Kusimamishwa kwa mchungaji Kimaro KKKT Mashariki na Pwani

ZEE LA HEKIMA

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
1,417
1,829
Nadhani watu wengi hawaelewi ni kwa nini wapenzi wa mahubiri ya Mch Kimaro, na waumini wengi wa Kanisa lake la Kijitonyama WAMECHUKIZWA SANA NA KUSIMAMISHWA KWAKE.

Naowaomba wanaowalaumu wanaomtetea Kimaro waelewe yafuatayo:-

1. Hakuna Mkristo yeyote ambae haelewi kwamba kulingana na dhehebu, kiongozi yeyote wa dhehebu kuanzia muumini wa kawaida mpaka askofu anaweza kupewa adhabu iwe ya kusimamishwa utumishi au hata kufukuzwa kabisa uanachama wa dhehebu kama ana makosa yaliyo kinyume na neno la Kristo na ambayo yameidhalilisha kanisa na Ukristo.

2. Hakuna Mkristo yeyote ambae hajui kwamba padri au mchungaji anaweza kuhamishiwa usharika au kanisa lingine lakini sababu iwe ni kukuza imani ya Wakristo na kusambaza neno wala sio kumkomoa auadhabu kwa anayehamishwa.

3. Hakuna Mkristo ambae hajui kwamba watu wote (pamoja na waliomfukuza Kimaro) wana mapungufu yao. Kwa hiyo, hakuna mtu anayesema Kimaro asichukuliwe hatua za kinidhamu kama kakosea.

BAADA YA KUSEMA HAYA NAOMBA NISEME YAFUATAYO:-

1. KUMSIMAMISHA KIMARO ASIFUNDISHE NENO LA MUNGU NI KINYUME NA BIBLIA NA SIO JAMBO LA KI-MUNGU
Kumsimamisha Kimaro wakati ndio ameanza semina ya wiki mbili ya neno la Mungu INALETA PICHA MBAYA SANA kwa waumini, wapenzi wake, na hata kwa dini nyingine. Semina ni kwa ajili ya kufundisha neno la Mungu. Ni shetani peke yake ndie anayepinga neno la Mungu lisihubiriwe. Kwa kujua hilo, viongozi waliomsimamisha, wangesubiri kwanza amalize semina ndipo wamsimamishe.

Siamini kwamba Mungu amefurahia kitendo cha kumzuia Kimaro kuwafundisha watu mambo ambayo Mungu alikuwa amemwelekeza kuwafundisha waumini na wapenzi wake wengine. Pengine hio semina ingeendelea, kuna watu wangempokea Yesu waokoke na wajiunge na hilo kanisa la KKKT Kijitonyama. Naamini KKKT inafurahi wakati idadi ya waumini inaongezeka. Kwa hiyo, kitendo cha kumnyima kuendelea na semina sio "msukumo wa ki-Mungu" kwa kuwa ni shetani pekee anayepinga neno la Mungu.

2. Tumesikia viongozi wa hilo kanisa wakisema "uchunguzi" unaendelea ijulikane ni makosa yapi Kimaro kafanya. Hivi kweli unaweza kumfunga mtu halafu akiwa gerezani ndipo uanze kuchunguza kama alifanya kosa?

3. Tuseme kwa mfano, Kimaro amefanya makosa makubwa yaliyo kinyume na msimamo wa KKKT, yanayostahili adhabu kulingana na taratibu zao. Hapo hapo, waumini hawajaona kosa la Kimaro. Viongozi wakimfukuza, wakati waumini wa kanisa hilo HAWAJAONA KOSA LAKE, si jambo lililo wazi kabisa kwamba waumini wake, wapenzi wa mahubiri yake, na hata waumini wa dini nyingine wataona wazi kwamba Kimaro kafukuzwa kwa CHUKI BINAFSI, HUSUSAN WIVU?

4. Kila dhehebu la Kikristo linasisitiza sana waumini wake kufuata amri ya msamaha ambayo Yesu aliifafanua akasema TUSAMEHE SABA MARA SABINI (Mt 18:22). Kama Kimaro amelikosea dhehebu lake MARA SABINI kwa nini viongozi wake wasimsamehe hizo mara sabini?

MAPENDEKEZO YANGU
1. Kimaro arudishwe hapo Kijitonyama AMALIZE SEMINA YAKE KWANZA (watu wapate kile ambacho Mungu alikuwa ameweka ndani ya moyo wa Kimaro kuwafundisha wahudhuriaji wa semina). Hata kama baada ya hapo atapewa hiyo likizo aliyoambiwa ni sawa tu.

