Kushirikiana taulo ni chanzo kikubwa cha maambukizi ya magonjwa ya ngozi

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
49,881
2,000
Unakuta mtu anamtembelea rafiki yake, akitoka kuoga anakuta taulo kwenye kamba analichukua na kutumia, utamsiki “huyu wangu sana “. Watoto wakiwa boarding school, taulo linaweza kula vichwa vitatu bafuni.

Hata hizi hotelini kama unaweza safiri na taulo lako. Fikiria hoteli haina mashine ya kufulia na dobi alilipua tu. Hujui aliyetumia taulo kabla yako alikua na magonjwa gani.

Wengine wana ujasiri wa kununua taulo la mtumba, Pale Karume anafungiwa taulo na akifika nyumbani anaendeleza libeneke. Hali za maisha zinatofautiana, taulo la mtumba ikibidi ulinunue liloweke na maji ya moto na sabuni, lifue uanike juani kabla hujalitumia.

Fungus ni ugonjwa unaoenezwa sana na kuchangia taulo. Pamoja na kutoanika taulo juani. Fungus ni ugonjwa unaousumbua na tiba yake ni ya muda mrefu.
 

Alvin Slain

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
6,184
2,000
Na wale wanaopenda kuazima nguo za watu wengine wanavaa unafikiri hawana uwezekano wa kuambukizana magonjwa ya ngozi kama m'ba nk?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom