Kushindwa kwa sera za CCM ndio chanzo cha umaskini wa Watanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kushindwa kwa sera za CCM ndio chanzo cha umaskini wa Watanzania!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 21, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sijasema kushindwa kwa "utekelezaji" wa sera; bali kushindwa kwa 'sera" zenyewe. Yaani, ni 'substantial failure" ya sera za CCM ndio chanzo hasa cha umaskini wa Watanzania.

  Siyo kukosekana kwa raslimali, siyo kukosekana kwa uwezo, fedha, mipango au hata raslimali watu; bali ni uwepo wa sera ambazo zimeshindwa kuyainua maisha ya WAtanzania. Kwamba hakuna sera hata moja ya CCM ambayo imefanikiwa na ikasifiwa kwa kufanya vizuri na kuinua maisha ya watu wetu. NONE.

  Siyo Sera ya Elimu
  Siyo sera ya Maji
  Siyo sera ya Ajira
  Siyo sera ya kodi/uchumi
  Siyo sera ya uwekezaji
  Siyo sera ya ubinafsishaji
  Siyo sera ya ulinzi na usalama (kwanza hii haipo technically)
  Siyo sera ya utawala bora
  Siyo sera ya madini
  Siyo sera ya nishati
  Siyo sera ya mazingira
  Siyo sera ya Utalii
  Siyo sera ya "kilimo"
  Siyo sera ya afya

  Sera zote zimeshindwa.

  Sasa sijasema hazijajaribiwa au kwamba hazijawahi kuwa na mafanikio madogomadogo ya hapa na pale la hasha nitakuwa si msema kweli. Shule zimejengwa, vyuo vimejengwa, barabara zimejengwa n.k Lakini ukizichukua sera zote na kuziweka kwenye mizani ya kubadilisha maisha ya mamilioni ya watu wetu utaona kuwa sera hizo zimefeli. Ukishatambua hili ni rahisi kuona kuwa wanaojaribu kufanya CCM waboreshe sera zilizoshindwa wanafanya zoezi litakaloshindwa.

  Hutaki?
   
 2. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  MM, hizo "sera" kwa kuanzia hazieleweki hata kwa "viongozi" wa ccm wenyewe. Kwa mfano MKUKUTA ni zao la yule mchumi wa Latin America (unfortunately sikumbuki jina lake kwa sasa). Kina Mchemba na Nape wamo humu, watuthibitishie kama ninachosema si kweli. Ndio maana fedha nyingi zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa hizo "sera" huishia kwenye makongamano na semina (unakumbuka semina "elekezi" za Ngurdoto?) kwa watu wale wale - namfahamu mtu aliehudhuria semina za aina moja zaidi ya mara 10 - na hivyo utekelezaji unaishia hapo.

  Unakumbuka ziara za mawaziri "kuelezea uzuri wa bajeti mikoani"? Ccm ina utaratibu wa kupeana uongozi si kwa competence ya mtu ball kwa kujuana - how can you explain watu semi illiterate kuwa wajumbe wa NEC ambayo inadaiwa kuwa ndio chombo cha juu cha kuratibu sera na utekelezaji wake?
   
 3. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  HIZI SERA ZINATEKLEZEKA TUU KAMA TUKIBADILI KATIBA YETU NA IWE NA NGUVU ZA WANANCHI KULIKO WANASIASA. kama tukifanikiwa kunyang'anya madaraka ya raisi na kugawa kwa bunge na mahama kuu kweli kila mbunge au waziri au mkuu wa mkoa atwajibika ipasavyo kupita tutegemeavyo.

  Pili lazima tupende tusipende adhabu ya kifo kwa wahukumu uchumi na wala na watoa rushwa lazima itumike kujenga na kulinda uchumi wetu. Adhabu ya kifo ni muhimu sana kupita kiasi. Lazuna Ikumbukwe kuwa Tanznaia ina wanasiasa waongo na walaghai sana kupita Nigeria.

