Kushushwa kwa bei za vifurushi vya intaneti

Kivumishi Kielezi

JF-Expert Member
Nov 1, 2019
1,028
2,448
Kwa kadiri teknolojia inavyopanuka, ndivyo watu wengi wanavyozidi kutumia simu janja na vifaa vingine vyenye upatikanaji wa intaneti!

Nilitegemea kutokana na wingi wa watumiaji wa intaneti, makampuni yatakua yamepanua sana wigo wa mapato na faida, hivyo kuwawezesha watu kununua vifurushi kwa gharama nafuu!

Badala yake makampuni ya simu yanazidisha gharama kila kukicha. Sikuwahi kuona gharama zinashuka. Zinapanda tu.

Ni lini vifurushi vya intaneti vitashuka gharama? au tusubiri miujiza?

Makampuni ya simu yamefanya intaneti kuwa bidhaa ya anasa na ya wenye ukwasi!

Utapeli mtupu!
 
INTERNET NI MAENDELEO YA HIGH-TEC,KUNA ELIMU MARIDHAWA YA HALI YA JUU NDANI YAKE..KUNA ELIMU AMBAYO HATA MADARASANI NA NDANI YA VYUO VIKUU HAIPO...!
 
Back
Top Bottom