2. Uongozi wa kanisa umsamehe kama alifanya makosa. Wamwachie Mungu amhukumu Yeye mwenyewe maana Mungu alishaweka amri "MSIHUKUMU MSIJE MKAHUKUMIWA NINYI (Mt 7:1-5). Na Mungu akaendelea kusema "kipimo kile mpimiacho ndicho mtakachopimiwa"

Na tena, kama uongozi wa kanisa utakataa kumsamehe, ujue kwamba Mungu alishasema "bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu (Mt 6:15)

MWISHO:-

Nawaomba Wakristo wenzangu tumwombe Mungu ajue mwenyewe atakavyo-solve tatizo hili. Hakuna linaloshindikana kwa Mungu
 
Dini ni biashara, hapo kuna mgogoro wa Kimaslahi.

Kama adabu hatua za kinidhamu wa kwanza ilibidi awajibishwe Askofu Malasusa, huyu alikuwa chawa kabisa wa Magufuli.
 
Kimaro hamna kitu hapo kavembewa huyo na uchaga mwingi sana
 
Anatakiwa afukuzwe kabisa anaita mpaka dhehebu lililomlea madalali wa kuuza vitu..anakiburu fulani.
Ila kuna makabila hata wakiwa watumishi wanakuwa kama waharibifu tu fulani hivi
 
Nilimtetea hadi povu likakauka,nilishavutwa na hoja ya mgongano wa maslahi,ila nilipokuja kumsikiliza vizuri nikaona aibu, tena anapoongelea wakristo anawaita "Nyie" kama vile yeye si mmoja wao,alizidisha sifa,umaarufu nao ukampiga ngwara,ajitafakari na kuomba msamaha,naye atasamehewa hizo mara 7×70,
 
Nadhani watu wengi hawaelewi ni kwa nini wapenzi wa mahubiri ya Mch Kimaro, na waumini wengi wa Kanisa lake la Kijitonyama WAMECHUKIZWA SANA NA KUSIMAMISHWA KWAKE.
1. Hana kanisa, ni mchungaji TU wa Usharika.
2. Umepimaje hizo chuki? Hadi ukasema "Wamechukizwa sana"?
 
Nilimtetea hadi povu likakauka,nilishavutwa na hoja ya mgongano wa maslahi,ila nilipokuja kumsikiliza vizuri nikaona aibu, tena anapoongelea wakristo anawaita "Nyie" kama vile yeye si mmoja wao,alizidisha sifa,umaarufu nao ukampiga ngwara,ajitafakari na kuomba msamaha,naye atasamehewa hizo mara 7×70,View attachment 2487846
Hahahahahaha Kuna post yangu ya mwaka Jana, Kuna watu walinitukana sana.
 
Wakati nasoma UDSM nilikua kiongozi wa CCT, CCT wao wana utaratibu wa Kila dhehebu kupeleka mchungaji Kila baada muda flani, basi miaka Ile aliondoka mchungaji tuliyemkuta akaletwa mchungaji mwingine, ila hakukaa Sana muda ukaisha akatakiwa kuondoka .

Kilichotokea ndio kinachotokea kwa Kimaro, alikuja Katibu Mkuu wa CCT kusuluhisha na ndio tukajua kumbe jamaa alishapewa Hadi warnings kadhaa.

Hizi mambo sivyo zilivyo huko ndani. Kimaro Sio exceptional
 
Nadhani watu wengi hawaelewi ni kwa nini wapenzi wa mahubiri ya Mch Kimaro, na waumini wengi wa Kanisa lake la Kijitonyama WAMECHUKIZWA SANA NA KUSIMAMISHWA KWAKE.

Naowaomba wanaowalaumu wanaomtetea Kimaro waelewe yafuatayo:-

1. Hakuna Mkristo yeyote ambae haelewi kwamba kulingana na dhehebu, kiongozi yeyote wa dhehebu kuanzia muumini wa kawaida mpaka askofu anaweza kupewa adhabu iwe ya kusimamishwa utumishi au hata kufukuzwa kabisa uanachama wa dhehebu kama ana makosa yaliyo kinyume na neno la Kristo na ambayo yameidhalilisha kanisa na Ukristo.

