Naomba niseme wazi kabisa, siasa za kudanganyana zitaangamiza nchi hii. Kila linalopigiwa kelele serikali inalitekeleza hata kama uwezo wa nchi ni mdogo.
Yapo madai kwamba bei ya units zinazozalishwa ni nafuu saana kiasi kwamba kuna haja ya kupunguza bei.
Ni wazi kwamba TANESCO inapata ruzuku kutoka serikalini. TANESCO inajiendesha kwa hasara na TANESCO ina madeni makubwa ambayo yanatishia uhai wake hii ni kutokana na uchakavu wa mitambo, urasimu, rushwa, uzembe na siasa.
Sasa hivi TANESCO wameshinikizwa kupeleka maombi EWURA ili bei ya umeme ipunguzwe. Maana yake ni kwamba hata yale malengo ya kuhakikisha nchi inawaka au kutumia umeme hadi asilimia 75 huenda yakachelewa au pesa nyingi zaidi zikaenda hivyo.
Ni ukweli uliowazi kwamba serikali cha kufanya inge-freeze bei ya umeme na si kuteremsha. Mahitaji yawe ni umeme wa uhakika ni si kupunguza bei.
Vinginevyo ile pesa ambayo ingepelekwa kwenye elimu, barabara na afya inatumika kulipia umeme. Hili hapana.
Tukiwa na umeme wa uhakika na tukazalisha wa kutosha ndio bei ipunguzwe. Katika hali ya kawaida huwezi kuwa unapata hasara na unaendelea kupunguza bei ya bidhaa.
Wataalam wa uchumi payukeni.