Allien
JF-Expert Member
- Jul 6, 2008
- 5,546
- 1,861
Viongozi na Wakuu wote hapa nyumbani JF Forums!
Kwa niaba yenu wote tunapenda kuihakikishia serikali kuwa JF si mahali tu pa kumkoma nyani na kuibua maovu ya serikali na jamii kwa ujumla, bali pia ni mahali ambapo ushauri mbadala unaweza kutolewa juu ya yale yote ambayo serikali imekuwa haifanyi vizuri.
Kwa kuanzia kuna hili la ATC (Shirika ka Ndege Tanzania) na TRL (Shirika la Reli Tanzania). Ni ukweli usiofichika kuwa serikali imeshindwa kuyaendesha au kuyasimamia mashirika haya.
Ufuatao ni ushauri wa bure kwa serikali nini cha kufanya ili kuyanusuru mashirika haya yaweze kujiendesha kwa faida. Ushauri wa ziada naomba wana JF tuendelee kuutoa katika thread hii.
Kwa kumbukumbu ya haraka na kwa mujibu wa Mkurugenzi mtendaji wa ATC, SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATC), litapata hasara ya sh milioni 300 kila wiki kutokana na kusimamishwa kwa huduma za ndege zake. Kwa maoni yangu huenda ikawa ni zaidi ya hapo kama utazingatia matumizi ya kutoka kila Idara za ATC na malipo ya wafanyakazi nk. TRL nayo nadhani inaelekea kaburini maana hata mishahara kulipa ni kwa tabu tu. Ningeshauri serikali ifanye makuu yafuatayo:
- Mambo mazuri hayataki haraka. TRL na ATC inafaa zijipange upya. Kwanza ni vema mikataba yote isiyo na maslahi kwa shirika na taifa ikavunjwa mara moja. Hata kama itatugharimu, lakini tunaweza kujiunda upya kwa ufanisi zaidi.
- Ufanyike Upembuzi yakinifu haraka sana kwa kushirikiana na timu ya wataalamu wazalendo kutoka ndani ya nchi na consultants kutoka mashirika yaliyobobea katika masuala ya uendeshaji wa safari za anga na reli. Serikali iyafanyie kazi haraka mapendekezo yenye tija baada ya kuyafanyia tathmini.
- Utashi wa serikali unatakiwa katika kuyaokoa mashirika. Kwanza uwekwe uongozi makini sana na pia staff wafanyiwe vetting upya wabaki wale wanaoweza kumudu kuyaendesha mashirika kijasiliamali. Serikali iwekeze mitaji ya kutosha kwa kuweka priority. Kama ilivyofanikiwa kuanzisha chuo kikuu cha Dodoma kwa muda mfupi wa miaka miwili tu chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 10,000 na kukipita chuo kikongwe UDSM, serikali inaweza kuyaokoa mashirika haya ili mradi isafishe uozo wote ndani ya mashirika haya.
- Baada ya miaka michanche ya kujiendesha kwa faida, serikali iuze baadhi ya shares zake DSM Stock Exchange Market.
Naomba wenye ushauri zaidi tuongezee . . .