Kushindwa kwa zoezi la Sensa; udhaifu mwingine wa JK na Serikali yake! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kushindwa kwa zoezi la Sensa; udhaifu mwingine wa JK na Serikali yake!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wimana, Sep 5, 2012.

 1. W

  Wimana JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 2,453
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 145
  Katika umri wangu ambao si haba nimeshiriki kuhesabiwa kwa miongo kadhaa. Katika miongo yote hiyo, sijawahi kuona zoezi lililodorora na kuborongwa kama Sensa ya mwaka huu. Wengi watakubaliana nami kuwa zoezi la sensa mwaka huu halikuwa na ufanisi na hata takwimu zake zitakuwa za mashaka makubwa na hazitakuwa za kuaminika.

  Hii ni ishara ya ushindi wa Sheikh Ponda na wenzake dhidi ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete na Serikali yake maana kwa ukubwa wa Tanzania, sijawahi kusikia nchi nyingine kama yetu ambayo imefanya zoezi la kuhesabu watu wake kwa wiki mbili! Huko nyuma, zoezi hili lilifanywa kwa siku moja tu na siku zote lilifanikiwa, hakukuwa na Polisi wala viongozi wa Serikali za mitaaa, zoezi lilikuwa shwari na Wachukua taarifa hawakupewa vitoisho vya aina yoyote.

  Kwa zoezi la mwaka huu, jinsi lilivyoendeshwa na kuchukua muda mrefu kukamilika, sina hofu yoyote kuungana na wale waliowahi kusema kuwa Serikali na Rais ni dhaifu.
   
Loading...