Kushindwa kwa sera za CCM ndio chanzo cha umaskini wa Watanzania!

Tatizo CCM haina sera ina propaganda!!

CCM Ingakua na Sera leo hii tungekua tumesonga mbele.

Waliotuangusha ni wale walioirudisha CCM madarakani 2015.

Haiwezekani Chama kimoja kitawale kwa nusu karne halafu kiwe kinapiga mark time. Chama kimoja marais watano lakini hakina mwendelezo wa pale alipoishia mwenzake.

Yaani tulitegemea CCM ambacho kwa muda wote kimeshika dola kiwe na dira ili pale anapoishia rais anayekua madarakani mwenzake anapokuja asipate tabu bali aendeleze aliyokuta lakini badala yake kila anayekuaja anakua kama chama kipya cha upinzani kilichoingia madarakani.

Alipoishia wa Awamu ya kwanza paliishia siku alipong'atuka na kutuambia kuwa ametuletea mtu wa kutupeleka mbele zaidi.

Akaja wa awamu ya pili akapindua kila kitu na kuanza na ya kwake mana dira na uelekeo ulikua umekomea hapo .Tukaambiwa kuwa taifa lilikua lina watendaji wazembe wakubwa na wala rushwa kila kona. Awamu ya pili ikaja na kauli mbiu ya fagio la Chuma. Kila wakati RTD ilikua ikitoa matangazo ya kukemea huku ikiipamba na kuitukuza serikali ya awamu ya pili kuwa imekuja kama mkombozi wa kuitokomeza rushwa na uzembe uliokuwepo kwa watendaji wa serikali. Propaganda zote zilielekezwa kutukuza na kusifia awamu hii. Awamu hii iliwafuta kazi mawaziri kila mara kutokana na tuhuma na utendaji mbaya. Wananchi hawakuona ubaya wa awamu hii mpaka awamu hii ilipokaribia kuondoka madarakani. Pindua pindua ya ikaanza na dira ikaishia hapo CCM na makada wake wakishirikiana na wale wenye siasa kali za kijamaa walioko ndani ya chama na kwenye taasisi za kidini ambao ni makada waliojivika ngozi za viongizi wa dini walianza kuiandama awamu ya pili kwa lengo la kuja na propaganda kuwa sasa atakuja masihi wa kurejesha dira iliyopotea .

Awamu ya pili ikapita waliotumia fursa za awamu hiyo vizuri walitajirika sana kuanzia watawala mpaka wananchi wa kawaida.

CCM ikajipindua tena kwa kuhakikisha kuwa kwanza haiji na mtu wa imani na hulka ya yule wa awamu ya pili. CCM hiyo hiyo ikawatangazia wananchi kuwa hali ya uchumi imekua mbaya na rushwa imekithiri.

Ikaja awamu ya Tatu kauli mbiu ikawa ni ukweli na uwazi.Ikaja na mbinu za kuziba mianya ya rushwa , kulipa madeni na kufungua milango kwa wawekezaji, kubinafsisha mali za umma. Kuuza rasilimali za nchi kwa wawekezaji wa ndani na nje.
Pakawa na maboresho mazuri kwenye ukusanyaji wa kodi.
Tukaambiwa uchumi unakua kwa kasi .
Nchi ikasifiwa dunia nzima kuwa imesiba mianya ya rushwa na kupambana na rushwa. Baadhi ya watendaji wa awamu ya pili wakafikishwa mahakamani kwa rushwa akiwemo waziri wa Ujenzi wa awamu ya pili.

Awamu ikajitahidi kufuata dira yake ya dharura mana ile ya mwanzo ilikua imeshapotea kwa kila mmoja anatafuta kadira ka kumfikisha mwisho wa safari ya utawala wake. Sera ya pamoja ya CCM kama chama haitekelezeki zaidi ya propaganda za kupata uungwaji mkono kwa kuimba wimbo wimbo wa kupambana na rushwa na kisha kuucheza kwa ustadi mkubwa.
Mashirika zaidi ya 350 na nyumba zaidi ya 8000 za serikali zikauzwa. Nadhani hapo serikali ya awamu hiyo ya tatu ilipata mtaji mkubwa wa fedha baada ya kuuza hizo mali za umma pamoja na kuwapa wawekezaji maeneo yenye madini. Hatukua na dira ya kupata fedha zaidi ya kupiga bei mali zetu zilizojengwa na kutafutwa na awamu ya kwanza kama dira ya mwanzo ili ziongezwe na sio kuuzwa.