2. Hakuna Mkristo yeyote ambae hajui kwamba padri au mchungaji anaweza kuhamishiwa usharika au kanisa lingine lakini sababu iwe ni kukuza imani ya Wakristo na kusambaza neno wala sio kumkomoa auadhabu kwa anayehamishwa.

3. Hakuna Mkristo ambae hajui kwamba watu wote (pamoja na waliomfukuza Kimaro) wana mapungufu yao. Kwa hiyo, hakuna mtu anayesema Kimaro asichukuliwe hatua za kinidhamu kama kakosea.

BAADA YA KUSEMA HAYA NAOMBA NISEME YAFUATAYO:-

1. KUMSIMAMISHA KIMARO ASIFUNDISHE NENO LA MUNGU NI KINYUME NA BIBLIA NA SIO JAMBO LA KI-MUNGU

Kumsimamisha Kimaro wakati ndio ameanza semina ya wiki mbili ya neno la Mungu INALETA PICHA MBAYA SANA kwa waumini, wapenzi wake, na hata kwa dini nyingine. Semina ni kwa ajili ya kufundisha neno la Mungu. Ni shetani peke yake ndie anayepinga neno la Mungu lisihubiriwe. Kwa kujua hilo, viongozi waliomsimamisha, wangesubiri kwanza amalize semina ndipo wamsimamishe.

Siamini kwamba Mungu amefurahia kitendo cha kumzuia Kimaro kuwafundisha watu mambo ambayo Mungu alikuwa amemwelekeza kuwafundisha waumini na wapenzi wake wengine. Pengine hio semina ingeendelea, kuna watu wangempokea Yesu waokoke na wajiunge na hilo kanisa la KKKT Kijitonyama. Naamini KKKT inafurahi wakati idadi ya waumini inaongezeka. Kwa hiyo, kitendo cha kumnyima kuendelea na semina sio "msukumo wa ki-Mungu" kwa kuwa ni shetani pekee anayepinga neno la Mungu.

2. Tumesikia viongozi wa hilo kanisa wakisema "uchunguzi" unaendelea ijulikane ni makosa yapi Kimaro kafanya. Hivi kweli unaweza kumfunga mtu halafu akiwa gerezani ndipo uanze kuchunguza kama alifanya kosa?

3. Tuseme kwa mfano, Kimaro amefanya makosa makubwa yaliyo kinyume na msimamo wa KKKT, yanayostahili adhabu kulingana na taratibu zao. Hapo hapo, waumini hawajaona kosa la Kimaro. Viongozi wakimfukuza, wakati waumini wa kanisa hilo HAWAJAONA KOSA LAKE, si jambo lililo wazi kabisa kwamba waumini wake, wapenzi wa mahubiri yake, na hata waumini wa dini nyingine wataona wazi kwamba Kimaro kafukuzwa kwa CHUKI BINAFSI, HUSUSAN WIVU?

4. Kila dhehebu la Kikristo linasisitiza sana waumini wake kufuata amri ya msamaha ambayo Yesu aliifafanua akasema TUSAMEHE SABA MARA SABINI (Mt 18:22). Kama Kimaro amelikosea dhehebu lake MARA SABINI kwa nini viongozi wake wasimsamehe hizo mara sabini?

MAPENDEKEZO YANGU

1. Kimaro arudishwe hapo Kijitonyama AMALIZE SEMINA YAKE KWANZA (watu wapate kile ambacho Mungu alikuwa ameweka ndani ya moyo wa Kimaro kuwafundisha wahudhuriaji wa semina). Hata kama baada ya hapo atapewa hiyo likizo aliyoambiwa ni sawa tu.

2. Uongozi wa kanisa umsamehe kama alifanya makosa. Wamwachie Mungu amhukumu Yeye mwenyewe maana Mungu alishaweka amri "MSIHUKUMU MSIJE MKAHUKUMIWA NINYI (Mt 7:1-5). Na Mungu akaendelea kusema "kipimo kile mpimiacho ndicho mtakachopimiwa"

Na tena, kama uongozi wa kanisa utakataa kumsamehe, ujue kwamba Mungu alishasema "bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu (Mt 6:15)

MWISHO:-
Nawaomba Wakristo wenzangu tumwombe Mungu ajue mwenyewe atakavyo-solve tatizo hili. Hakuna linaloshindikana kwa Mungu
Tatizo limeshatatuliwa. Amepewa likizo ya miezi miwili kwa mujibu wa katiba ya kanisa! Akimaliza anatakiwa akaripoti makao makuu
 
Back
Top Bottom