  wewe ona tuu Luhanjo wakati ule wa kesi ya David Jairo. sasa tusipoweka adhabu ya kifo kwa wanasiasa waongo, basi twiga wengi sana watapelekwa uarabuni na mikataba ya madini haitasaidia wananchi bali wajanja wachache .
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  hata sera yao ya uongo imeshindwa pia.
  sera pekee zilizofanikiwa ni
  1, sera za siasa za majitaka
  2, sera ya ufisadi
  3,sera ya udini
  4, sera ya ukabila
  (hazikuwepo kwenye ilani yao, ila kwenye utekelezaji wa ilani yao ndo zikajitokeza kwa nguvu zaidi, kwa kasi zaidi na kwa ari zaidi)
   
 5. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Mzee Mwanakijiji,

  Sera moja tuu nimeona imetekeleza ipasavyo. Nayo ni kuwatukana wayahudi bila ya kosa kwa miaka 20! sera hii ya tanzania kununua ugomvi wa myahudi na mpalestina na kuufanya ni kilio cha nchi nzima kuwalilia wapalestina, kweli ilifikia kipindi ilifanikiwa sana wakati wa chama chashika hatamu.

  na bado serikali mpaka leo haitaki kuweka ofisi ya ubalozi tel aviv eti ndugu zetu wakipalestina bado hawako huru!! sasa jiulize, kasumba hii inasaidia nini ktk kujenga uchumi? mimi kweli nampatia hongera mzee Kenyatta kwa msimamo wake wa kuwapenda wayahudi na kuhakikisha Kenya inakomba kisawasawa investment nyingi za myahudi ili wakenya waneemeke kiajira, elimu na biashara. sasa hivi shilika la ndege za marekani limeanzisha direct flight from USA to Nairobi. China inawajengea mpaka ma overpass ya nguvu katikati ya Nairobi. Israel ina mahoteli ya kitalii mengi mengi tuu na wakenya wanapata ajira za nguzu humu.

  Kwa kifupi nataka kusema Tanzania iachane na kasumba ya kujifanya inajua sana kusaidia vyama vya ukombozi. Kasumba hii sisi kama taifa hatuna CV ya nguvu ya kutambia. tuweke mkazo ktk kujenga uchumi na siyo kutafuta masifa ya kiungwana, eti sisi ni wana huruma!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hivi unajuwa maana yake hiyo au unajipachikia tu ili mradi uonekane umeandika Kiingereza?
   
 7. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania bado tuna kazi ndefu sana maana hata hao wanaohubiriwa hizo sera hawafahamu hata maana yake, nakumbuka mfano kuna mtu aliulizwa MKUKUTA ni nini alishindwa hata kuelewa, hivi kweli mtu kama huyo itakuwa rahisi kwenda kushirikiana naye katika kutekeleza sera za huo mkukuta? Mie nadhani kinachotakiwa kila wanapotaka kuanzisha kitu chocgote ni bora wakawekeza zaidi katika kuwaelimisha juu ya hilo jambo
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sera kwa maana ya sera zipo tena nyingine ni nzuri sana. Lakini utekelezaji ndio umekuwa shida. Na huu ndio ugonjwa wa serikali ya CCM. Ni wazuri sana wa kuandika na kuweka makabrasha makabatini. Ndiyo, kuna sekta kadhaa haziko vizuri kisera lakini nyingi wanazo sera. Kwa mfano kwenye uchumi, MKUKUTA hasa ule MKUKUTA I (sasa hivi tuko kwenye MKUKUTA II) una make sense kabisa. Unaongelea uchumi mpana unaoegemea kwenye 'pro-poor policy, na fiscal discipline. Na kuna malengo kwa kila sekta, viashiria (indicators), na malengo yake yanaoana kabisa na Millenium Development Goals (MDGs); elimu, maji, afya ya mama na mtoto, utawala bora, usawa wa kijinsia etc.

  Na huu MKUKUTA unatokana na National Developmement Vision 2025. Kenya walifuata baadae sana wakaandaa Vision yao 2030. (Prof Humphrey Moshi wa UDSM anaweza kufafanua zaidi maana alikuwa kwenye timu iliyoandaa MKUKUTA).

  Nchi kama Brazil zimepiga hatua kwa kufuata pro-poor policy kama ambavyo MKUKUTA ulikusudua. Kwa kifupi, theoritically, Tanzania wana sera nzuri kwenye mambo kadhaa, shida ni usimamizi/utekelezaji. Na unapokuwa na sera ambayo haifuatwi is just as bad as having nothing!