Awanu ya tatu ikamaliza muda ikiwa imechokwa na wananchi wa chini kutokana na ukame wa fedha mifukoni. Wakati huo Professor Lipumba alikua anavuma sana huku akikosoa mbinu za uchumi za awamu hiyo na akieleza kwa ustadi mkubwa jinsi ambavyo mzunguko wa fedha umekua mdogo wa fedha unavyoadhiri ukusanyaji wa kodi zaidi ya kuwakamua wafanyabiashara wadogo.
Awamu hii ilisifiwa na wale waliokua wanasifia siku zote mana CCM ina makada kila kona kwa hiyo ikiamua tu kupiga propaganda ya jambo lolote basi ni lazima livume na wananchi waliamini kwa gharama yoyote. Wataanzia kwa wakuu wa idara, taasisi na kila aina ya vikundi walipoandaliwa makada wao.

Tatizo ni CCM kushindwa kuwa na dira ya kitaifa na kuisimamia iwekwe kisheria na kikatiba ili kila mtu aifuate.
Awamu ya Tatu ikapita huku ikiandamwa na kashfa nyingi za rushwa na viongozi kujimilikisha mali za umma na kubwa zaidi ikaanzishwa dira ya kushinda uchaguzi iliyoitwa takrima .
Hata hivyo kashfa hizo hazikusemwa sana kutokana nguvu ya wapambe wa awamu hiyo. Zikawekwa kiporo kusubiri awamu itakayofuata.

Awamu ya Nne ikaja na ari mpya ,nguvu mpya na kasi mpya. Kama kawaida propaganda zikaandaliwa bila dira watu wakaaminishwa kuanzia kwenye mitaa mpaka nyumba za ibada walipo andaliwa makada wa kupamba kuwa sasa Sio wanadamu tena waliochagua bali ni Mungu. Yaani Mungu ameamua kuwachagulia watanzania kiongozi. Akaitwa chaguo la mungu. Akaanza kwa ziara za kushtukiza akiwa na majina yote mazuri na kila aina ya shamrashamra huku vyombo vya habari vikitumia jina la Boys II Men.

Mambo yakaanza kwa kasi ya ajabu shule za kata zikajengwa nchi nzima bila dira maalum ya kufuata. Ghafla tu kila kata ikawa na shule. Mikataba ya madini ikawa inaingiwa mchana na usiku, mpaka wakati mwingine wakaamua kuwafuata wawekezaji huko huko na mihuri yao na kumalizana huko juu kwa juu.
Awamu hii ikaja na dira yake ya kukuza demokrasia na utawala bora ,uhuru wa kupata habari ukaongezeka, diplomasia ya kimataifa ikaongezeka mara dufu.
Wawekezaji wakaongezeka ,ujenzi wa majengo ya ofisi za umma ukafanywa kila eneo. Ofisi zikaboreshwa. Mahospitali yakaongezewa majengo na vifaa tiba kuanzia kule Muhimbili mpaka zile za mikoa, Mabarabara yakajengwa kwa kasi zaidi na madaraja makubwa . Udahili wa wanafunzi wa vyuo ukaongezeka. Vyuo vikajengwa , viwanja vya ndege vikajengwa , jiji la Dsm ,Arusha ,Mwanza yakastawi kwa majengo mazuru mazuri. Mahoteli mengi ya kitalii , Safari za nje zikawa nyingi kwa viongozi. Mara paaa katiba mpya.Watu wakajua amekuaja masiha aliyeswa kuwa amechaguliwa na Mungu mwenyewe.
Tukajua hii itakua ndiyo dira ya CCM ,kumbe ilikua ni dira ya muda tu ya awamu hiyo kwa utashi wake tu.

Awamu ya Nne ikapita na dira yake ya muda.


Sasa tupo awamu ya tano na dira ya tano tangu uhuru ,chama kikiwa ni kile kile. Tuombe Mungu wakubali kuweka dira ya Taifa ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.
 
Absolutely; kwani tangu wakati wa kampeni na hata baada ya kuchaguliwa Magufuli sijasema lolote ambalo linaonesha kuwa CCM imebadilika.
Well said,
Sijasema kushindwa kwa "utekelezaji" wa sera; bali kushindwa kwa 'sera" zenyewe. Yaani, ni 'substantial failure" ya sera za CCM ndio chanzo hasa cha umaskini wa Watanzania.

Siyo kukosekana kwa raslimali, siyo kukosekana kwa uwezo, fedha, mipango au hata raslimali watu; bali ni uwepo wa sera ambazo zimeshindwa kuyainua maisha ya WAtanzania. Kwamba hakuna sera hata moja ya CCM ambayo imefanikiwa na ikasifiwa kwa kufanya vizuri na kuinua maisha ya watu wetu. NONE.
Umeona?! Kumbe tatizo lako wewe sio utekelezaji (ambapo kulikuwa hakuna watekelezaji) ambapo tungesema you're now comfortable kwa sababu CCM imepata mtekelezaji!!! Tatizo lako wewe ni sera mbovu za CCM ambazo zimeshindwa! Na kwa maana hiyo, unampigania kiumbe aliyekuja kupigania kikamilifu sera mbovu na zilizoshindwa!!!

