Kushuka huduma za mawasiliano si ndoto tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kushuka huduma za mawasiliano si ndoto tena

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Sep 21, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Sep 21, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ukiwasha radio yako sasa hivi kila dakika 30 hivi utasikia kampuni fulani ya simu ikitangaza punguzo la bei kwa huduma zake za mawasiliano haswa mawasiliano kati ya wateja wa kampuni moja na zile za mtandao yaani Internet.

  Hapo mwanzo wengi wetu hawakuamini kwamba huduma za mawasiliano zinaweza kushuka kutokana na kuunganishwa na mkonga wa mawasiliano pamoja na huu mpya wa essy Ambapo kampuni nyingi za mawasiliano zimejiunga na huduma zao kwa ajili ya Kutoa huduma za kuwasiliana kwa wateja wao .

  Mimi natumia simu ya mkono ya mtandao wa Zain pekee hapo nyuma niliwahi kuwa na mtandao wa Tigo kutokana na huduma zao kuwa nafuu lakini nilimalizana nao mwaka 2009 katikati toka hapo nikawa natumia zain tu katika mawasiliano ya kawaida .

  Naweza kusema natumia mtandao huo kutokana na kuwa na huduma bora pamoja na kuwa na mtandao unaoeleweka Karibu África nzima na Mashariki ya kati lakini zaidi ni wepesi wa utoaji wa huduma za kwanza endapo umepata tatizo kwenye simu yako linalohusiana na mtandao huo .

  Kule nyumbani ninakifurushi changu ambacho nalipia chini ya alfu 30 kwa mwezi kutokana na matumizi yangu hiyo kifaa nilinunua shilingi alfu 70 lakini tatizo lake ina hati miliki ya kutumika kwenye mtandao wa zain tu kwahiyo nimeshikwa hapo .

  Kwa kuwa wakati mwingi nakuwa niko barabarani nalazimika kuwa na simu yenye uwezo wa mtandao wa Internet kwahiyo nikaamua kuwa na simu hiyo pamoja na kuunganishwa na mtandao wa vodacom hapa huwa nalipa shilingi 500 kwa siku kwa ile huduma yao ya Cheka Internet .

  Pamoja na hayo yote bado kuna chipuka huduma mbalimbali za bunguzo la bei kwa huduma za mawasiliano toka kwa kampuni kama SASATEL , ZANTEL , TTCL NA SELCOM .

  Haya ni maoni yangu tu lakini wewe unaweza kuchagua unataka kutumia mtandao upi wa mawasiliano kutokana na mahitaji yako na shuguli zako unazozifanya mara kwa mara , mfano kama wewe ni msafiri wa mara kwa mara unajua unatakiw akutumia mtandao gani manake kuna mengine ya mujini mujini .

  Hongera kwa kampuni zote zilizoonyesha nia ya kupunguza huduma za mawasiliano nchini na hongera Tume ya mawasiliano Tanzania kwa hatua hii iliyofikiwa mpaka sasa hivi kwa kipindi hichi cha miaka 5 .

  Sasa tufikirie maeneo ya vijijini kwa kushirikiana na saccos za huko na benki za vijijini kwa ajili ya kukopesha wananchi wa huko vifaa vya mawasiliano kama simu na vingine kwa ajili ya kuwasiliana naamini wale ni rahisi zaidi tulipa kuliko watu wa mjini wanao hama hama .

  Na mwisho kuboresha sheria zetu zinazohusu mawasiliano haswa ya mtandao , kule ile inayoitwa Epoca – Electronic and Postal Act hii ilibidi kuongezewa na ile ya Data Protection Act kwa ajili ya kulinda wateja mbalimbali wa huduma za mawasiliano nchini kwa sababu kuna watu wengi wanaadhiriwa kutokana na kukosekana sheria hii muhimu kwa nchi yetu .
   
 2. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  ni kweli kaka, Zaidi Naamini kuna watu wengi wangependa kutumia hizi fursa bt hawajui or wanadhani ni gharama sana, Naamini tutafikia ya India, internet on streets, Dunia Kijiji.
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Sep 21, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Huduma za mawasiliano haswa ya Simu na Internet zimepungua kwa kiasi kikubwa sana ndugu ila tatizo kubwa pia limeonekana ni kwa hizi kampuni za mawasiliano haswa simu kutokupeleka ujumbe kwa njia ya matangazo kwa watu wengi zaidi pamoja na watu wengi zaidi haswa vijana kutokuwa tayari kujaribu baadhi ya huduma kwa imani ile ile ya kizamani kwamba bado ni gharama sana kutembelea mitandao kutumia simu za mikono , ukitaka kitu kama nyimbo kwa mfano nazo ni gharama na vitu vingine vinavyofanana na hivyo .

  Sasa basi kwa kumalizia napenda kutoa ushauri kwa kampuni za mawasiliano haswa simu za mikono ambazo zimejipenyeza maeneo mengi ya nchi kutoa labda offer maalumu kwa rika Fulani la watu haswa vijana mfano hawa wanaoingia chuoni kuanzia mwezi wa 10 mwaka huu mfano kukopeshwa vifaa vya kama Modem au simu zenye uwezo huo kupitia mawakala maalumu ambao watakwepo ndani ya vyuo na mashule yenye wanafunzi wengi zoezi hili liendane na zile offer za kuuziwa vifaa kama laptop na komputa kwa bei rahisi naamini hii ikifanyika vizuri ujumbe utafiki kwa vijana wengi zaidi na italeta changamoto kwa watu kuanza kutafuta masoko mapya kwenye vifaa zaidi na kwenye mitandao ambayo itakuwa inatembelewa na watu haswa vijana .

  Kama mnakumbuka Zain iliwahi kuwa na Offer moja chuo kikuu cha DSM miaka 2 iliyopita ambapo kama mtu anatumia mtandao ule ndani ya eneo la chuo kikuu basi gharama za mawasiliano yake huwa nafuu zaidi hiyo ilifaidisha watu wengi kipindi hicho kwahiyo kunaweza kubuniwa huduma zingine zinazofanana na hizi .

  Naomba niishie hapa kwa leo

  Usiku mwema
   
Loading...