Kusimamishwa kazi kwa kamishna mkuu TRA je bodi yake ilikuwa wapi

mastersajenti

Senior Member
Dec 4, 2015
165
23
Watanzania napenda nimpongeze Mh.Rais Magufuli Kwa hatua ya kumsimamisha Kazi Kamishna Mkuu TRA Kwa kuhusika Na upotevu Wa makontena Na ukwepaji mkubwa Wa kodi.Swali langu je Bodi ya TRA ilikuwa wapi mpaka Rais agundue wizi huo?Kwa kitendo cha Rais kugundua wizi in dhahili Bodi imezembea nilitarajia Na Bodi ingevunjwa Mara moja.
 
watanzania tukubali tusikubali tawala zilizopita za ccm zilikuwa na kawaida ya kuchukua pesa ktk mashirika mengi ya serikali so ilikuwa vigumu sana kuzuia hiki tunachokiona sasa kwa hiyo rais wetu wa sasa ameamuua kujivua uccm na ndiyo maana unaona haya yanatokea jiulize CAG ,TAKUKURU TISS walikuwa wapi kwa hiyo ujinga huu ulikuwa na Baraka za jk
 
Sio tu bodi....
Tra haikuwa na wakaguzi wa ndani na wa nje?
He waliripoti hilo tatizo kwenye taarifa zao?
Management na bodi walizipata hizo taarifa? Zilifanyiwa kazi au walizitupa kwenye dustbin????

Kama hawakurepoti hata hao wakaguzi (especially wa ndani) hawafai
 
Ndiyo tatizo la kufanya kazi kwa kushtukiza. Pangekuwa na mpangilio yote haya yangefuatiliwa na ukweli zaidi ungwfahamika na wengi zaidi wangetiwa mbaroni.
 
Ndiyo tatizo la kufanya kazi kwa kushtukiza. Pangekuwa na mpangilio yote haya yangefuatiliwa na ukweli zaidi ungwfahamika na wengi zaidi wangetiwa mbaroni.

wengi akina nani mkuu hawa wanatosha kabisa maana mwenye mbwa yu ndani .. atataja tu na kuna siku hizi kukujua kuwa umepata mali kwa njia za wizi ni rais mno maana wakichungulia kwenye account tu wanakudaka
 
Vipi kama hayo makontena hayakuwekwa katika rekodi kabisa?
 
Bodi nyingi za mshirika ya umma zimejaa waganga njaa ambao hawajui majukumu yao ni nn, wanawanyenyekea mabosi badala ya wao kunyenyekewa, wantetemekea posho kama vile huyo bosi anzitoa mfukoni kwake, wengine ni unemployed kila siku utawakuta ofisi za mashirika kama vile ni muajiriwa
 
Back
Top Bottom