Kushuka umaarufu kwa muziki wa bongo fleva..

Lavit

JF-Expert Member
May 16, 2011
13,110
26,997
Bado sijajua kipi hasa kimewakumba wasanii wetu, kiukweli wasanii wanaofanya kazi serious ni wachache sana watu wamebaki kusifia video tu!

Nikisikiliza na kuangalia hizo top 10/20 zao huwa huwa hata sielewi wanaimba nini! Hapa hata ukiniambia nitaje ngoma kali 10 tu kwa sasa siwezi kufikisha hata 3, sijui bongo fleva inaenda wapi!

Ukirudi mtaani wengi wanasikiliza old skul za miaka ya 2000, ukiwauliza kulikoni wanadai muziki ulikuwa zamani!

Mimi mwenyewe 80% ya bongo fleva nilizonazo ni oldies, playlist yangu mara nyingi inabeba oldies!

Ninachojiuliza kipi kimekumba muziki wetu, kwanini hakuna ngoma kali tena? Kwanini nyimbo zinakaa wiki mbili zinapotea? Je inawezekana media zinawabeba wasanii wabovu na kuwaacha wale wakali??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili suala ni kweli mkuu usemavyo siku hizi wasanii wengi sana, halafu unakuta maudhui ya nyimbo yanafanana kwa kiasi kikubwa...Ubunifu unapotea, kwa hiyo usishangae ukikuta mtu anasikiliza playlist ya oldies..

Sometimes pia media zinachangia mkuu..
 
Hili ndicho watanzania wanataka.Kwamba wanamuziki wakubwa warudi chini au kupotea kabisa.Yan kama kauli ile ya matajiri waje kuishi kama maskini.
Unakuta mtu anakuambia mfano Diamond au weusi kuwa hawajui kitu,hawana lolote.Kwamba mwisho wao umefika.Huyo ni mtanzania wa kawaida anaesema hayo kuwa wasanii wakubwa wapotee tu.
Sasa najiuliza kama watu wanaonesha njia ya muziki wetu kupaaa zaidi na bado SISI WENYEWE tuna kuwa wachawi wa sanaa yetu unategemea tutafika wapi????
MUDA TUACHE CHUKI NA WIVU WA KIJINGA KWA HAWA WASANII WETU.BEEF ZISIINGIE KATIKA KAZI AU SANAA YA WASANII WETU.BADALA YAKE TUUNGANE KATIKA KUSAPOTI MZIKI WETU.
Ama sivyo kama mdau alivyosema ni kweli mziki wetu unakufa aseee.
 
Ukiachana na bongo flavour ya akina Ferooz,Mac D,Dudu Baya,Fagio la chuma,Bizman,University corner na wengineo wengi ambao walikuwa wakiumiza vichwa plus production kali kama za P.Funky,Master J,Mika Mwamba na Said Comorien.Sasa hiv Hamna Music tena ila kuna kelele ambazo zinafanana na music,huwa cpati hisia zozote nikisikiliza bongo flavour ya hivi sasa kwa sabab haina Uniqueness

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili ndicho watanzania wanataka.Kwamba wanamuziki wakubwa warudi chini au kupotea kabisa.Yan kama kauli ile ya matajiri waje kuishi kama maskini.
Unakuta mtu anakuambia mfano Diamond au weusi kuwa hawajui kitu,hawana lolote.Kwamba mwisho wao umefika.Huyo ni mtanzania wa kawaida anaesema hayo kuwa wasanii wakubwa wapotee tu.
Sasa najiuliza kama watu wanaonesha njia ya muziki wetu kupaaa zaidi na bado SISI WENYEWE tuna kuwa wachawi wa sanaa yetu unategemea tutafika wapi????
MUDA TUACHE CHUKI NA WIVU WA KIJINGA KWA HAWA WASANII WETU.BEEF ZISIINGIE KATIKA KAZI AU SANAA YA WASANII WETU.BADALA YAKE TUUNGANE KATIKA KUSAPOTI MZIKI WETU.
Ama sivyo kama mdau alivyosema ni kweli mziki wetu unakufa aseee.
Mkuu kwanini mtu akitoa maoni yake mnakuja kucoclude na habari za chuki, mimi katika muziki napata burudani na ndo burudani yangu kuu..sasa niwachukie wasanii kwa lipi labda??

Mimi sikioni hicho cha kusupport, maana hakuna ubunifu wowote wa ziada zaidi ya kucopy na kupaste!

Mbona us wasanii wakubwa wa wadogo wote wanafanya kazi zinaeleweka, hakuna mtu anataka eti wasanii wapotee...

Mi siku zinavyoenda mbele naanza kujikuta nahama kwenye huu muziki wetu, nawasikiliza zaidi akina Bieber, Zayn, Shawn Mendez, Selena,Zarra na wengine..atleast nyimbo zao naweza kuzisikiliza na kuzirudia mara mbili mbili!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukikutana na wazee wa zamani watakwambia tokea amefariki Marijani Rajabu hakujawahi kutokea mwanamuziki Tanzania,kwa kifupi you're growing old.Wanamuziki huwa manakua namashabiki wao, kijana anaeibukia kupenda muziki sasa hivi huwezi kumuelezea flavours unazopenda we wewe, atakuona haujui kitu, una mambo ya kizamani na umepitwa na wakati.Concentrate na muziki unaokufurahisha hii mingine waachie wanaoipenda,ni wengi mno ndio soko linazidi kuongezeka halikadhalika na kipato chao kinaongezeka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom