Kusikia aibu kwa kitu alichokifanya mtu mwingine sababu ni nini?

Zacht

JF-Expert Member
Jul 17, 2020
1,009
2,197
Habari wakuu,

Kabla sijaenda moja kwa moja kwenye swali langu naomba nijieleze nilivyo

Mimi binafsi sipendi kabisa kuhaibika huwa najiepusha sana na mambo ambayo yanaweza kumuaibisha mtu, kuongea hata vitendo

Imeafika steg hadi nikienda toilet nakagua mara nyingi kama choo kisafi baada kukitumia, kama nimeflash choo siondoki hadi nihakikishe mzigo umesafiri vizuri.

Hivyo hivyo hata kwenye kuvaa, kuongea, kutembea yani design kama sijiamini lakini yote yanafanya nisihaibike na nashukuru mimi kuhaibika kwenye mambo kama hayo ni very rare.

Sasa shida nilyokuwa nayo ukiacha kutojiamini ni kusikia aibu ya mwingine, kitu unaweza kufanya wewe lakini aibu naisikia mimi, muda mwingine naziba masikio au namkwepa huyo mtu nisisikie aibu... Sasa imekuwa kama ugonjwa kwangu kuna muda natamani kuishinda hiyo hali lakini naona kama mtihani mzito.

Sasa naomba mnisaidie je tatizo kuna mwingine linamsumbua, linasababishwa na nini, madhara yake, na tiba yake??

Asanteni
 
20200816_195541.jpg
 
Unapatwa na Hali hiyo sababu umeshajijengea mazoea.lakini ukiamua kuacha inawezekana!
 
Back
Top Bottom