Uchaguzi 2020 Kushindwa kwa maandamano ya CHADEMA na ACT-Wazalendo ni ushahidi wa wazi kuwa ushindi wa CCM hauna dosari zozote

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,891
2,000
Wadau, amani iwe kwenu.

Watu hawashiriki kwenye maandamano kwa kushawishiwa. Maandamano ni utashi wa mtu na hushiriki tu kwa kuwa ameguswa. Maandamano ya kushawishiwa kwenye mikutano na waandishi wa habari ama kwenye mitandao ya kijamii siku zote hayafanikiwi.

Wananchi wakiguswa hata utumie vifaru huwezi kuwanyamazisha. Maandamano ya CHADEMA na ACT Wazalendo hayakuwa na hisia za wananchi bali yaliitishwa na watu waliokosa ulaji kupitia sanduku la kura.

Wananchi wanajua wazi kuwa Ushindi wa CCM ni wa halali hivyo wameamua kuwapuuza waandaaji wa maandamano hayo. Maandamano ya CHADEMA na ACT Wazalendo hayakuwa na hisia za wananchi bali yalisukumwa na genge la watu lililokuwa linapigania maslahi binafsi.

Hivyo tunahitimisha kuwa Ushindi wa CCM ni halali kabisa na wananchi wameamua kuwaadhibu CHADEMA na ACT Wazalendo kupitia sanduku la kura na kupitia maandamano feki.

Hongereni sana Waheshimiwa Wananchi. Ninyi ni zaidi ya Wale Wajumbe wa CCM. Mmetuheshimisha Watanzania. Mmewatia adabu CHADEMA na ACT Wazalendo kupitia sanduku la kura na kukataa maandamano yao
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
15,531
2,000
Achaneni na wapinzani, leteni maendeleo ya vitu na watu. Pandisheni mishahara na madaraja ya watumishi wa umma, hela ziingie kwenye mzunguko.

Acheni biashara ifanywe na private sector ili kuleta mzunguko wa hela mtaani, hakuna haja kila mradi wa serikali ujengwe na JKT au TBA. Mambo ya kuwakamata wapinzani hayasaidii maendeleo
 

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
307
1,000
Wewe endelea kutetea ujinga na Ighondo wenu huyo aliyekuondoa mkuku mkuku. Huna lolote unachotetea wala hakipo moyoni mwako umeichukia CCM tangu huyo mng'oa kucha akuondoe na kuta zako 12. Kimsingi huna jipya umekua kijana wa hivyo hovyo sana. Wasalimie huko Chamwno unakotaftia ugali wako
 

niachiemimi

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
3,073
2,000
Kwenye kampeni.
Nikishindwa uchaguzi, nitawaingiza wananchi barabarani.
Baada ya uchaguzi hata mwenyewe ameogopa kuingia barabarani. Kwa ujumla siasa za Lissu kwenye kampeni zilikua ni sanaa za kuwaletea raia matatizo. Kuvuka ziwa kwa mtumbwi, mara kuwatukana polisi, amzodoe Magufuli ni.
 

Bendanda

JF-Expert Member
Jun 25, 2020
323
500
Maandamano ya kwenye mtandao tu hayo! Hakuna kuandamana field kila mtu anaangalia mkate wake, ukidhurika hao viongozi hauwezi kuwaona, akili za kuambiwa changanya na zako.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom