Kusimamishwa kwa Askofu Gwajima na Silaa; Je, wana ugomvi binafsi na Spika wa Bunge? Angalia utaratibu uliotumika

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,415
2,000
Hivi ndivyo ilivyojiri kikaoni (bungeni) tarehe 31 Agosti 2021 (sio rasmi)

Mwenyekiti wa Kamati: (Baada ya kuwasilisha taarifa ya kamati) Mheshimiwa Spika, Natoa Hoja wabunge hao wasimamishwe kuhudhuria mikutano miwili ya bunge

Spika Ndugai: Hoja imepokelewa na kuungwa mkono.

Spika Ndugai: Sasa nawakaribisha wabunge waweze kujadili hoja (ambayo tayari imeshaungwa mkono). Mwenyekiti, kaa hapa wewe ndio mtoa hoja.

Mbunge wa 1 mpaka wa 8 (Wote wakiwa ni wajumbe wa Kamati iliyowasilisha hoja): Tunaunga mkono hoja

Mbunge wa 9 na wa 10: Wasio wajumbe wa Kamati: Tunaunga mkono hoja

Spika Ndugai: Mtoa hoja, funga hoja yako.

Mwenyekiti wa Kamati: Kwa mara ya kwanza naona leo, hoja inaungwa mkono na wabunge wote waliochangia (Wabunge 10 na wabnge 8 wakiwa ni wanakamati), hakuna hata mbunge mmoja anayepinga hoja. Nafikiri hii inaonesha ni namna gani wabunge wamekasirishwa na matendo ya mashahidi (wabunge watuhumiwa) na pia imeonesha weledi wa Kamati wakati wa kushughulikia jambo hili.

Spika Ndugai: Sasa tunapitisha azimio kwa kura kama utaratibu wetu ulivyo. Wanaounga mkono hoja waseme NDIYO!

Sauti nyingi nyingi kwa pamoja: NDIYOOOO

Spika Ndugai: Wasiounga mkono hoja waseme SIYO

Kimyaa

Spika Ndugai
: Waliosema NDIYO wameshinda, Bunge limeunga mkono hoja na limepitisha azimio kuwa Waheshimiwa Josephat Gwajima na Jerry Slaa wasimamishwe kuhudhuria mikutano miwili ya bunge. Kipindi walichosimamishwa watalipwa nusu mshahara na wasikanyage viwanja vya bunge.

Aliyepo bungeni leo ni Mheshimiwa Jerry Slaa, Mheshimiwa Slaa ninaomba utoke, askari akuongoze nje ya ukumbi wa bunge tuonane Januari 2022. Waheshimiwa wabunge niwasihi sana, someni hizi kanuni za bunge, huwezi kushindana na spika halafu ukawa salama, kila sehemu inamtaja Spika, spika, spika!! Spika ndio kila kitu hapa bungeni.​
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom