi' dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa madai ya kufikisha uuzaji nje wa mafuta yake katika kiwango cha sufuri zinafuatiliwa kwa karibu na watawala wa White House na ndio maana wakafutilia mbali kibali kilichotajwa kwa baadhi ya nchi zilizokuwa zimeruhisiwa kununua mafuta hayo kutoka Iran. Jambo hilo linabainisha wazi kuendelea kwa siasa zilizofeli za upande mmoja za Rais Donald Trump wa Marekani katika ngazi za kimataifa. Serikali ya Trump inatumia kila njia na mbinu ili kubadilisha sera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ndio maana ikawa inatoa mashinikizo ya kila upande ya kiuchumi dhidi ya taifa la Iran. Siasa za upande mmoja za Trump zina maana ya kulazimishwa nchi zote za dunia kufuata siasa za serikali ya Washington. Katika uwanja huo Muhsin Mujtaba, mtaalamu wa sheria za kimataifa anasema: Katika fremu ya siasa zake za upande mmoja, Marekani inataka kuilazimisha dunia iendane na matakwa pamoja na maslahi yake, jambo ambalo halikubaliki kabisa katika mtazamo wa kisheria.
Siasa za hivi sasa za Marekani dhidi ya Iran zinahatarisha usalama wa nishati ulimwenguni ni bila shaka jambo hilo litazidhuru nchi zote za dunia. Kwa kutilia maanani ukweli huo, ni wazi kuwa kuna ulazima wa kusimama imara mbele ya siasa hizo za kijuba za Marekani. Siasa za upande mmoja za Marekani zina madhara makubwa katika ngazi za kimataifa na hivyo kuna udharura wa kukabiliana nazo. Misimamo ya wazi ambayo imechukuliwa hivi karibuni na baadhi ya nchi kuhusiana na suala la kutorefushwa muda wa kibali cha Marekani kinachoziruhusu baadhi ya nchi kuendelea kununua mafuta ya Iran bila shaka inaonyesha kuwepo kwa aina fulani ya upinzani wa kimataifa dhidi ya siasa hizo hatari za Marekani, na ni wazi kuwa iwapo dunia itakaa kimya kuhusiana na suala hilo basi sheria za mwitu zitachukua nafasi ya utawala wa sheria zinazopaswa kufuatwa na jamii ya mwanadamu.
Mbali na kuanza kudhiri dalili hizo za upinzani dhidi ya siasa za kibeberu na kibabe za Marekani katika ngazi za kimataifa, katika mtazamo wa kiufundi na kielimu pia hakuna uwezekano wowote wa kuzibwa pengo linaloweza kuwachwa wazi kutokana na kusimamishwa kabisa uuzaji wa mafuta ya Iran katika soko la kimataifa. Nukta ya kwanza ni kuwa, kinyume na matarajio ya Marekani, Saudia na Imarati katika mtazamo wa kiufundi na usafishaji mafuta, hazina uwezo wa kuzalisha mafuta kuliko kiwango chao cha hivi sasa na ahadi zilizotolewa katika uwanja huo kimsingi ni za kisaikolojia tu. Nukta ya pili ni kuwa wepesi wa mafuta ya Iran unayafanya mafuta hayo yasiwe na mshindani yoyote kati ya nchi mbili hizo za Kiarabu.
Mafuta haya ya Iran katika mtazamo wa viwango vya wepesi na uzito unaohitajika katika matumizi ya viwanda mbalimbali ulimwenguni vikiwemo vya mabara ya Asia na Ulaya, yana ubora wa hali ya juu na maalumu yakilinganishwa na mafuta ya Saudi Arabia na Imarati. Ni kutokana na ukweli huo ndipo nchi nyingi za dunia zikiwemo India na Korea Kusini, zikalalamikia vikali siasa za upande mmoja za Marekani za kuyawekea vikwazo mafuta ya Iran.
Katika uwanja huo, Shirika la uchumi la Korea Kusini hivi karibuni lilitoa taarifa likitangaza kukasirishwa na uamuzi wa Marekani wa kuzuia ununuzi wa mafuta ya Iran na kusema: Hakuna mbadala mwingine bora wa mafuta sokoni kuliko mafuta ya Iran.
Viwanda vya kusafisha mafuta vya baadhi ya nchi zinazonunua mafuta kutoka Iran vinaoona tu na aina ya mafuta yanayozalishwa nchini Iran na vimejengwa kuambatana na viwango vya uzito wa mafuta ya Iran. Kwa kuzingatia mazingira yanayotawala hivi sasa katika soko la kimataifa la mafuta na ubora wa mafuta ya Iran katika soko hilo ukilinganishwa na wa mafuta ya Saudia, kivitendo hakuna mbadala wowote wa mafuta ya Iran katika soko hilo, hivyo kutumiwa mafuta kama chombo cha kisiasa bila shaka kutakuwa na matoke mabaya na hatari.
Tags
IRAN MAFUTA