  NB: Pro-poor policy ni pale unapokuwa na sera inayolenga kuinua watu wa daraja la chini na kati, mitaji midogo midogo i.e SMEs. Hakuna nchi yeyote inayoweza kupiga hatua bila kuimarisha daraja la kati (middle class). Hakuna. Hawa ndio wengi, ndio wazalishaji wakubwa, ndio wanaotoa ajira kwa wingi maana hawahitaji mtaji mkubwa au very specialised skills, na kama watu wengi wanakuwa na chanzo cha kipato i.e ajira au kujiari maana yake wataweza kununua (hata kama ni nyanya) hivyo consumption inaongezeka.

  Mkapa alianza vizuri, lakini sijui aliingiwa na pepo gani mchafu akageuza ikulu sehemu ya biashara zake. Hapa ndipo alipopoteza mwelekeo. Na sioni ni kwa vipi CCM inaweza kurekebisha mambo maana wote wamedakia mtindo wa kugeuza ofisi za umma kuwa sehemu zao za biashara. Mfumo mzima ni wa kufumua. Huwezi kuweka viraka maana matobo ni mengi mno.
   
 9. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Nina uhakika anakijua alichokiandika both on English and Kiswahili. Na ni reflection ya mambo halisi, kitu ambacho wewe usingependa kisemwe/kiandikwe- japo ninaamini kuwa hata wewe mwenyewe unajua ni ukweli ila huwezi kukiri hadharani.
   
 10. Michese

  Michese JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nadhani ufumbuzi ni kuiondoa ccm madarakani then ndio sera zitatekelezeka
   
 11. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Kama vipi mwanakijiji mchane Ribosome kwa uzi kidhungu! Nawe Ribosome kwani wewe ni mngreza? hebu tohoa 'kujuwa' na 'kujua' 'ilimradi, ili mradi na alimradi'
   
 12. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  MZEEE TULIA BWANA TUKOKWENYEMCHAKATO WA KUTEKELEZA HAYO,
  TUMEFANYA VYEma kunachangamoto kadhaa tuu,
  tupeni kamuda kidogo tutamaliza haya!
   
 13. S

  Shembago JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sioni logic ya kuchambua hii topic maana sera za CCM hazitekelezeki! Sio mimi ila ni kauli ya mtu anayesadikika ndani ya magamba kwamba bado safi alipokuwa Rais wa TZ na mwenyekiti wao!
   
 14. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ila kushindwa kwa sera na kushindwa utekelezaji kuna ka-uhusiano fulani. Ukweli ni kwamba sera za CCM hata wana CCM wenyewe hawazijui. Hutungwa na wataalam wa elimu ya siasa pale UDSM, na kupelekea wagombea wao wakariri na kuzisoma siku za kampeni.
   
 15. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,468
  Likes Received: 6,761
  Trophy Points: 280
  Dah,Umecomment kama KIKWETE anaongea vile
   
 16. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Khaaa maneno haya kama ya Jakaya..
   
 17. T

  TOWASHI JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ingependeza kama ungeelezea maana yake na kuonyesha jinsi gani imewekwa kimakosa katika hiyo sentesi. Otherwise kamata huu usemi, utakusaidia siku za usoni. A silent fool is counted wise
   
 18. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  NIKWELI TUNAPATA CHANGAMOTO NYINGI SANA, EUMEJENGA MADARASA TUNACHANGAMOTO ZA WALIMU
  TUMEJENGA BARABARA TUNACHANGAMOTO ZA UHARIBIFU WA BARABARA
  TUMEJENGA HOSPITALI TUNACHANGAMOTO ZA WAUGUZI,
  Maji tunachangamoto za miundombinu
  Ajira tunachangamoto ya watu kukimbia na mabilion ya jk
  kodi/uchumi tunachangamoto ya fedha za bandia
  Tunajitahidi jamani hata kama changamoto zipo
  na kumbukeni!
   
 19. Freeland

  Freeland JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 14,468
  Likes Received: 6,761
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha,Sasa wapi mmefanikiwa ndugu KIKWETE,Ambapo hakuna any other Changamoto?
   
 20. MANI

  MANI Platinum Member

  #20
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Nice one !
   
Loading...