Sasa ikiwa CCM ambayo ilikuwa na uwezo wa kumkosoa Mwenyekiti/Rais wake tu ilikuwa totally failed what about CCM ambayo haina uthubutu wa japo kukohoa mbele ya mwenyekiti wake?! CCM ambayo kwavile mwenyekiti wake ametaka mwaka 2020 awakilishe yeye bila kupingwa na mwanachama yeyote hata kama ni kwa kiini macho; nayo imekubali kubadili katiba ili asimame bila kupingwa yule anayeamini kwamba yeye ndie mwenye uwezo kuliko yeyote yule (hivi uliwahi kusema hii ni sifa mojawapo ya madikteta enh?)!!!!!
 
Sijasema kushindwa kwa "utekelezaji" wa sera; bali kushindwa kwa 'sera" zenyewe. Yaani, ni 'substantial failure" ya sera za CCM ndio chanzo hasa cha umaskini wa Watanzania.

Siyo kukosekana kwa raslimali, siyo kukosekana kwa uwezo, fedha, mipango au hata raslimali watu; bali ni uwepo wa sera ambazo zimeshindwa kuyainua maisha ya WAtanzania. Kwamba hakuna sera hata moja ya CCM ambayo imefanikiwa na ikasifiwa kwa kufanya vizuri na kuinua maisha ya watu wetu. NONE.

Siyo Sera ya Elimu
Siyo sera ya Maji
Siyo sera ya Ajira
Siyo sera ya kodi/uchumi
Siyo sera ya uwekezaji
Siyo sera ya ubinafsishaji
Siyo sera ya ulinzi na usalama (kwanza hii haipo technically)
Siyo sera ya utawala bora
Siyo sera ya madini
Siyo sera ya nishati
Siyo sera ya mazingira
Siyo sera ya Utalii
Siyo sera ya "kilimo"
Siyo sera ya afya

Sera zote zimeshindwa.

Sasa sijasema hazijajaribiwa au kwamba hazijawahi kuwa na mafanikio madogomadogo ya hapa na pale la hasha nitakuwa si msema kweli. Shule zimejengwa, vyuo vimejengwa, barabara zimejengwa n.k Lakini ukizichukua sera zote na kuziweka kwenye mizani ya kubadilisha maisha ya mamilioni ya watu wetu utaona kuwa sera hizo zimefeli. Ukishatambua hili ni rahisi kuona kuwa wanaojaribu kufanya CCM waboreshe sera zilizoshindwa wanafanya zoezi litakaloshindwa.

Hutaki?
je hivi sasa hizo sera ndio zimeweza ? Usaliti ni laana mbaya sana !
 
Well said,Umeona?! Kumbe tatizo lako wewe sio utekelezaji (ambapo kulikuwa hakuna watekelezaji) ambapo tungesema you're now comfortable kwa sababu CCM imepata mtekelezaji!!! Tatizo lako wewe ni sera mbovu za CCM ambazo zimeshindwa! Na kwa maana hiyo, unampigania kiumbe aliyekuja kupigania kikamilifu sera mbovu na zilizoshindwa!!!

Sasa ikiwa CCM ambayo ilikuwa na uwezo wa kumkosoa Mwenyekiti/Rais wake tu ilikuwa totally failed what about CCM ambayo haina uthubutu wa japo kukohoa mbele ya mwenyekiti wake?! CCM ambayo kwavile mwenyekiti wake ametaka mwaka 2020 awakilishe yeye bila kupingwa na mwanachama yeyote hata kama ni kwa kiini macho; nayo imekubali kubadili katiba ili asimame bila kupingwa yule anayeamini kwamba yeye ndie mwenye uwezo kuliko yeyote yule (hivi uliwahi kusema hii ni sifa mojawapo ya madikteta enh?)!!!!!
Akija kujibu hili nistue mkuu .
 
Mabutu Sseseko alijenga uwanja wa ndege mkubwa kijijini kwao Cheto..ooh sorry Kijijini kwao Lisala ila sasa hivi ile runway ya uwanja wanakijiji wanaanikia udaga
 
Mzee Mwanakijiji , Mwalimu alipoona nchi haiendi tena kwa misimamo yake kiungwana kabisa akasema hawezi kugeuka jiwe akatangaza kung'atuka!!

Na wewe nakushauri kwa flip-flop na U-turn unayoipiga kwa kasi sana katika haya mapambano ya fikra ni bora ung'atuke tu!. La sivyo kalamu yako ya kale itakuhukumu sana!

Sasa hivi uko loyal kwa mtu na si principles tena!!
 
Back
Top Bottom